Ugomvi wa Jirani na Mke/Mchepuko wake, Ulivyonigombanisha na Mke wangu

Mnawatoaga wapi wanawake waropokaji?
Kwenye suala la mahusiano, mwanamke mwenye mdomo usio na breki kwangu hanaga nafasi.
Kusaidia majirani ni kuzuri lkn usiwe peke yako unaweza kuchomwa kisu ukawaacha wao wanakulana
😀😀😀angeenda ageuziwe yeye kivao watu huwajui wagombane usiku wa manane ujifanye kiherehere kwenda kusuluhisha
 
Yaani una-suggest kuwa majirani wanagombana na wewe huna mazoea nao halafu ukimbilie kichwa kichwa? You are not serious! Kwa taarifa yako unaweza kuuawa mapema sana. Kuna kisa kimoja kilitokea, jamaa alikimbilia ugomvi wa jirani ile kuingia ndani akalimwa shaba na ilikuwa bahati hakufa. Na mbaya zaidi yule mwanamke aliyekuwa anapigwa alikuja ku-side na mumewe na kudai jirani aliingia bila kubisha hodi wakadhani ni mwizi.
 
Si mchezo kuna kipindi niliwahi ingilia ugomvi tena ulikuwa Mwanamke na Mwanamke, ile kesi ilitafsiriwa vibaya mno.

Ikaonekana walikuwa wanapigana kwa sababu yangu ilihali siwafahamu kabisa yani.
Niliwakuta tu njiani wanadundana.
Ulifanya vizuri sana. Jirani unayeweza kukimbilia ugomvi wake kwa haraka ni yule ambaye una mazoea naye. Bora hata ufikishe habari kwa balozi wa shinda kuliko kujiingiza kwenye ugomvi wa mume na mke usiye na undugu naye au urafiki au ukaribu.
 
Acheni umbeya wewe na mkeo kuingilia umbeya wa watu ungeenda wangekugeuzia kibao, niliishi sehemu mke na mume daily kupigana nilikuwa siamulii na wakidundana kesho mahaba ka yote kimoyo moyo nilikuwa nasema uaneni tu mtajiju nani wakuwa shahidi wa jamhuri
 
Ila haya maisha yana mambo mengi sana kwa kweli.

Kuna mahusiano yanapitia nyakati ngumu sana.
 

Unajua kusoma na kuandika? Nimesema angafanya chochote, hata kutoka sebuleni, kukaa na mwanamke, ku symphasize, na kutoa taarifa taarifa police....

Sijui mnajibu mkiwaza nini, ingekuwa ni mimi kwenye hiyo case nisingetoka, na ningelala na mke kwa amani sana bila gubu, ni art tu ya kuishi na mwanamke.

Kama kutoka nje si sawa na sio usalama, jamaa angetoka kitandani akakaa na huyo mwanamke akamwelewesha asingeelewa?
 
We jamaa ni mimi kabisa. Am that kind of person sipendagi kuingilia mambo ya watu. Hasa ugomvi. Yaan ugomvi mnaanzisha wenyewe halafu mimi niingilie, hell no. Mi uwa hata nikikuta watoto wanagombana, sijishughulishi nao kabisa. Naendelea na mambo yangu. Wazichape, atakayeshindwa awe na adabu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kama kawaida yao, mwanamke anaweza kumuona wa maana sana muuza bucha alimuongeza kifundo kimoj cha nyama na akadharau aliyempa 10k akanunue kilo yahio nyama. Wanawake wanatabia za kulipuka from small things halafu akakomalia kabisa. Huna baya mkuu, nilipoanza kusoma uzi nilikua najiambia mimi nisingeenda kuamulia wala nini hadi mwisho wa uzi na wewe hukwenda. Ww ni kama mm tu.

We mpuuze tu atalala ataacha. Ukimpa attention na kuanza kutaka yazungumzike ndio atakaza fuvu ku prove kuwa una hatia. Mwache awe analala chumba kingine, usuulize, kuwa normal kabisa kama hakuna jambo lolote. Atajirudi mwenyewe tu
 
Unajua kusoma na kuandika? Nimeeema angafanya chochote, hata kutoka sebuleni, kukaa na mwanamke, ku symphasize, na kutoa taarifa taarifa police....
Usinichekeshe tena. Jirani akigombana kwake, wewe ukikaa sebuleni kwako na kusikitika na mke wako utasaidia nini? Alichafanya ndicho alichatakiwa kufanya. Mtu huna ukaribu naye, hujui ni nini imetokea halafu uite polisi?
 
Mf angeenda. Akakutane na kisu kinarushwa, kimpate cha uso.

Angemlaumu nani?
Mke wake angebaki na majuto kwanini kamwambia aende.
Mfano wangeuwana pale, angejiskiaje watu wamepoteza maisha na hakufanya chochote?
 
Alitaka uwe mstari wa mbele kama wale mgambo wanaotangulizwa vitani ili wafe wa kwanza.

Kahama chumba muulize anachotaka, yaani wewe ukafe kisa ugomvi usioujua.

Miaka ya nyuma kidogo hapo mbezi walimpiga mbaba risasi kwenye saa nne usiku, hata polisi hawakuonekana mpaka hali ilipotulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…