Ugonjwa wa Figo wazidi kuwatesa vijana, Hospitali zapokea wanne hadi 9 kila siku

Pombe chafu na feki serikali ndio imezifumbia macho kabisa[emoji849]
Tunathamini sana kodi kuliko maisha ya watu wetu. Tunasubiri nini kuvifungia hivi vinywaji wakati vijana wetu walio nguvu kazi ya taifa wakiteketea? Itafika wakati tutakuwa tumechelewa kwani mdharau mwiba mguu huota tende.
 
Leo kwenye kipindi cha kina zembwela chumvi,mende na ndimu wamezungumzia pia kuna chumvi mpya inatumika sana sasahivi hiyo inapiga moja kwa moja kwenye figo
Ipi hiyo mkuu, hebu iweke wazi watoto wetu tutawaua bila kujua aiseeee[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mkuu leta makala utatusaidia wengi
 
Tunasubiria hilo bandiko, kiukweli kila ninaponunua matunda roho huwa inaniuma nahisi kabisa yamejaza sawa. Basi tu vile matunda ni muhimuu.
 
Kuna jamaa yangu anazipiga zile kubwa za Mo extra mil 400 kama 6 hivi kwa siku
 
Kwa nn serikali isifanye utafiti kujua sababu ya mfumuko huu wa tatizo la figo kwa sasa? Ama hatujaona kama ni tatizo la dharura kiasi cha kuhitaji utafiti??
 
Ukiondoa pombe kali vyakula vingi sana sahizi vimejaa sumu ..

Kila kilimwacho ni mbolea tu ..
Mbolea na madawa ya magugu, viwatilifu vya kuuwa wadudu shambani vinatumika ovyo Sana.
Ogopa kachumbari humo kuna sumu nyingi vitu vikipikwa vinaweza pungua nguvu ya sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…