Ugonjwa wa ghafla na changamoto ya kutembea

Ugonjwa wa ghafla na changamoto ya kutembea

Ugonjwa wa ghafra na changamoto ya kutembea no 2

Baada ya kuzinduka nikaambiwa ni siku sita tangia nifike hospital pale

Nabaada ya hapo niliendelea kutibiwa hospital hapo kwasiku nyingine tatu za ziada

Lakini huku ndugu walikuwa wanaendelea kufanya mchakato wa tiba mbadara na hatimaye waka mpata mtaaramu

Baada ya kumpata mtaaramu Huyo ukafanyika mchakato wa kunitoa hospital hatimaye Mambo yaka kaa sawa nikatoka

Kuna swali nilijiuliza na hatimaye sikusita kuuliza kwamba mbona Hali yangu haija tenga maa na ndugu Wana taka nitoke mapema hivi?

Mdogo wangu akanijibu hivi wewe brother unavyo ona ugojwa huu niwa kawaida?

Skumjibu kitu zaidi nikamuuliza Kuna mpangonwowote baada ya kutoka hapa kwani?

Akanijibu tuta angalia tukifuka nyumbani

Nikawaomba watu wote watoke mle ndani isipo kuwa tu mdogo wangu aliye nifwata

Baada ya yeye kubaki peke yake nikamuuliza hivi...

Mdogo wangu wewe nimwanaume Sasa nataka unijibu Kama mwanaume .

Je! ni Nini au niugonjwa gani umenifikisha hapa hospital?

Mdogo wangu aliye nifwata akasema wengi Wana amini lakini Mimi siamini

Wengi wanahofia ukijua utaugua zaidi na hata kufa lakini Mimi siamini

Nikamuuliza Nina ukimwi?

Akani jibu hapana Kaka wanasema una pressure ya kushuka na kisukali lakini Mimi najua huna huo ugonjwa ebu tutoke hapa utaniamini kaka

Tukatimiza taratibu zote pale hospitali kisha tukaludi nyumbani


Nabaada ya hapo ndugu wakalibu wakawa wamefika pale nyumbani akiwemo.

mama,baba,mjomba,mdogo wangu wa kunifuata,bada mdogo na shangazi


Baada ya mda kidogo wakaniambia Wana mazungumzo namimi namimi sikusita kuwa sikiliza

.hivyo nikamwambia mke atupishe kidogo tuna mazungumzo

Mke akatoka baada ya kutoka mazungumzo yakaanza Kama ifwatavyo..

Alianza baba kwakusema. Tumekutoa hospital sionkwasababu umepona hapana

. Ila nikwasababu tume pata njia nyingine ambayo tuna amini itakuponya

Akaendelea kusema ulipo kuwa hospital mdogobwako alikuja aka niambia ugonjwa wako sio wa kawaida umelogwa

nami nilipo muuliza umejuaje akanielekeza nika mwelewa vizuli Sana

na hata mtu wakutu saidia amepatikana na tayali hata malipo ya awali tume kwisha kumtumia tayali na
safari inaanza Leo jioni saa kumi na moja

baada ya hapo Mimi nikawauliza kwamba Kuna haja gani ya kwenda kwa wataaramu wakati ugonjwa umejulikana na masharti yake Yana julukana?

Kabla mzee haja jibu mdogo wangu akadakia kwa kusema

ugonjwa wako sio wa kawaida umelogwa na mtu alkiku Loga huloga hata njia za kujiokoa

kwahiyo kuanzia Sasa jukumu la afya yako nila kwetu Kama family hivyo unapaswa kutuamini na kufuata maelekezo sio vinginevyo Kaka angu..

Baada ya kuona jinsi watu wanavyo uchukulia ugonjwa wangu najinsi walivyo hangaika siku zote nikiwa hospital

nikajikuta Sina jinsi ila kuwaamni tu ndugu zangu Hawa wa damu
.
Kikao Kika fungwa saa kumi na moja ikatimia simu ikapigwa kwa mtaalamu kwamba ndiyo tunakuja

Mtaalamu akatoa ratiba nyingine kwamba inatakiwa tuondoke saa Saba za usiku

pasipo mtu kujua Kama tuna ondoka kwani tayali majilani walikuwa Wana jua kwamba naumwa

Utaratibu ukafwatwa saa Saba ikafika gali ilikuwa imelala nyumbani na driver pia

tukaaa mshana Nami nikaamshwa

Nilipo pewa nguo nivae namke wangu nilijikuta nashindwa hata kuvaa mwili mzima unauma

Nikapewa viatu pia nikashindwa kuvaa kwani miguu ilikuwa inauma sana na imeanza kuvimba tayali


Nilicho kifanya nikumwambia achukue ndala azilushue kwenye kwenye gali na shati Nita vaaga mbeleni huko

Kisha akanitoa akiwa ameni shikilia mpaka kwenye gali

tukaingia Mimi,mama,mdogo wangu, na mzee wangu/baba

mke akabaki nyumbani kwani nayeye nilikuwa nimeanza kumtilia Shaka hasa nikiangalia mazingila ya kuumwa kwangu
.
safari inaanza mpaka Sheri ambapo tuka weka mafuta ya laki na hamsini safari inaanza

cha ajabu kadri nilipo kuwa nauacha mji nilizidi kujiskia hafadahali

nakingine tulipo fika katikati ya safari tukagundua hatuku beba dawa hata moja Kati ya zile tulizo pewa hospital kwa ajili ya kuzitumia nyumbani Yani dawa za kutuliza skali na presha

hapo ukatokea ubishi baadhi wakisema tuludi tuka chukue dawa na baadhi wakisema tusonge mbele

nahapo ndipo nilipo tamka kwamba hakuna kuludi nyuma Kama nimetembea nusu safari bila dawa naweza fika safari mzima bila dawa


safari ikaendelea mpaka saa tatu za hasubuhi tukawa tumefika eneo la tukio/kwa mtaaramu mwenyewe
.
baada ya kushuka nikabebwa mgongoni na driver wangu mpaka ndani kwani tayali nilikuwa siwezi kutembea

baada ya kufika pale ndani tukamkuta mama mmoja mwenye wastani wa miaka 37 mpaka 38

akatupokea nakutuelekez mahali pa kukaa Kisha akasema

poleni na safari poleni Sana mgonjwa wenu ugonjwa wake nimeuona niwa kawaida kwahiyo atapona" Ila atakaa hapa miezi miwili au mmoja na nusu

kila mtu akabaki anashangaa
.
akaendelea kusema kwasababu mmevuka geti lile mmeingia hapa amepona

Kisha akasema Tena bila longolongo nyingi inabidi tuanze kazi lakini kwanza inabidi muone nikipi kilicho msibu mpaka akaumwa Kisha tuingie kwenye tiba

ndipo akasema niwangapi wataenda kuona isipo kuwa mgonjwa tu ndiye haruhusiwi

ndipo baba,mama,na mdogo wangu wakamjibu sisi tuta enda kuona

wakapewa dawa wakanywa Kisha wakapelekwa kwenye chumba Cha kuona huko walikaa zaidi ya masaa ma tatu Kisha wakatoka

Walikuwa wamechoka ikabidi walale kwa mda Kisha waamke waoge ndipo wakaitwa nakuanza kutoa maelezo juu ya kile walicho kuwa wamekiona

Ndipo wakaanza kuzungumzia Kwamba..

wameona nilikuwa nakumywa pombe sehemu nikatoka kwenda kukojoa

baada ya kutoka Kuna mwanamke akamiminia dawa kwenye pombe hiyo Kisha akanywa kidogo nakuiweka pale ilipo kuwa

.na baada ya kuludi Mimi nikanywa ile pombe bila kujua
.
Lakini pia wakasema wame mwona rafiki yangu akijificha nyuma ya mwanamke mweupe

ambaye rafiki Huyo alikuja kunitembelea hospital nikiwa nimelala na aling'ang'ana Sana nihamishwe hospital ile kwa kudai hapakuwa na matibabu sahihi lakini ndugu walimkataa

na baada ya kumchunguza vizuli mwanamke yule ikaonekana nimwana mke aliye Wai kuwa mke wangu miaka 14 iliyo pita mungu akijalia ntaleta habari zake hapa

mwanamke Huyo tulisumbuana mno mpaka tukafikishana jera na ndipo nikaamua kumtema

Sasa kumbe ndiye aliye kuwa staring kwenye mchezo wote wa kuwekewa dawa kwenye pombe

Na mpaka kuumwa kwangu lakini pia sio hivyo tu nilishuhudiwa nikiwa kwenye jeneza nachapwa fimbo za kutosha na kiongozi akiwa ni mama chanja huyo wa zamani
.
Kumbe kipindi nasumbuana na mwanamke Huyo rafiki yangu alikuwa ndiye anaye mmiliki pasipo Mimi kujua

Nilijikuta naanza kugundua mengi juu ya mke wangu wa zamani na rafiki yangu ambayo skuya jua baada ya kufika pale na kuyaskia Yale

Lakini lingine na kubwa zaidi walimwona mwanamke Huyo na kundi lake lisilo pungua watu 30 wamemshika mtoto ambaye nime mwacha nyumbani na mke wangu

Huku wakiwa Wana mpeleka kwenye jeneza nililo kuwa nime wekwa mimi

Na baada ya yote hayo ndipo mtaaramu akasema hivi Hilo ndiyo tatizo ambalo mmelifanya

Sasa Kuna changa Moto moja hapa mme mleta mgonjwa hapa lakini mme mwacha mke na mtoto nyuma

Je! Hamuoni kwamba baada ya maadui zenu kumkosa huyu killing machine wata ona ni Bora waivamie familia iliyo baki nyumbani?

Kisha aka malizia kwa kusema..

inabidi mtoto na mama wachukuliwe Mara moja waje hapa ili waanze matibabu pamoja na killing machine

kinyume na hapo tuta okoa baba tuta poteza mtoto

Ndipo Nika mtazama driver wangu nakumuuliza unasemaje ndugu yangu?

Akanitazama kwa huruma Kisha akasema Kaka skuchangia chochote kwenye tatizo lako

Sasa Leo Nina maombi mawili Kama ifwatavyo..

Kwanza naomba uniruhusu nikamchukue shemeji na mtoto huko tuliko toka haraka iwezekanavyo

Pili nipo tayali niendeshe gali yako miezi miwili bule na usini lipe kitu Kama sehemu ya mchango wangu kwako kwani

siku fikilia Kama takuwa namatatizo kiasi hiki

Ndipo Mimi nikamjibu Hilo lakwanza nakubaliana na wewe lakini Hilo la pili haliwezi kutokea

Baada ya hapo ikabidi Mimi,na mama,tubaki kwa mtaaramu
Huyo

Lakini pia mdogo wangu pamoja na mzee waanze kuludi mjini Kisha driver kuwa tayali kuja na mke na mtoto wangu pale kwa mtaaramu

Safari ikaanza ya kuondoka kwao huku Mimi na mama tukiwa pungia mikono...

Itaendelea










.
SIjakuelewa! Kikao cha familia kujadili afya yako ukaamulu mkeo atoke asiwepo! Kwanini?.
 
Inabd mtoa mada kwanza audhihirishie uma kwamba either hii story ni ya kweli au ni ya kutunga then ndo tuendelee
 
Hilo linaitwa shambulio la kimwili.

Mwili umevamiwa na adui.Na inatokea mtu akipata mlango.
 
Ugonjwa wa ghafra na changa Moto ya kutembea no 3/mwisho....

Baada ya Mimi kubaki na pamoja na mama yangu nilifanyiwa tiba nzito ndani ya lisaa limoja nikajikuta mwili unaanza kujiwa na nguvu

Kiza Kika ingia na Usiku wa manane ulipo ingia Hali ilikiwa ngumu Sana kwangu kwani nilijiskia mwili mzima ukiuma

Nilikuwa nikilala chali Basi mgongo uliniuma vibaya mno"

na nikilalia tumbo Basi kukunja shingo ilikiwa shida nyingine iliyo nitesa Sana

Kila kiungo Cha mwili wangu kiliuma Kwa maumivu makali kuanzia shingo mpaka kidole Cha mwisho Cha mguu wangu

Baada ya kukucha mnamo saanane za mchana mke na mtoto wakawa wamefika tayali na baada ya mda mfupi tiba zikaendelea

Cha ajabu nikwamba nilifika sitembei lakini ndani ya siku nne nilianza kutembelea fimbo

Nilianza kupata tumaini lankuishi Tena nikaanza kupata tumaini lakuungana Tena na familia yangu

Nyayo zangu zilizo kuwa zime vimba zikaanza kupungua taratibu maimivu ya mapaja na mgongo na misuri ya miguu viakaamza kuisha kadri siku zilivyo zidi

Taratiibu nikaanza kutembea Tena japo skuwa natembea umbali mlefu nikama robo ya uwanja wa mpila hivi

lakini nilimshukulu mungu kwa Hilo kwani halikuwezekana kabla

Kadri nilivyo zidi kupata nafuu ndivyo nilivyo jitahidi kufanya mazoezi zaidi na hatimaye baada ya mwezi mmoja na wiki mbili nikawa tayali naweza mpaka kukimbia

Nakumbuka Christmass ya mwaka 2024 na mwaka mpya ya 2025 nime sherehekea nikiwa huko

Hatimaye baada ya mwezi mmoja na wiki mbili ndipo mtaaramu wangu akaniambia Sasa waweza kwenda upo tayali

Nikatajiwa gharama za matibabu sikuamini Ila naamini Kama ingekuwa hospitali Basi ningepigwa pesa ndefu

Kwani gharama ambayo niliitumia pale hospital zile siku sita za mwamzo ilikuwa imeizidi gharama niliyo kuwa nime tajiwa na mzee wangu/mtaaramu pale nyumbani

Mungu mwema nikalipia gharama na ulipo fika mda wa kuondoka safari ikaanza Kisha nikaludi nyumbani na kazini

Baada ya kufika kazini watu walini shangaa kwani niliondoka nikiwa hoi lakini nililudi nikiwa mwenye
Afya tere

Niliondoka nikiwa na langi Kama majivu yaliyo lowa nikiwa hospital kwa muujibu wa mashuhuda lakini nililudi nikiwa nang'aa

Hakika sioni neno zuli lankumshukuru mungu kwa haya aliyo nitendea

nilikuwa wakufa Mimi mungu kanipa nafasi nyingine Tena ya kuishi

Sasa nime pona kabisaa hasa ninapo malizia kipande hiki Cha mwisho nimepona kabisa kabisa siumwi kabisa ndugu zangu

Japo changa Moto ninayo iona kwa sasa ningozi ya miguuni kwenye ugoko mpaka chini ya unyayo na viganjani kubanduka pasipo maumivu yoyote

Na nime jalibu kuwasiliana na mtaaramu ananiambia mwiliwako ndiyo unaludi usjali Wala usiogope

Kwankumalizia naomba niwa kumbushe ndugu zangu Wana jf kwamba..

Shetani yupo na mungu yupo lakinini pia

watu wanao kufa/mizimu wapo wanaishi

..Kingine nikwamba..

kwenye maisha hasa maisha ya mjini ili uishi maisha malefu Basi unapaswa uchague Kati ya haya yafwatayo

1)mungu au shetani

2)mchungaji au mganga

3)uokovu au uovu

Na Kama utachagua Kati ya hayo Basi hakikisha unayatumikia kweli kweli

Kinyume na hapo wewe nimnyama Poli/mnyama asiye na mfugaji/mlinzi tu


ambaye unaweza ukawi ndwa na yeyote mda wowote na pasiwepo na mtu wa kuhoji kwanini umetendwa hivyo

ndugu yangu chagua moja mda bado unao


...Mwisho,,,,
 
Back
Top Bottom