Ugonjwa wa Masundosundo mwilini na sehemu za siri (Genital & Skin Warts)

Ugonjwa wa Masundosundo mwilini na sehemu za siri (Genital & Skin Warts)

Mi nilisikia kitunguu saumu ni effective katika kutibu maradhi ya virus kama flu na wengine
 
wicalumtata mkuu hapa JF kuna uzi unahusu huu ugonjwa wameuelezea kwa makini sana sina ujuzi wa kuweka link ila just nenda sehemu ya ku-search thread andika genital and skin warts na uzi utakuja hakika tatizo lako litaisha kwa utayoyakuta uko.
 
Last edited by a moderator:
Hapana havifanani, uvimbe unaoota nyuma ya sikio ni tofauti na huu, uke unaitwa Keloid. mara nyingi matibabu yake ni kukata na kuchoma sindano ya betamethasone kwenye eneo liloathirika. hii hutokana na reaction ya mwili. mara nyingi tafiti zinaonyesha kadri mtu anvyotoga masikio akiwa mkubwa ndo chance ya kupata keloid inakuwa kubwa. Hivyo tunashauri kutoga masikio kwa watoto wakiwa bado wachanga ndo risk ya kupata keloid inapungua. naomba uwaeleweshe na wengine.
Nakutakia kila la Kheri

Tafadhali naomba unielekeze kuhusu hiyo Keloid yaani vyote viwili vinafanyika kukatwa na kuchomwa sindano au kimojawapo, naomba unipe contact ya hospital inayofanya vizuri nataka nimpeleke mdogo wangu yaan kinamboa na yeye alitoboa akiwa mkubwa kikatokea hicho kinundu ila ndo hatujui pa kuanzia kukitoa Mupirocin
 
Last edited by a moderator:
Mimi ninalotatizo hili

Tumia dawa hii haina madhara yoyote na bei rahisi sana ..achana na madawa yote uloambiwa hapo...nenda pale sokoni kariakoo stendi ya mwenge kuna maduka ya madawa asili..nunua mafuta ya castrol oil ya asili na si ya viwandani wanauza shs 2000 chupa ya nusu lita..yana kiarufu kidogo cha kukera ila usijali mana unatafuta tiba..pakaza ile sehemu zenye hizo warts mara 2 kwa siku asubuhi na usiku kabla kulala..vitapona kwa muda wa wiki 1 mpaka 2 na havitorudi tena..
 
Hivi ndio sunzua ama ni ugonjwa tofauti?
 
Nilikuwa nacho mkononi nikakikata nawembe
 
Habari rafiki, natumaini mnaendelea vizuri leo napenda nizungumzie tatizo la kutokewa vinyama katika sehemu za siri na sehemu mbalimbali za mwili, (Masundosundo /vigwaru /genital warts & skin)
~MASUNDOSUNDO /VIGWARU /GENITAL WARTS & SKIN NI NINI?

~NI vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri, vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), maeneo yanayozunguka haja kubwa na sehemu mbalimbali za mwili,
~Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana (SEXUAL TRANSMITTED INFECTION) STI)

CHANZO CHA TATIZO HILI
~Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao HUMAN PAPILLOMA VIRUS ( HPV) hata hivyo Kuna Aina tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanaosababisha Masundosundo katika sehemu tofauti kama vile mkono, mgongoni, mguuni nk pia HPV huweza kasababisha saratani ya shingo ya kizazi(CARCINOMA OF THE CERVIX) kwa wanawake, na pia huweza kusababisha saratani ya sehemu ya haja kubwa (ANAL CANCER) kwa jinsia zote mbili
~Ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo watu wenye wapenzi wengi, wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo na haja kubwa, wajawazito, watumiaji wakubwa wa sigara na pombe, watu wenye upungufu wa kinga mwilini wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huu.

DALILI ZA MASUNDOSUNDO
~mgonjwa wa tatizo hili hutokewa na vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye katika maeneo tofauti (MFANO HALISI TIZAMA KATIKA PICHA) ingawa wakati mwingine huwa ni vidogo kiasi cha kutoweza kuonekana kwa njia ya kawaida.
~mgonjwa kupata ganzi maeneo yaliyozungukwa na Masundosundo
~kutokwa na uchafu mzito sehem za siri na kuwashwa kupita maelezo
~kutokwa damu ukeni mara baada ya kufanya tendo la ndoa
NOTED :mwanaume huwa anachelewa kupata dalili na huwa na uwezekano mkubwa wa kuambikiza wenza wao

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU
~matibabu ya tatizo hili hupatikana kirahisi iwapo tatizo halijachelewa kupatiwa tiba, matibabu hutolewa kwa kufuata utaratibu wa Majibu yaliyopatikana katika vipimo mbalimbali, matibabu hayo huweza kuwa ya kuviondoa vinyama kwa kufanya operations au kutumia dawa, hata hivyo njia ya operation sio nzuri sana kwasababu huweza kutengeneza madhara zaidi na uwezekano mkubwa wa kupata kansa hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa ambazo zitatibu na kuondoa tatizo hilo na mgonjwa kupona kabisa ila cha kuzingatia ni kwamba ugonjwa huu ni wa kuambikiza hivyo inashauriwa wenza wote kupata matibabu hata kama atajihisi hana dalili yoyote ni vyema akafanya vipimo ili kujihadhari kabla ugonjwa haujaleta madhara zaidi.

~Waswahili wanasema bora kinga kuliko matibabu hivyo ni vyema ukajiepusha na ugonjwa huu kwa kuepuka yafuatayo
EPUKA KUWA NA WAPENZI WENGI
EPUKA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
ACHA ORAL SEX UKISHINDWA BASI KUWA NA MPENZI MMOJA TU AMBAYE NDIO UNAWEZA KUMNYONYA SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZINGATIA MAPENZI UJUZI LAKINI AFYA YAKO NI MALI ZAIDI WADADA/WAKAKA WENGI MMEKUA MKITAKA KUWARIDHISHA KILA MNAOKUTANA NAO KIMWIL KWA KUWANYONYA SEHEMU ZA SIRI KITU AMBACHO KINAKUWEKA KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU NA KANSA YA KOO.

EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, SIGARA NA POMBE KUPITA KIASI
NOTED :NDUGU RAFIKI ugonjwa huu una madhara makubwa unaweza kusababisha kansa ya kizazi, kansa ya uume, kansa sehemu ya haja kubwa NK hivyo hakikisha unapata matibabu ya uhakika iwapo una tatizo hili au ikiwa hauna jitahid kujiepusha na vihatarishi vya ugonjwa huu


Kwa maoni na ushauri Niandikie whatsapp/sms
+255 714 206 306
Blog: Tovuti ya Uelimishaji na Ushauri wa magonjwa sugu, kisukari, shinikizo la damu, kansa, ugumba, upungufu wa nguvu za kiume n.k.
Email : khalidgugu@gmail.com
Makala hii imeandaliwa na
Khalid Gugu
USISAHAU KUSHARE, KUCOMENT, KULIKE
 
Ugonjwa huu kwa mwanamke huanza kuonyesha dalili kwa muda gani?
 
Tiba Ya Skin Warts Ni Dawa Ya Kupaka Iitwayo WARTS REMOVING PAINT Au WARTS REMOVING SOLVENT.
Matumizi
Nipaka Ktk Sunzua Chache Na Zote Husagika Na Kupukutika Bila Madhara.Mimi Nilikuwa Nazo Mwili Mzima Na Nilipona Kwa Dawa Hiyo Na Gharama Ilikuwa Tsh.7000/=tu
Inapatikana wapi hii dawa
 
Masundosundo ni ugonjwa gani?

Masundosundo ni ugonjwa wa ngozi unaosababisha uoto mgumu kwenye ngozi wenye umbo mithili ya mboga iitwayo koliflawa (cauliflower). Ugonjwa huu husababishwa na kirusi kiitwacho HPV-Human Papilloma Virus.
phototake_rm_hand_warts.jpg


Nini husababisha masundosundo kwenye ngozi?

Chanzo cha ugonjwa huu ni kirusi kiitwacho HPV-Human Papilloma Virus. Kuna aina zaidi ya 100 ya kirusi HPV, aina nyingi ya HPV huwa na madhara madogo kwa binadamu. Baadhi ya aina za kirusi hichi huweza kusababisha kansa mfano kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake.(type 6,11,16,18)

Kirusi hichi humwingia mwanadamu kupitia sehemu za ngozi zenye mikato (broken skin).

Aina za masundosundo:

Kuna aina nyingi za ugonjwa huu ila kwa urahisi tunaweza kuzigawanya katika aina mbili kuu; masundosundo ya ngozi(skin warts) na masundosundo ya sehemu za siri(genital warts).

Masundosundo ya ngozi huwa na dalili kwenye ngozi ya kawaida na masundosundo ya sehemu za siri huambatana na uoto sehemu za siri.

916058-16464641-a72d-4abf-ad8c-d5dcd90162ae.jpg



Tiba ya misundosundo:

Ukiachana na mwonekano wa ngozi, ugonjwa wa misundosundo hauna madhara kwa binadamu. Baadhi ya aina ya kirusi HPV husababisha kansa ila uoto wa misundosundo hauna madhara.

Tiba yake ni kuondoa uoto huu kwa njia mbalimbali. Dawa aina ya Salicylic acid husaidia kuondoa masundosundo kwenye ngozi. Pia tiba ya cryotherapy ambayo uoto wa masundosundo hugandishwa kwa gesi yenye joto dogo.

Kinga ya misundosundo:

Chanjo ya kirusi HPV itwayo Gardasil imetengenezwa kwa ajiri ya kinga ya kansa isababishwayo na baadhi ya aina ya kirusi HPV.

Pia ethanol 90% husaidia kupunguza maambukizi ya kirusi HPV kwenye ngozi.


Dr Luhaja Nginila,MD
 

Attachments

  • upload_2016-6-13_21-24-5.png
    upload_2016-6-13_21-24-5.png
    19.7 KB · Views: 379
  • upload_2016-6-13_21-24-38.png
    upload_2016-6-13_21-24-38.png
    19.8 KB · Views: 300
Mkuu pole sana.

Tiba mbadala ninayoifahamu mimi na iliniponya nilipokuwa secondari ni utomvu wa ile miti (vines) inayopandwa kama hedge na ukikata kitawi kinatoa utonvu mweupe. Huu mti siujui jina lake lakini nadhani wakuu MziziMkavu , FaizaFoxy et al. wanaweza kutusaidia. Hii tiba inafanana na tiba ya utomvu wa papai bichi aliotoa mkuu Nyamgluu

Hivi karibuni swahiba wangu nae aliathiriwa na haya maradhi. Daktari akamuelekeza kununua Dr. Scholl's Wart Remover. (Hii sio dawa ya prescription ni off-the-counter). Aliweka hizi plasta na katika kipindi cha wiki moja zile warts zilidondoka mpaka mizizi. Active ingredient ya hii wart remover ni Salicylic Acid (40%). Sasa kama huwezi kuipapata hii Dr. Scholl's Wart Remover nadhani unaweza kusaga asprin ambayo ina hii Salicylic Acid.

Hapa pa kusaga asprin naomba tuwaulize madaktari ushauri wao.
Riwa watu8 georgeallen AshaDii ZeMarcopolo Mupirocin, et al.

Singida wanaiita minyaa.
 
Back
Top Bottom