Black7
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 367
- 116
Wew umenenaHuu uzi type nyng za ngiri zimeongelewa
(still zinaongelewa)lkn hii kitu "EPIGASTRIC HERNIA" Sijaona izungumziwe kabisa au hii iko vp wataalamu,ebu igusieni nayo kwa faida ya wengne,!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wew umenenaHuu uzi type nyng za ngiri zimeongelewa
(still zinaongelewa)lkn hii kitu "EPIGASTRIC HERNIA" Sijaona izungumziwe kabisa au hii iko vp wataalamu,ebu igusieni nayo kwa faida ya wengne,!!
Yes inawezekana,, reducible herniaWanabodi habari za asubuhi.<br />Kwa anayefahamu naomba ushauri au ufafanuzi wa nini kitakuwa kinanisumbua kulingana na maumivu nitakayoyaeleza hapa.<br /><br />Huwa napatwa na maumivu makali upande wa kulia wa tumbo, maumivu haya huwa kama inavuta misuli kwa ndani kuelekea juu tumboni lakini kuna muda huwa yanashuka kwenye misuli ya korodan hii hutokea kila siku asubuhi kuazia saa kumi au kumi na moja mpaka mida ya saa moja hivi au saa mbili.<br /><br />Nilienda kupiga ct scan ikaonekana hakuna tatizo.<br />Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Je hii inaweza kuwa hernia?Natanguliza shukrani
Mkuu hii inaweza sababisha kupoteza hamu ya papachu?Yes inawezekana,, reducible hernia
Ndo nn sasa sielewiHenia
Ni ugonjwa wa wanyama pori ndiyo maana hukufundishwa! Una undugu na ngiri kwani?
Ile ni sunna bhana zinafichwa ili kujikinga na baridi ila jua likitoka nzo paaap zinatokelezea! Ni kaugonjwa amazing kama kombolela maana kanajumuisha kujificha kwa hizo ndude ulizozitaja![emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] wacha fujo zako
ugonjwa huu unazibeba kirodani nje zinakoning'nia na kuzificha ndani haswa nyakati za baridi na kusababisa maumivu makali sana. Kwa wanawake sijui labda wale wanawake waliotunukiwa korodani wanaweza kuupata [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847][emoji847]
KeWewe ni ke au me ndipo ujibiwe
[emoji3][emoji3][emoji3]kumbe sna undugu na ngiriNi ugonjwa wa wanyama pori ndiyo maana hukufundishwa! Una undugu na ngiri kwani?
Ile ni sunna bhana zinafichwa ili kujikinga na baridi ila jua likitoka nzo paaap zinatokelezea! Ni kaugonjwa amazing kama kombolela maana kanajumuisha kujificha kwa hizo ndude ulizozitaja!
Wee ulijuaje ama ushahidi wako ni wa kusikia?zinapotea kabisa yaani panakuwa flat . Hizo ndude nazo zina mambo
Hapa sna swali nashukuru mkuuu
NAMNA AMBAVYO MTU ANAPATA UGONJWA WA NGIRI (HERNIA)
Home » Health Blog » Articles » NAMNA AMBAVYO MTU ANAPATA UGONJWA WA NGIRI (HERNIA)
KUWA NA MALARIA BAADA YA KUMALIZA DOZI YA MALARIAFAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI
TATIZO LA NGIRI (HERNIA)
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).
Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).
Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.
Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.
Chanzo: Tanzlife Company Limited
ambavyoanawezaherniakupatamtunamnangiritatizo
October 13, 2013 ArticlesJackson Nyabusani57 Comments
57 Comments
innocent urassa
January 28, 2015 at 7:45 pm
dawa ya ngiri ni ipi
REPLY
admin
January 28, 2015 at 8:06 pm
njia mojawapo inayotumika kutatua tatizo hilo ni upasuaji, hivyo inategemeana na ukubwa wa tatizo
REPLY
Arnold kajuna
January 29, 2015 at 6:32 pm
Wa dauhu niambieni
REPLY
Arnold kajuna
January 29, 2015 at 6:33 pm
Kuna haina ngapi za ngiri
REPLY
admin
January 29, 2015 at 7:09 pm
aina au jina la ngiri inategemeana na sehemu katika mwili ambapo ngiri hiyo imejitokeza, hivyo hakuna jibu la moja kwa moja kuna zipo aina ngapi. Ila ni aina nyingi zipo….
REPLY
abubakari mkingiye
February 26, 2015 at 8:16 am
je!kuna njia mbadala ya kutubu ngiri tofauti na upasuaji na yapi madhara ya ngiri…?
REPLY
admin
February 26, 2015 at 5:47 pm
matibabu kwa njia ya upasuaji hayafanyiki kwa kila ngiri, bali hutegemeana na ukubwa au uzito wa tatizo, na pia pamoja na kumkosesha mtu Uhuru kwa uvimbe kuonekana mkubwa pia wakati mwingine MTU hupata Maumivu makali mno.
REPLY
Annanjohn
March 24, 2015 at 1:44 pm
Shukrani za dhati kwenu wapenzi wa lugha,wasomi,walio na moyo mwema na madaktari kwa kutujuza.mola awafariji
REPLY
admin
March 24, 2015 at 5:33 pm
Nasi tunawashukuru na Mungu azidi kuwapa Afya njema.
REPLY
festo
June 3, 2015 at 2:51 pm
je ngiri inaweza kutokea sehemu za siri
REPLY
admin
June 3, 2015 at 2:57 pm
Inawezekana pia.
REPLY
kaja
June 7, 2015 at 1:37 pm
ni athali zipi za ugonjwa wa ngili?
REPLY
admin
June 7, 2015 at 5:16 pm
pamoja na kuonekana kama uvimbe na kukufanya ukose amani, pia wakati mwingine MTU hupata Maumivu makali, na mwanaume huweza kushindwa kufanya tendo la ndoa.
REPLY
flora
June 23, 2015 at 8:53 am
je kwa mtu anayefanya mustebation kuna uwezekano wa kupata ngiri?.
REPLY
admin
June 26, 2015 at 1:22 pm
Haiwezi kuwa ni sababu kuu ya MTU kupata ngiri, ila kitendo hicho chaweza kuwa na athari nyingine kwa MTU.
REPLY
frank hossa
June 26, 2015 at 1:02 pm
mm natatizo korodan moja ilivimba alaf ikarudi ikawa ndogo xana nayo ni ngiri?
REPLY
admin
June 26, 2015 at 1:28 pm
Labda ilivimba kwa muda/siku ngapi na ilirudi baada ya kufanya nini au kutumia Dawa gani?.
REPLY
ezrah
July 6, 2015 at 7:46 am
ngiri inaweza kusababisha mwanaume kutokupata mtoto? namaanisha kupunguza uwezekano wa kuzalisha?
REPLY
admin
July 6, 2015 at 5:24 pm
Endapo tatizo ni kubwa litamfanya mwanamme ashindwe kufanya tendo la ndoa na hivyo kutamfanya ashindwe kumwezesha mwanamke apate ujauzito.
REPLY
efraim
August 7, 2015 at 3:20 am
Je, tatizo la hernia ya tumbo
linaweza kuua kabisa mbegu za mwansume
REPLY
Jackson Nyabusani
August 21, 2015 at 10:18 am
Tatizo la hernia huweza kumfanya mwanamme apate maumivu makali yatakayomfanya ashindwe kushiriki tendo la ndoa. Hernia ya tumbo haiuwi nguvu za kiume.
REPLY
Vicky
October 18, 2015 at 11:28 am
Mwanamke akijamiana na mwanaume wenye ugonjwa wa ngiri anaweza pata athari yoyote huyo mwanamke au kupata magonjwa
REPLY
Jackson Nyabusani
October 24, 2015 at 11:08 am
Hakuna athari au ugonjwa ambao mwanamke anaweza kuupata kwa kujamiiana na mwanamme mwenya ngiri.
REPLY
John Kimaro
November 4, 2015 at 4:19 pm
Je ni wakati gani mtu mwenye ngiri anapata maumivu??
REPLY
Fred
November 5, 2015 at 5:05 pm
Na inapotokea muwasho ktk mishipa ya uume kuwaka moto wakati Wa haja ndogo pia inasababishwa na nn?
Na Tina yake n mini?
REPLY
Fred
November 5, 2015 at 5:07 pm
Na inapotokea muwasho ktk mishipa ya uume kuwaka moto wakati Wa haja ndogo pia inasababishwa na nn?
Na Tiba yake ni nini?
REPLY
renald
January 30, 2016 at 4:53 pm
vp wakubw naomb nisaidiwe tatizo la mbegu za kiume kutoa haruf inasababishwa nanin
REPLY
Jackson Nyabusani
February 15, 2016 at 6:36 pm
Mara nyingi miongoni mwa vitu vinavyochangia haruf hiyo ni aina ya vyakula ambavyo mwanaume huvitumia. Hivyo ni vyakula.
REPLY
Rehema nelson
February 19, 2016 at 8:33 pm
Mimi nimepimwa ninayo juu ya tumbo au kwenye moyo,natakiwa opp na imevimba sana nani naogopa nakunywa za kienyeji nifanyeje nasikia kukabwa.
REPLY
Jackson Nyabusani
June 19, 2016 at 8:01 pm
Pole, ni vyema ukafuata ushauri huo wa kufanyiwa OP, kutofanyiwa kutapelekea tatizo kuwa kubwa zaidi.
REPLY
Elias mabula
June 11, 2016 at 3:46 pm
Je huu ugonjwa unaweza kuupata kwa kuambukizwa au vipi wadau
REPLY
Jackson Nyabusani
June 19, 2016 at 7:34 pm
Ugonjwa huu siyo wa kuambukiza
REPLY
experius gaudensi
June 15, 2016 at 5:14 pm
je kuna tahadhi yoyote inatolewa na shirika la afya juu ya ugonjwa huu hatari?
REPLY
Jackson Nyabusani
June 19, 2016 at 7:33 pm
Elimu za Afya hutolewa kujikinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa huu
REPLY
einhard
July 14, 2016 at 12:45 pm
Naomba kujua tiba mbadala zaidi ya Operation?
REPLY
Jackson Nyabusani
July 15, 2016 at 9:24 pm
Tiba hutegemeana na uzito wa tatizo, kwa ambaye yupo katika hali ya ulazima wa operesheni ni vyema upasuaji ukafanyika, tofauti na hivyo hakuna njia ya kuondoa hali hiyo.
REPLY
don don
July 18, 2016 at 10:16 pm
Habari ya kazi
Hivi kama kolodan zinakua na maumv fln hv kama ganzi yan kama umezigonga hivi na maumivu hayo yanakua kwa mda alaf yanaavha na mda mwingine hanaweza kufika hadi masaa mawili yakaacha ila kazi. Zote zinafanyika bila shida na ni maumv yan kama ganz fln hv na kuvutavuta kwambali.tatzo ni kitu gani hapo.?
REPLY
Jackson Nyabusani
August 12, 2016 at 8:44 am
Maumivu sehemu za korodani yaweza kusababishwa ni vitu tofauti tofauti mfano, kwa watu wanaojihusiha sana na mifugo chanzo chaweza kuwa ni jamii ya bakteria, brucella, ampapo kupitia michubuko katika mwili wa mtu bakteria hawa huweza kuingia katika mzunguko wako wa damu na hatimaye kukusababishia maumivu katika korodani na ili kuweza kugundua ni lazima vipimo vya maabara vifanyike ili kupata uhakika. Nakushauri ufike katika kituo cha tiba kwa ajiri ya uchunguzi na matibabu. Pole sana.
REPLY
Jimmy
August 8, 2016 at 9:45 am
Mimi Nina pata maumivi chini ya kitovu,afuu tumbo linanguruma,mwisho korodani ya kushoto inaanza kuuma,na kunakuwa na ka kitu kama ka uvimbe flani hivi.Je yaweza kuwa Ngiri japo mashine napiga kama kawa.
REPLY
Jackson Nyabusani
August 12, 2016 at 8:29 am
Pole, ni vizuri ukaonana na daktari ili kuweza kufanya uchunguzi na kupata uhakika zaidi. Daktari katika kituo cha tiba chochote unaweza kuonana naye ili kufanya uchunguzi huo.
REPLY
ephraim ndelwa
August 9, 2016 at 9:23 am
je endapo nitakuwa nimefanyiwa op naweza tena kuendelea na tendo LA ndoa iwapo nimepona?
REPLY
Jackson Nyabusani
August 12, 2016 at 8:25 am
Ndiyo, op haitazuia wewe kuendelea na tendo la ndoa.
REPLY
Daniel Kadushi
September 14, 2016 at 3:10 pm
Na mie pia huwa ninapata maumivu makali sana kila nikijamiiana na mke wangu yaan mara ya kwanza kabla sjaoa kalikuwa hakachukui sku nying kupoa lakn sku iz ni kila ninapofanya tendo hilo mara mbili tu kanaanza kuuma sana, je itakuwa tayar tatizo limekuwa kubwaa? ingawa uume husimama kama kawaida
REPLY
Jackson Nyabusani
October 1, 2016 at 8:23 am
Pole…katika hiyo changamoto uipatayo nakushauri wewe pamoja na mwenza wako muonane na wataalamu wa afya ya uzazi katika kituo chochote cha tiba ili kwa pamoja muweze kushauriwa…hii itakuwa na msaada mkubwa kwenu nyote.
REPLY
Bhudagala
September 20, 2016 at 12:12 am
Mimi nina korodani moja, lakini huwa kuna uvimbe unajitokeza upande wa kushoto mwa shina la mashine na halii ni ya toka utotoni. Uvimbe huo huambatana na maumivu flan hivi ya tumbo pamoja na korodani (hiyo moja) kuwa kama inaminywa hivi! Hii ni ngiri? Na saivi aged 24yrs. Msaada please.
REPLY
Jackson Nyabusani
October 1, 2016 at 8:16 am
Nachoweza kukushauri ni kwamba jipange uweze kuonana na daktari katika kituo cha tiba kilicho karibu na wewe, kwani tatizo umekuwa nalo tangu utotoni na pia kuna baadhi ya matatizo ambayo ili kuweza kupata msaada au ushauri mzuri…ni vyema daktari akuone.
REPLY
Barack
November 23, 2016 at 11:11 pm
Mimi Nina tatizo moja..pmb yakulia imeshuka chini alafu imejaa kidogo yaani kama kuna majiivi..alafu niyabaridi.. na nikifanya tendo natoa shahawa nyepesi.
REPLY
Jackson Nyabusani
January 10, 2017 at 7:33 am
Umefanya vizuri kubaini hali hiyo ya utofauti mapema na Nakushauri ufike katika kituo cha tiba ili kuweza kubaini aina ya tatizo ulilonalo ili kuweza kupata matibabu sahihi zaidi.
REPLY
jassone jasper
September 22, 2016 at 7:42 pm
mimi naumwa chini ya kitovu karibu na sehemu ya siri kwa ndani nahisi kama kuna ka upele na muda mwingine napata maumivu alafu yanapotea karibu mwaka mzima na nikigusa nakasikia kwa ndani. je iyo ni hernia?
REPLY
Jackson Nyabusani
October 1, 2016 at 8:12 am
Pole sana kwa usumbufu na maumivu uliyoyapata kwa kipindi chote hicho, aidha ili kuweza kutambua kama ni hernia au lah! ni vyema ukaonana na daktari ili aweze kukuchunguza na kutoa jibu stahiki.
REPLY
Fredinand
November 2, 2016 at 6:17 pm
Tatizo langu ni hapa chini ya kitovu kulia, kunauvimbe umeshuka hadi kwenye mfuko WA korodani. Lakn nikilala chali uvimbe huo wenye ukubwa saizi ya ngumi unarudi tumboni taratibu lakini kila ninapo simama wima tuu uvimbe Hui huchomoza tena. Tatizo hili ni mwaka wanne sasa… Nini madhara yakuchelewa kufanyiwa oparesheni
REPLY
Jackson Nyabusani
January 10, 2017 at 6:39 am
Madhara yake ni pamoja na uwezekano wa uvimbe kuongezeka, nakushauri uwahi matibabu mapema ili kuondokana na usumbufu unaoweza kuupata na madhara ya kiafya.
REPLY
Said
November 12, 2016 at 12:58 am
Hv na ghalama za upasuaji wa ngiri unaweza mufka shiling ngp…?
REPLY
Jackson Nyabusani
January 10, 2017 at 6:31 am
Huduma za upasuaji kiujumla hutegemeana na aina ya tatizo na pia hutofautiana kwa taasisi na taasisi…hivyo ni vyema ukafika katika kituo chochote cha tiba wanapotoa hudua za upasuaji ila nafahamu kuwa siyo bei kubwa.
REPLY
Yasini Haruna
November 22, 2016 at 12:20 am
Shukran
REPLY
Mahmood Mohammed
November 26, 2016 at 11:38 pm
hernia ya leta gesitumboni kweli
REPLY
Jackson Nyabusani
January 10, 2017 at 7:25 am
Hernia huweza kukufanya upate hisia za kuwa na gesi tumboni.
REPLY
Leave a Reply
Your email address will not be published.
Name *
Email *
Website
NEWS / UPDATES
More Videos and Slides will be uploaded time after time
LOCAL WEATHER
Currency Converter
Convert your Currency here:
From:
GBP EUR USD CAD AUD SGD EGP ARS BBD BRL CLP CNY CZK DKK XCD EEK HKD HUF ISK INR IDR ILS JMD JPY LVL LBP LTL MYR MXN NAD NPR NZD NOK OMR PKR PAB PHP PLN QAR RON RUB SAR ZAR KRW LKR SEK CHF THB TRY VEF
To:
GBP EUR USD CAD AUD SGD EGP ARS BBD BRL CLP CNY CZK DKK XCD EEK HKD HUF ISK INR IDR ILS JMD JPY LVL LBP LTL MYR MXN NAD NPR NZD NOK OMR PKR PAB PHP PLN QAR RON RUB SAR ZAR KRW LKR SEK CHF THB TRY VEF
Amount:
OTHER SITES/BLOGS
www.thepharmajournal.com
www.pharmacycouncil.go.tz
www.chezasalama.com
www.jamiiforums.com
www.sikika.or.tz
NEWSPAPERS LINKS
The Guardian
The Citizen
Mwananchi
LOCAL CHANNELS LINKS
ITV
Star TV
CONTACT US
Dar-es-Salaam, Tanzania
+255 762 777580
info@tanzlife.co.tz
tanzlife
ARCHIVES
ARCHIVES Select Month August 2016 (1) February 2016 (1) July 2015 (5) January 2015 (1) November 2014 (2) October 2014 (3) September 2014 (1) August 2014 (1) July 2014 (2) June 2014 (2) April 2014 (1) February 2014 (2) January 2014 (2) December 2013 (1) November 2013 (18) October 2013 (30) September 2013 (18)
FOLLOW US




PAGES
Home
About Us
Contacts
Health Blog
Health Forum
ABOUT US
Tanzlife is the private company aiming to provide health services to the community through hospitals, health centers, dispensaries, laboratories, pharmacies and counseling centers. Already the company is...
[emoji767]2015 Tanzlife - Terms & Privacy | Developed by Adams Digicom

Ama ulimtembelea shem siku moja tule tuball twake kama mpira wa golf tukawa tumetokeka?[emoji3][emoji3][emoji3]kumbe sna undugu na ngiri