Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.Nakuja kwenu wanajamvi kuomba msaada wa mawazo nifanyeje niweze kuondokana na tatizo hili sugu na lililonitesa kwa miaka 22 sasa.
Tatizo hili liligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 hospitalini na nikaanza kutumia dawa na kufuata masharti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuepuka aina fulani za vyakula na madawa na pia kubadili lifestyle.
Nikiri kuwa baada ya muda fulani baada ya kuanza matibabu nilipata nafuu kubwa hadi husahau maumivu ya tatizo hili lakini nilijitahidi kubaki katika masharti yale.
Baadaye tatizo lilianza upya na nikaanza kutumia dawa zile zile nilizotumia awali lakini sikupata nafuu. Nimebadilisha dawa mbalimbali lakini bado tatizo limeng'ang'ania. Baadhi ya dawa ninazokumbuka nilizotumia mpaka sasa ni: CIMETIDINE, RANITIDINE, OMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE, LANSOPRAZOLE na Antiacids za maji kama MILK OF MAGNESIA na RELCER GEL.
Nimewahi pia kutumia dawa za kienyeji kadhaa bila mafanikio. Mfano: Unga wa mbegu ya parachichi, mafuta ya ubuyu, asali mbichi na mdalasini, kuchemsha mmea wa mbigili n.k.
Nimeshawahi pia kupima H.PYLORI TEST mara 2. Mara moja nilikutwa Positive nikapewa HELIGO KIT dozi ya wiki 2 na nikaendelea na lansoprazole kwa wiki 2 zaidi. Nilipopima tena H.PYLORI ikasoma Negative lakini bado nikindelea kuumwa.
Mwaka jana nilifanyiwa kipimo cha OESOPHAGOGASTRODUODENOSCOPY hospitali moja ya rufaa na ripoti ya Daktari ilisomeka: "Multiple wounds found around the duodenum". Nilipewa dawa lakini bado sikuona nafuu kubwa.
Hivi leo nina siku ya 6 natumia TINIDAZOLE, LANSOPRAZOLE NA CLARITHRIMYCIN kwa pamoja na bado sijisikii nafuu yoyote. Maumivu ni makali, tumbo linauma na kutonesha (painful & tender), nikila chakula kidogo tu nasikia tumbo limejaa. Siwezi kulalia ubavu wa kulia tena sababu ya maumivu.
Usiku wa leo tumbo liliniuma sana mpaka jasho likanitoka japo kulikuwa na baridi.
Kwa ufupi nateseka jamani na nimekuja kwenu kama kuna mhanga kama mimi aliyewahi kuugua tatizo hili na kupona au madaktari mliomo humu jamvini mnisaidie jinsi ya kufanya.
Natanguliza shukurani nikiomba radhi pia kwa post ndefu. Nimelazimika kuandika hivi ili tatizo langu lieleweke vema.
ASANTENI!
Mwanajamvi mwenzenu anayeteseka.
Pili pili inaponesha kweli lakini hiyo tiba haishauriwi ni kama vile unaionja sumu... kuna waliojaribu waka enda moja kwa moja kuna waliopona.... pia ufahamu kuna aina mbili za vidonda vya tumbo na hata maumivu na tiba zake ni tofauti, inawezekama tiba hiyo ikawa kwa wale wa aina nyingine akatumia huyu ikamdhuru na kwa maelezo yake vidonda vimemla sanaaaa.Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.
Acha roho mbaya wewe, kwamba hiyo dawa unataka itibu watu wachache kwa nn usiweke watu wote wajue iwasaidie. Roho mbaya na ubinafsi huoPole mkuu.. samahani wewe ni me au ni ke..
Mimi nina dada yangu amesumbuliwa na vitonda toka miaka hyo ya 90s kaja kupona mwaka jana kapona kabisa na dawa yake ni easy ambayo waweza tengeneza mwenyewe nyumbani, huhitaji kulipa hata senti kwake..
Kama ni ke, basi uje pm ntakupa namba yake uzungumze nae, mie pia ntakiwa nishampa muhtasari wa haya..
Ila kama ni me njoo pia pm lakin sintakupa namba yake maana ni mke wa mtu, sasa nisije nikaleta tafarani kwa kutoa namba yake na sijui atajisikiaje pale nitakapotoa namba tena kwa mwanaume.. nitakupa yangu , niyazungumza nae then nitakujulisha kila kitu mkuu..
Pole sana, nina imani mwenyezi mungu atakuafu inshaallah
Mkuu umekurupuka, sijui umeandika haya ikiwa kichwa chako umeegemeza upande mmoja.. nimemwambia kuna dada yangu ambae alisumbuliwa n vidonda vya tumbo kuna daw alitumia na akapona sasa niwaunganishe na wawasiliane wao kama wao maana mimi sijui dawa, ila ni namba ya simu tu ndio ninaweza kumpa..Acha roho mbaya wewe, kwamba hiyo dawa unataka itibu watu wachache kwa nn usiweke watu wote wajue iwasaidie. Roho mbaya na ubinafsi huo
Mie dawa siijui ntashare nanyi nini sasa.. nilichosema ni kwamba aje nimpe mawasiliano nae, kwani akija pm ndio nitawafanya nini, kama ningehitaji kitu mimi ndio ningewafata huko pm kwanza..Ninyi mnao muita inbox kwann msitoe hapa hiyo tiba ili na wengine wanufaike nayo??? huko inbox mnataka kuwafanya nini wenzenu.....
sio vizuri kama unajua kitu flani ukashare kwa wenzio hata baraka zinaongezeka.
Mkuu nimekuja pm kwa tatizo kama la mkuu hapo juu. Vidonda vya tumbo vinaninyima furaha. Usingizi umekuja wa kubahatisha shauri ya maumivu. Naomba unikumbuke nami.Sawa mkuu, nikionana nae tu ntakuja pm mkuu
Mkuu pm yako nimeiona, na nimekujibu kaka, ondoa hofu.. hapa nafunga safari ya kwenda kwake nakupigia uongee nae ndugu yangu.Mkuu nimekuja pm kwa tatizo kama la mkuu hapo juu. Vidonda vya tumbo vinaninyima furaha. Usingizi umekuja wa kubahatisha shauri ya maumivu. Naomba unikumbuke nami.
Na kama ukimuelewa, utawaandikia dawa hapa.Mkuu nimekuja pm kwa tatizo kama la mkuu hapo juu. Vidonda vya tumbo vinaninyima furaha. Usingizi umekuja wa kubahatisha shauri ya maumivu. Naomba unikumbuke nami.
Ni kweli maana wahanga tuko wengiNa kama ukimuelewa, utawaandikia dawa hapa.
Hapo nimekupata kiaina.....nilikuwa sijakumanya kiswanuMkuu umekurupuka, sijui umeandika haya ikiwa kichwa chako umeegemeza upande mmoja.. nimemwambia kuna dada yangu ambae alisumbuliwa n vidonda vya tumbo kuna daw alitumia na akapona sasa niwaunganishe na wawasiliane wao kama wao maana mimi sijui dawa, ila ni namba ya simu tu ndio ninaweza kumpa..
Sasa ulitaka namba ya simu ya dada yangu niiweke hapa hadharani.. humu namba zetu tu hatuweki ndio itakuwa niweke namba ya mtu bila ya mwenyewe kuruhusu, mara zote jitahid kutumia akili zako na si vidole vyako..
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.
Mkuu namba unisaidie hiyo tiba nami ni mhanga wa vidonda vya tumboPole sana nicheck private nikupe dawa alafu utakuja kutoa ushuhuda