Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ukipata tiba tafadhali naomba feedback kwani wenye jii shida ni wengi sana
 
Ulikosea kuanza kutumia madawa yote hayo wakati vidonda vya tumbo hutibika vizuri tu na alternative medicine.
Mie nnavyo leo mwaka wa tano japo havijafikia kunitesa kivile zaidi ya mara mojamoja ,na nikitumia tiba mbadala vinaniacha hata kwa mwezi japo tena hujisahau na kuanza lifestyle hatarishi na hivyo kurudi tena.
Nilipima mara moja tu nikaambiwa ni vidonda tumbo ,mie nikadhani ni appendex,
nikatoa appendex kumbe tatizo halikwisha,
sijawahi kutumia dawa ya hospitali kwa ajili ya vidonda tumbo,
 
Sijui kama utaupenda na kuuzingatia ukweli huu mchungu.

Ganja wengi wanaiita Bangi ni dawa nzuri kwa tatizo lako.. Iwe ni kwa kuvuta au kutumia mbegu zake (unazisaga) au kupika chai ya ganja.. Kama utaivuta sokota ganja kavu (usichanganye na tumbaku).

Wakati unafanya hayo.. Fanya haya pia..
1. Acha kutumia sigara za viwandani. (Fegi)
2. Hakikisha Umekula/Umeshiba muda wote
3.Acha kutumia pilipili au vitu vyenye uchachu.
4.Punguza Stress (msongo wa mawazo)
5.Acha Maziwa na Kahawa.
7.Lala Mapema, Kunywa maji Mengi.. Mengi sana
8.MUOMBE NA KUMTUKUZA MUNGU WAKO.

Aitumiae na Aje Atoe Ushuhuda.
 
Vidonda vya tumbo hua vinaleta complications, complications muhimu ni 1. Perforation.2. Malignant/Cancer.3.Bleeding.Huenda wewe ugonjwa wako umeshaleta complications ambazo matibabu yake sio dawa za kumeza tena bali ni operations. Unatakiwa uende hatua nyingine ya uchunguzi ili kama itabainika unazo complications ufanyiwe operations. Halafu matumizi holela ya madawa mengine yanaweza kuleta madhara makubwa kwa kukinzana ( drug interactions )Epuka matumizi holela ya madawa mengine.Pia elewa kuwa dawa hua zinafeli kufanyakazi na kwako hili tayari limeshakutokea kwa hiyo wewe sasa ni moja kwa moja kwenye hatua ya pili ya matibabu ambayo ni operation. Lakini pia pima HIV kwani ni moja ya kikwazo kikubwa cha kuingilia mfumo wa
tiba na kuleta ugumu katika uponyaji wa magonjwa.
 
Nakuja kwenu wanajamvi kuomba msaada wa mawazo nifanyeje niweze kuondokana na tatizo hili sugu na lililonitesa kwa miaka 22 sasa.

Tatizo hili liligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1995 hospitalini na nikaanza kutumia dawa na kufuata masharti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuepuka aina fulani za vyakula na madawa na pia kubadili lifestyle.

Nikiri kuwa baada ya muda fulani baada ya kuanza matibabu nilipata nafuu kubwa hadi husahau maumivu ya tatizo hili lakini nilijitahidi kubaki katika masharti yale.

Baadaye tatizo lilianza upya na nikaanza kutumia dawa zile zile nilizotumia awali lakini sikupata nafuu. Nimebadilisha dawa mbalimbali lakini bado tatizo limeng'ang'ania. Baadhi ya dawa ninazokumbuka nilizotumia mpaka sasa ni: CIMETIDINE, RANITIDINE, OMEPRAZOLE, PANTOPRAZOLE, LANSOPRAZOLE na Antiacids za maji kama MILK OF MAGNESIA na RELCER GEL.

Nimewahi pia kutumia dawa za kienyeji kadhaa bila mafanikio. Mfano: Unga wa mbegu ya parachichi, mafuta ya ubuyu, asali mbichi na mdalasini, kuchemsha mmea wa mbigili n.k.

Nimeshawahi pia kupima H.PYLORI TEST mara 2. Mara moja nilikutwa Positive nikapewa HELIGO KIT dozi ya wiki 2 na nikaendelea na lansoprazole kwa wiki 2 zaidi. Nilipopima tena H.PYLORI ikasoma Negative lakini bado nikindelea kuumwa.

Mwaka jana nilifanyiwa kipimo cha OESOPHAGOGASTRODUODENOSCOPY hospitali moja ya rufaa na ripoti ya Daktari ilisomeka: "Multiple wounds found around the duodenum". Nilipewa dawa lakini bado sikuona nafuu kubwa.

Hivi leo nina siku ya 6 natumia TINIDAZOLE, LANSOPRAZOLE NA CLARITHRIMYCIN kwa pamoja na bado sijisikii nafuu yoyote. Maumivu ni makali, tumbo linauma na kutonesha (painful & tender), nikila chakula kidogo tu nasikia tumbo limejaa. Siwezi kulalia ubavu wa kulia tena sababu ya maumivu.

Usiku wa leo tumbo liliniuma sana mpaka jasho likanitoka japo kulikuwa na baridi.

Kwa ufupi nateseka jamani na nimekuja kwenu kama kuna mhanga kama mimi aliyewahi kuugua tatizo hili na kupona au madaktari mliomo humu jamvini mnisaidie jinsi ya kufanya.

Natanguliza shukurani nikiomba radhi pia kwa post ndefu. Nimelazimika kuandika hivi ili tatizo langu lieleweke vema.
ASANTENI!

Mwanajamvi mwenzenu anayeteseka.
Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.
 
Aiseee sikutishi ila vidonda vyako vipo stage ya mwisho be careful sana,

Nakupa dawa tatu usidharau kabisa.

Moja, chukua bamia kata kata vipande weka kwenye blender na glass ya maziwa blend kisha kunywa asubuhi kabla hujala chochote na usiku nusu saa baada ya kula.

Najua itakupa shida kumeza ila pambana utanipa mrejesho.

Dawa ya pili, unga wa mbegu za mlonge,
Chukua kijiko kimoja cha unga huo weka kwenye maziwa au uji kunywa, unaweza kuharisha au kutapika au vyote, usijali jikaze endelea kutumia.

Dawa ya tatu ni maziwa mtindi,
ndio glass moja ya maziwa mtindi kila siku asubuhi mchana na jioni, utaleta mrejesho.

Achana na hizo dawa za hospital hakuna tiba bali zinapunguza makali halafu kumbuka unazidi kujaza chemical mwilini.

NB: Kama una kawaida ukisikia maumivu ya tumbo unakunywa maziwa fresh nakushauri acha mara moja, maziwa fresh huzidi kukwangua kwenye vidonda lakini mtindi wale bacteria wake ndio tiba yako.
 
Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.
Pili pili inaponesha kweli lakini hiyo tiba haishauriwi ni kama vile unaionja sumu... kuna waliojaribu waka enda moja kwa moja kuna waliopona.... pia ufahamu kuna aina mbili za vidonda vya tumbo na hata maumivu na tiba zake ni tofauti, inawezekama tiba hiyo ikawa kwa wale wa aina nyingine akatumia huyu ikamdhuru na kwa maelezo yake vidonda vimemla sanaaaa.
 
Ninyi mnao muita inbox kwann msitoe hapa hiyo tiba ili na wengine wanufaike nayo??? huko inbox mnataka kuwafanya nini wenzenu.....
sio vizuri kama unajua kitu flani ukashare kwa wenzio hata baraka zinaongezeka.
 
Pole mkuu.. samahani wewe ni me au ni ke..
Mimi nina dada yangu amesumbuliwa na vitonda toka miaka hyo ya 90s kaja kupona mwaka jana kapona kabisa na dawa yake ni easy ambayo waweza tengeneza mwenyewe nyumbani, huhitaji kulipa hata senti kwake..

Kama ni ke, basi uje pm ntakupa namba yake uzungumze nae, mie pia ntakiwa nishampa muhtasari wa haya..

Ila kama ni me njoo pia pm lakin sintakupa namba yake maana ni mke wa mtu, sasa nisije nikaleta tafarani kwa kutoa namba yake na sijui atajisikiaje pale nitakapotoa namba tena kwa mwanaume.. nitakupa yangu , niyazungumza nae then nitakujulisha kila kitu mkuu..

Pole sana, nina imani mwenyezi mungu atakuafu inshaallah
Acha roho mbaya wewe, kwamba hiyo dawa unataka itibu watu wachache kwa nn usiweke watu wote wajue iwasaidie. Roho mbaya na ubinafsi huo
 
Acha roho mbaya wewe, kwamba hiyo dawa unataka itibu watu wachache kwa nn usiweke watu wote wajue iwasaidie. Roho mbaya na ubinafsi huo
Mkuu umekurupuka, sijui umeandika haya ikiwa kichwa chako umeegemeza upande mmoja.. nimemwambia kuna dada yangu ambae alisumbuliwa n vidonda vya tumbo kuna daw alitumia na akapona sasa niwaunganishe na wawasiliane wao kama wao maana mimi sijui dawa, ila ni namba ya simu tu ndio ninaweza kumpa..

Sasa ulitaka namba ya simu ya dada yangu niiweke hapa hadharani.. humu namba zetu tu hatuweki ndio itakuwa niweke namba ya mtu bila ya mwenyewe kuruhusu, mara zote jitahid kutumia akili zako na si vidole vyako..
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Ninyi mnao muita inbox kwann msitoe hapa hiyo tiba ili na wengine wanufaike nayo??? huko inbox mnataka kuwafanya nini wenzenu.....
sio vizuri kama unajua kitu flani ukashare kwa wenzio hata baraka zinaongezeka.
Mie dawa siijui ntashare nanyi nini sasa.. nilichosema ni kwamba aje nimpe mawasiliano nae, kwani akija pm ndio nitawafanya nini, kama ningehitaji kitu mimi ndio ningewafata huko pm kwanza..

Siwez kuweka namba hapa.. samahanini kwa hilo.
 
Mkuu nimekuja pm kwa tatizo kama la mkuu hapo juu. Vidonda vya tumbo vinaninyima furaha. Usingizi umekuja wa kubahatisha shauri ya maumivu. Naomba unikumbuke nami.
Mkuu pm yako nimeiona, na nimekujibu kaka, ondoa hofu.. hapa nafunga safari ya kwenda kwake nakupigia uongee nae ndugu yangu.
 
Mkuu umekurupuka, sijui umeandika haya ikiwa kichwa chako umeegemeza upande mmoja.. nimemwambia kuna dada yangu ambae alisumbuliwa n vidonda vya tumbo kuna daw alitumia na akapona sasa niwaunganishe na wawasiliane wao kama wao maana mimi sijui dawa, ila ni namba ya simu tu ndio ninaweza kumpa..

Sasa ulitaka namba ya simu ya dada yangu niiweke hapa hadharani.. humu namba zetu tu hatuweki ndio itakuwa niweke namba ya mtu bila ya mwenyewe kuruhusu, mara zote jitahid kutumia akili zako na si vidole vyako..
[emoji124] [emoji124] [emoji124]
Hapo nimekupata kiaina.....nilikuwa sijakumanya kiswanu
 
Mie si daktari niliambiwa pilipili kichàa ni dawa komesha vidonda vya tumbo. Mtanzania mmoja alienda India masomoni akiwa na shida hiyo. Vyakula vya kule vilimshinda maana ni pilipili tupu. Akawa hali sana na shida iliendelea. Hatimaye asife njaa akawa anajilazimisha kula vyakula vilivyojaa pilipili. Baada ya muda wa miezi michache akazoea na sambamba na hiyo akapona vile vidonda. Wanasema watalaam wa Tiba za leo, pilipili inaenda kukausha acids kwenye vile vidonda navyo vinapona. Chunguza ongea na daktari ujiridhishe usijaribu pasipo ushauri wa madaktari. Narudia mimi si mtaalamu nimeeleza nilichosikia. Na kisa hili kilithibitishwa na mtu aliyekuwa nami nikieleza kazi ya pilipili kwa vidonda vya tumbo.

Upo sahihi pilipili inatibu vidonda vya tumbo.
 
Back
Top Bottom