Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Chamomile!

chamomile.jpg
 
nan kakudanganya vdonda vya tumbo havna dawa:dawa ipo ila n sisi tu wabish unaambiwa usinywe soda o kilev na ule kwa mda unaostahil watu hawatak mwshowe mnasema havtibki na rem.hawo n bacteria wanao sababisha
 
Flax [wakati nautafuta huo mmea imejitokeza mimea mengi tofauti tofauti!]

VarigatedFlaxLily.jpg
 
Nina mgonjwa wa vidonda vidonda vya tumbo ametumia dawa za hospt kwa muda mrefu nafuu hamna.nimeamua kujaribu tiba mbadala.nimenunua kitabu cha mtalaam fulani yuko Amerika amefanya utafiti wa dawa mbadala na anatibu magonjwa mengi kwa tiba mbadala.kwenye tiba ya vidonda vya tumbo kina maelezo haya-

some bioflavonoids(including quercetin,catechin and apigenin) inhibit the growth of the bacteria(Helicobacter pylori) which causes the ulcers.chamomile contains those bioflavonoids.

licorice has been used for centuries to soothe inflamed and injured portions of the intestinal tract.it increases mucin and fights H.pylori. best to take it in the form of DGL (deglycerinated licorice),which will not increase blood pressure or cause water retention.take 1-2 chewable tablets of GDL 1-2 hours before bedtime.aiso extremely good:marshmallow root.

. st.john's wort and malva both calm the stomach and reduce intestinal irritation.also helpful are bilberry,flax,catnip,goldenseal,bayberry , myrrh and alovera accelerates healing.

also Hops,skullcap and valerian will help you sleep


nimeamua kuweka maelezo hayo ili yasaidie wengi.ombi langu hiyo mimea niliyo iandika kwa rangi ya bluu siijui kwa kiswahili inaitwaje.mwenye kuijua atusaidie kwa kiswahili.karibuni

Tumia hii njia mimi nimetumia imeniponya. Chukua carrot saga kama juice na unywe asubuhi na jioni hakika atapona huyo ndugu yako katika jina la Yesu Kristo.
 
Kwa sababu vidonda vya tumbo vingi vinasababishwa na uwingi wa tindikali,Hydrochloric acid inayochangiwa na hormone gastrin hormone,basi tiba ya kweli itakuwa ni kupunguza uzalishwaji mwingi wa gastrin.
Nadhani kuondolewa kwa cells zinazozalisha gastrin hormone au kuharibu receptors za hii hormone kutaponya moja kwa moja.
Vinginevyo,dawa nyingi ni kwa ajili ya ku-neutralise gastric acid.
Hivi ndivyo nionavyo.
 
Mwenye kufaham dawa ya vidonda vya tumbo.hasa za asili anijuze!

TIBA NA USHAURI WA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO


By MziziMkavu at 18:28 TIBA No comments







Dawa ya Vidonda vya Tumbo MAANDALIZI;





-Chukua karoti kilo1 ponda iwe laini na kisha uchemshe kwa dakika 15 ndani ya maji lita 1 na nusu au mbili chuja,kunywa juisi yake kwa kutibu vidonda tumbo au saratani ya tumbo,saratani ya kizazi tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6. Dawa ingine ya Vidond vya tumbo Vidonda tumbo:
Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.


Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani. VYAKULA



TIBA KWA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO


Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.


Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:


VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.


POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine', vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.


ULAJI CHUMVI
Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.


MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.


VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.


STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha. chanzo.
TIBA NA USHAURI WA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
 
Back
Top Bottom