Tetesi: Ugumu wa Maisha Tanzania wasababisha AAR kufunga ofisi zake Tanzania

Tetesi: Ugumu wa Maisha Tanzania wasababisha AAR kufunga ofisi zake Tanzania

Acheni mambo yenu, sasa Kama shida ilikua mwenda zake, si wabakie! Si kunamama ambaye mnadhani si mzalendo?!

AAR! Wahuni hao. Nimedeal nao miaka kibao?!

Fanyeni tafiti kabla ya kuandika.

Kazi iendelee!!!!!
Hakuna haja ya kufanya utafiti mwingine kabla ya kutuwekea hapa wa kwako unaothibitisha kuwa AAR ni wahuni!
 
Taarifa ni ya muda mrefu hii,kama sikosei zaidi ya Mwezi. Huku Tigo ( na Zantel) wanaondoka wanauza kampuni

Tulikuwa tunaelekea kubaya sana, Mama ana kazi nzito sio kidogo na itachukua miaka 10 mpaka 20 kurudi katika hali ya kawaida ya mwanzo
Kampuni moja kuuza hisa zake kwa kampuni nyingine ni mambo ya kawaida sana.

Mbona mmiliki wa hisa nyingi za nmb Rabobank alipouzwa hisa zake kwa Arise B. V hamkusema biashara mbaya ila Tigo kuuza hisa zake biashara imekua mbaya.

Bavicha kweli ni nyumbu.
 
Ingekuwa jambo jema kama ungetupa taarifa kama baada AAR kufunga na kuondoka labda kuna upungufu wa upatikanaji wa huduma za afya kuliko kuleta uchochezi wa kishamba.
Upungufu wa huduma za afya nchini jupo obvious
 
AAR kama bima ya afya tegemeo laio kubwa lilikuwa wafanyakazi wa serikali na taasisi zake walikuwa wakihonga maafisa wa serikali ili wafanyakazi wakatiwe bima kwao serikali baada ya kuanzisha bima ya afya kwa ajili yao ya NHIF kwa wafanyakazi wake ikala kwao .Sekta binafsi ipo si wangejikita kutafuta soko huko? Wafanyakazi wa serikali wako chini ya laki nne wakati watanzania wako milioni 60 wangetafuta soko huko
 
AAR kama bima ya afya tegemeo laio kubwa lilikuwa wafanyakazi wa serikali na taasisi zake walikuwa wakihonga maafisa wa serikali ili wafanyakazi wakatiwe bima kwao serikali baada ya kuanzisha bima ya afya kwa ajili yao ya NHIF kwz wafanyakazi wake ikala kwao .Sekta binafsi ipo si wangejikita kutafuta soko huko? Wafanyakazi wa serikali wako chini ya laki nne wakati watanzania wako milioni 60 wangetafuta soko huko
CHIF ni mfuko gani huu? Embu utufafanulie? 🤔
 
Watanzania tuko vizuri tutembee vifua mbele! Never again to let a dictator, horrible person, much know and murderer to see the inside of the State House. Mwenyezi Mungu ashukuriwe sana kwa kuinusuru nchi yetu.
Nimeona clip kwa Kigogo ni kweli wafanyakazi wamesitishiwa ajira huku hawana uhakika wa kulipwa haki zao. Wafanyakazi wanadai haki zao.

Kweli Magu bora tu kaenda.
 
Hii ndio taarifa mpya inayozunguka mitandaoni kwa sasa kwamba ile Taasisi inayotoa huduma bora za afya imeamua kusitisha huduma zake nchini Tanzania kutokana na anguko la biashara na uchumi

Tuendelee kutega sikio kwa taarifa zaidi .
Na kwa Kauli ya Mama kuwa Yeye na Mtwaliwa ni Kitu kimoja na kwamba atapita mule mule tu kuna Uwezekano hali ikaendelea kuwa mbaya zaidi.

Wachumi wabobezi wanahitajika Kumshauri Mama juu ya kuweka Mizani sawa katika Ujenzi wa Miundombinu na kurejesha Uchumi Rafiki kwa Wananchi na kupunguza tatizo Kubwa la Ajira nchini kwa sasa.

Nchi itakuwaje na Maendeleo na Uchumi mzuri kama 85% ya Graduates na Intellectuals wake hawana Ajira na wapo tu Mitaani?

Sisemi Serikali iajiri ila iruhusu Wawekezaji wengi ( ambao bahati mbaya walikimbia nchini ) wawekeze zaidi ili Ajira zaidi zipatikane na Serikali kupitia TRA isiwakomoe katika Kodi kama ilivyokuwa.

Kuwe na Sera Maalum kwa Benki nchini za Kuwakopesha kwa Riba nafuu kabisa na za muda mrefu Wahitimu wa Vyuoni ili waweze Kujiunga na Kuchukua Mikopo hiyo kisha Wajiajiri.

Elimu ya Tanzania ifanyiwe marekebisho na iwe sana ya Technical Based ili kuendana na dunia ya sasa ambapo itasaida Watu ( Wahitimu ) wengi kuwa Wabunifu na hata kuweza Kujiajiri wenyewe.

Hata Serikali yenyewe pia ili Kupunguza hili tatizo la Ajira na kutaka Kujiimarisha Kiuchumi inaweza ikaanzisha Mkakati Maalum ( hata wa Kuingia Ubia ) na Matajiri wakubwa na Wakavifufua Viwanda vyao vyote nchini ambavyo vilikuwa vinaajiri Watu wengi na hii itasaidia sana tu.

Rasilimali zote za Tanzania zikisimamiwa vyema na tukaacha Upuuzi na Uswahili Uswahili wetu tuliouzoea huku Sera za Kukuza na Kuimarisha Uchumi wa Mtu na wa Taifa zikizingatiwa Tanzania itapaa na Wananchi nao 24/7 watakuwa na Tabasamu Nyusoni mwao kwakuwa Mifuko yao itakuwa hainuni na uhakika wa Kipato kuwepo.
 
Acheni mambo yenu, sasa Kama shida ilikua mwenda zake, si wabakie! Si kunamama ambaye mnadhani si mzalendo?!

AAR! Wahuni hao. Nimedeal nao miaka kibao?!

Fanyeni tafiti kabla ya kuandika.

Kazi iendelee!!!!!
Uyo mnaemuabudu alikuwa anapizi kwenye masaburi yenu nini!!!? Maana mmekuwa mandondocha
 
Hii ndio taarifa mpya inayozunguka mitandaoni kwa sasa kwamba ile Taasisi inayotoa huduma bora za afya imeamua kusitisha huduma zake nchini Tanzania kutokana na anguko la biashara na uchumi

Tuendelee kutega sikio kwa taarifa zaidi .
Kabla ya kuandika mambo usiyo yajua na kuleta fantasies zako ingekuwa busara kwanza uka aangalia Website yao kwanza ukajua ubora wa hiyo kampuni.

Nimegundua kuwa nyie ni watu wajinga sana. Mnapenda kushabikia vitu ambavyo hamvijui kwa undani wake. Hiyo kampuni ilikuwa haitoi Services zozote bora ukilinganisha na zile za serikali. Ni matapeli tu hao.

Ukweli ni kwamba Serikali hivi sasa inatoa huduma bora sana kuliko wao. Kulingana na hali hii it is obvious kuwa wanakosa wateja. Ili wapata wateja wengi kama mwanzo walitakiwa kuboresha huduma zao zaidi ili ku compete na zile zinazotolewa na institutions za serikali. Wameshindwa kuwafanyia hivyo Customers wao ndiyo maana wamekosa market.
Sijaona kampuni ambayo imeshindwa hata ile kujitangaza yenyewe kama hii kampuni. Angslieni wenyewe Wensite yao. Mnaweza mkaniambia kuwa hawa waendeshaji wako serious na biashara yao?


Watanzania jiaminini wenyewe. Nchi yetu na sisi wenyewe tunaweza zaidi kuliko hawa wageni. Msiwe na mawazo ya kwamba makampuni yanakuja kwetu eti kwa sababu sisi nii bora sana. Wanakuja kuchuma na kulimbikiza pesa kwao. Amkeni watanzania wenzangu. Msipende kushabikia uozo unao watuumiza.
 
Kwanini sababu ya kufungusha iwe uchumi umedorora tu?

Kwanini sababu isiwe uzembe wa hospitali kutegemea wateja waliokuwa wenye kipato serikalini ambao kwa sasa wanaishi Dodoma, ivyo kupungukiwa wateja.

Kwanini isiwe serikali baada ya kuboresha huduma za afya watu wanakimbilia kwenye huduma zao.

Yaani kila ya aina uzembe wa kibiashara au impact za sera zenye faida kwa wengi; side effect zake apewe hayati.

Sijapata kuona mtu bogus kama huyu mleta mada yeye kila tatizo wakulaumiwa ni serikali tu; matatizo mengine ni mipango mibovu ya biashara au kubadalika kwa external environment ukishindwa ku-adapt unapotea.
 
Hii ndio taarifa mpya inayozunguka mitandaoni kwa sasa kwamba ile Taasisi inayotoa huduma bora za afya imeamua kusitisha huduma zake nchini Tanzania kutokana na anguko la biashara na uchumi

Tuendelee kutega sikio kwa taarifa zaidi .
Misambwada imewafilisi walituma na ya kutolea.Bongo sio mchezo warembo Wana nundu kama vichuguu
 
Kama miaka mitano ya mwendazake imetuachia hali hii vipi kama angemalizia kumi yote mambo yangekuwaje?

Kuna watu wengi sana wamepoteza ajira kipindi cha utawala wake, wapo wengi ambao hawakuajiriwa kabisa, na hata wale waliokuwa wameajiriwa wakawa wanalia kupandishwa madaraja na mishahara.

Sijui kwanini bado hatujifunzi kama taifa kwamba panahitajika mpango maalum utaohakikisha unafuatwa na kila Rais atakaeingia madarakani ili kuhakikisha hali kama hiyo haijirudii tena, badala ya hivi sasa kila Rais kuja na vipaumbele vyake, tutakuja kulia tena mbele ya safari.
Tutakuja kulaumiana wakuu, akitokea mtu kama jiwe tena, jiwe alikuwa hana idea yyte ya masuala ya uchumi , alikuwa anapuyanga tu chapa ng'ombe mwenzangu yule...na alikuwa na kichwa kigumu kweli akiamin yy ndo yupo sahihi
 
Kwanini sababu ya kufungusha iwe uchumi umedorora tu?

Kwanini isiwe uzembe wa hospitali kutegemea wateja waliokuwa wenye kipato serikalini ambao kwa sasa wanaishi Dodoma, ivyo kukosa wateja.

Kwanini isiwe serikali baada ya kuboresha huduma watu wanakimbilia kwenye huduma zao.

Yaani kila ya aina uzembe wa kibiashara au impact za sera zenye faida kwa wengi; side effect zake apewe hayati.

Sijapata kuona mtu bogus kama huyu mleta mada yeye kila tatizo wakulaumiwa ni serikali; mengine ni mipango mibovu ya biashara tu.
AAR wapo Dar tuu?? Wale wapo mpaka Mwanza.....na wateja wao wakubwa ni wafanyakazi wa sekta binafs ambayo ipo taabani.....!! G4S wenyewe wamepoteza kazi Barick, jiwe aliwabana Barick mpak ikabdi G4S watemeshwe mzigo na wakaondoka na mamia ya wafanyakazi ,kimbembe kikawa kwenye mafao Yao NSSF hakuna kitu... Mambo ya Jiwe basi Tu wakuu mana wengine walinufaika na utawala
 
AAR wapo Dar tuu?? Wale wapo mpaka Mwanza.....na wateja wao wakubwa ni wafanyakazi wa sekta binafs ambayo ipo taabani.....!! G4S wenyewe wamepoteza kazi Barick, jiwe aliwabana Barick mpak ikabdi G4S watemeshwe mzigo na wakaondoka na mamia ya wafanyakazi ,kimbembe kikawa kwenye mafao Yao NSSF hakuna kitu...
Si unaona sasa kumbe watu wanafungua biashara target yao ni segment fulani yakitokea yakutokea awawezi ku adapt halafu lawama apewe serikali. Hizi tabia za kukariri ndio maana waafrika atusogei.

Huko kwenye mafao yao NSSF waandamane ofisi za B.o.T sheria zipo wazi za kimataifa na financial institution regulation za Tanzania hiyo taasisi airuhusiwi kuwekeza kwenye miradi ya kuzalisha moja kwa moja; unless kama wananunua hisa kwenye kampuni ambayo ishaanza operation.

NSSF mpaka wanachukua shamba, wanalima miwa na wanataka kujenga sijui walishajenga kiwanda cha miwa anawaangalia tu; just common sense watu hawana reserve za kutosha kulipa madeni ya wastaafu wanaokaribia kupeleka madai halafu wanaangaliwa wakiwekeza tsh 130 billion kwenye investment zenye return za 5-10 years na bank of Tanzania aifanyi risk assessment zake.

Hayati Prof Ndullu asingeruhusu upuuzi wa aina hiyo kisa watu wanataka kujipendekeza kwa raisi.
 
Back
Top Bottom