Kama miaka mitano ya mwendazake imetuachia hali hii vipi kama angemalizia kumi yote mambo yangekuwaje?
Kuna watu wengi sana wamepoteza ajira kipindi cha utawala wake, wapo wengi ambao hawakuajiriwa kabisa, na hata wale waliokuwa wameajiriwa wakawa wanalia kupandishwa madaraja na mishahara.
Sijui kwanini bado hatujifunzi kama taifa kwamba panahitajika mpango maalum utaohakikisha unafuatwa na kila Rais atakaeingia madarakani ili kuhakikisha hali kama hiyo haijirudii tena, badala ya hivi sasa kila Rais kuja na vipaumbele vyake, tutakuja kulia tena mbele ya safari.