Uchumi ni taaluma ndugu sio kila mtu anaweza kuuelezea uchumi. Pili uchumi una vipimo vyake vilivyokubalika na ndivyo vinavyotumika kupima na kulinganisha kwa vipindi tofauti au/ na kati ya uchumi mmoja na mwingine. IMF na World bank ndizo zinazotathmini chumi zote za dunia na ripoti hutolewa kila mwaka; hao hawaburuzwi na wana namna mbalimbali za kukusanya data, kuzitunza, kufanya analysis, kuzitafsiri. Hata nchi ikipika data bado wana uwezo wa kuelezea jambo kwa usahihi. Katika uchumi kuna kitu kinaitwa forecast, data zinaweza hata kukisiwa kwa kutumia njia zinazokubalika kiuchumi mfano kwa kutumia econometrics na wakawa sahihi.Kabla hata ya Corona, uchumi wetu tayari ulikuwa uko hovyo, kilichokuwepo ni propaganda ikisaidiwa na utungwaji sheria zenye lengo za kufanya kutopatikana takwimu mbalimbali kwa umma. Hakuna uchumi unaokua wakati biashara nyingi zinafungwa, hakuna uchumi unaokua wakati kiwango cha uwekezaji kinashuka kadri muda unavyosogea, hakuna unakuwa wakati kuna siku soko la hisa manunuzi ni 0, hakuna uchumi unakuwa unashindwa kupandisha mishahara ya watumishi wako kwa miaka mitano huku gharama za maisha zikikuwa , uchumi unakuwa vipi wakati katika kipindi cha miaka mitano tu umekopa kuliko miaka 30 ya waliokutangulia? Propaganda tu
Kikawaida uchumi sio siku zote utakwenda juu tu, kitu kimoja kinaweza shuka na kingine kupanda katika muktadha wa uchumi mzima. Wengi humu wanaoshabikia hawana uelewa wa uchumi wala hawasomi ripoti za uchumi za taasisi kubwa na zinazoheshimika katika nasuala ya uchumi duniani. Ukisoma kwa mfano ripoti ya mwaka 2020 utaonaTanzania japo haikufikia lengo la ukuaji wa uchumi lakini bado ilifanya vizuri kulinganisha na nchi nyingi tena za hapa africa na duniani kwa ujumla.