Uhaba wa Lactogen Formula 1 pigo kwa wafanyakazi wenye watoto wachanga

Uhaba wa Lactogen Formula 1 pigo kwa wafanyakazi wenye watoto wachanga

kamwamu

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,521
Reaction score
3,309
Jumuia ya akina mama wafanyakazi wenye watoto wachanga huwanywesha watoto maziwa f1 na kuwanyonyesha wanapotoka kazini.

Moja ya f1 iliyozoeleka ni lactogen toka Kenya au France. Ni wiki ya 2 sasa nimeshindwa kupata maziwa hayo madukani kwa mtoto wa ndugu yangu Dar.

Amejaribu agiza mikoani, Mwanza na Mbeya, jibu hakuna maziwa. Tafadhali if member mwenye ufahamu yalipo maziwa ya lactogen formula 1 anijulishe, au mbadala wake.
 
Pole mkuu.

Ushauri tu anunue Breast pump awe anamkamulia mtoto maziwa aweke kwenye Friza. Akiwa kazini wanaomwangalia mtoto wanayawarm nakumpa mtoto, Hii kuwarm sio kuyachemsha Bali anachukua chombo anaweka maji vuguvugu au moto Halafu anatumbukiza chombo chenye maziwa ili maziwa yapate uvugu ndio apatiwe mtoto.

Anunue tu zile storage bags za kuweka kwenye Friza yanaweza kukaa kwenye Friza Hadi miezi 6.

Working mom's wengi wanafanya hivyo nowdays mama Anafanya Kazi na mtoto anapata maziwa ya mama, formula si lazima
 
Wewe jamaa hauko serious yaani unakosa bidhaa Dar alafu unaagiza Mbeya utegemee kupata.. wakati hao wote wanachukua hapa mjini.
Dar ndio waagizaji na watumiaji wengi wa bidhaa. Maelezo ya wauzaji ni kuwa muda mrefu mzigo mpya haujaingia. Mikoani ni kuharibu kwa vile watumiaji si wengi.
 
Nashukuru kwa ushauri, nitauwasilisha.
 
breast pump Anunue electronic pump Ni nzuri sababu hatatumia nguvu kukamua anachomeka kwenye umeme inamkamua.
Baadhi yake ni hizi
1618073154890.png

Atazipata hapa
Code:
 https://www.amazon.com/Breast-Pumps/b?ie=UTF8&node=166786011

Na ukihitaji kuagiziwa basi pitia huu uzi
kamwamu
 
Na pia Kama atanunua breast pump Anunue electronic pump Ni nzuri sababu hatatumia nguvu kukamua anachomeka kwenye umeme inamkamua. Manual pump Ni Bei ya rahisi lakini kukamua unatumia mikono inachosha Sana.
Wanawake siku hizi wanatumia pump hata kukamua maziwa kwenye vifua vyao wenyewe ?[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Wanawake siku hizi wanatumia pump hata kukamua maziwa kwenye vifua vyao wenyewe ?[emoji2][emoji2][emoji2]
Ndio kurahisisha ukamuaji pia kukamua maziwa mengi kwa muda mfupi. Teknolojia kwa Wamama wanaofanya Kazi, hata akiwa kazini anaweza kwenda rest room akakamua na kuyastore kwenye coolers baadae akampa mtoto.
 
Na pia Kama atanunua breast pump Anunue electronic pump Ni nzuri sababu hatatumia nguvu kukamua anachomeka kwenye umeme inamkamua. Manual pump Ni Bei ya rahisi lakini kukamua unatumia mikono inachosha Sana.
Zinauzwa bei gani mkuu?
 
Ndio kurahisisha ukamuaji pia kukamua maziwa mengi kwa muda mfupi. Teknolojia kwa Wamama wanaofanya Kazi, hata akiwa kazini anaweza kwenda rest room akakamua na kuyastore kwenye coolers baadae akampa mtoto.
Ok sawa sawa nimekupata
 
Ndio kurahisisha ukamuaji pia kukamua maziwa mengi kwa muda mfupi. Teknolojia kwa Wamama wanaofanya Kazi, hata akiwa kazini anaweza kwenda rest room akakamua na kuyastore kwenye coolers baadae akampa mtoto.
Nakumbuka niliwahi kukamua maziwa kwa zile za kawaida jaman nilishindwa.Mama akanifundisha kukamua kwa mkono ninakamua vizuri tu,sijui kwa sababu ninayo mengi.Ndo nashangaa humu siku hizi kuna za umeme.
 
Back
Top Bottom