Uhaba wa Lactogen Formula 1 pigo kwa wafanyakazi wenye watoto wachanga

Uhaba wa Lactogen Formula 1 pigo kwa wafanyakazi wenye watoto wachanga

Na pia Kama atanunua breast pump Anunue electronic pump Ni nzuri sababu hatatumia nguvu kukamua anachomeka kwenye umeme inamkamua. Manual pump Ni Bei ya rahisi lakini kukamua unatumia mikono inachosha Sana.
Breast electric pumb kwa Dar inauzwa wapi na ni bei gani?
 
Zinauzwa bei gani mkuu?
Sina uhakika Sana lakini manual inaweza kuwa Kama elfu 30 Hadi 40 hivi na electronic elfu 60 Hadi 80. Yangu sikununua bongo hapo najaribu kukisia kutokana na hela nliyonunulia kule.

Kuna mkuu kaquote comment yangu huko juu kasema anauza unaeza mcheck au uende baby shop kubwa kubwa unaweza zipata
 
Nakumbuka niliwahi kukamua maziwa kwa zile za kawaida jaman nilishindwa.Mama akanifundisha kukamua kwa mkono ninakamua vizuri tu,sijui kwa sababu ninayo mengi.Ndo nashangaa humu siku hizi kuna za umeme.
Me mwenyewe manual ilinishinda na mkono pia ndo kabisaaaa ilikuwa hakitoki kitu. Electronic unakaa tu chini inapump Hadi maziwa yanaisha unabadilisha ziwa jingine.
 
Ni vizuri wizara ya afya wakawa wanafanya uchunguzi Mara kwa Mara(sampling) vyakula vya watoto vinavyoingizwa nchini,tusije kuwa tunadumaza akili taifa la kesho bila kujua.
 
Breast electric pumb kwa Dar inauzwa wapi na ni bei gani?
Nenda baby shop kubwa kubwa au ingia istagram search breast pump Tanzania Kuna page utaona wanatangaza wanauza.
Na Kuna mkuu ka quote comment yangu hapo juu kasema anauza unaweza mcheck
 
Ni vizuri wizara ya afya wakawa wanafanya uchunguzi Mara kwa Mara(sampling) vyakula vya watoto vinavyoingizwa nchini,tusije kuwa tunadumaza akili taifa la kesho bila kujua.
Uko sahihi. Yapo ya Brazil ni tabu tupu. Yakitikiswa povu kama wanzuki.
 
Ni vizuri wizara ya afya wakawa wanafanya uchunguzi Mara kwa Mara(sampling) vyakula vya watoto vinavyoingizwa nchini,tusije kuwa tunadumaza akili taifa la kesho bila kujua.
Waziri wa tangawizi na malimao alisikie hili hata kama yupo kwenye mashine ya kujifukiza Mlonganzila.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Me mwenyewe manual ilinishinda na mkono pia ndo kabisaaaa ilikuwa hakitoki kitu. Electronic unakaa tu chini inapump Hadi maziwa yanaisha unabadilisha ziwa jingine.
Mi nakamua kwa mkono nashukuru Mungu nina maziwa mengi Sana.Nikiwaga maternity nakamua namwaga manake yakijaa Sana yananipa homa.
 
Pole mkuu.

Ushauri tu anunue Breast pump awe anamkamulia mtoto maziwa aweke kwenye Friza. Akiwa kazini wanaomwangalia mtoto wanayawarm nakumpa mtoto, Hii kuwarm sio kuyachemsha Bali anachukua chombo anaweka maji vuguvugu au moto Halafu anatumbukiza chombo chenye maziwa ili maziwa yapate uvugu ndio apatiwe mtoto.

Anunue tu zile storage bags za kuweka kwenye Friza yanaweza kukaa kwenye Friza Hadi miezi 6.

Working mom's wengi wanafanya hivyo nowdays mama Anafanya Kazi na mtoto anapata maziwa ya mama, formula si lazima

Maziwa ya mama kwa mtoto ni the best kwa afya bora ya mtoto kiakili na kimwili.

Watoto wengi wamekuwa zombies kutokana na kutumia hiyo mi -maziwa ya kutengeneza viwandani.
 
Mi nakamua kwa mkono nashukuru Mungu nina maziwa mengi Sana.Nikiwaga maternity nakamua namwaga manake yakijaa Sana yananipa homa.
Hongera, binadamu hutofautiana. Kuna kinamama maziwa kifuani ni kiduchu.
 
Maziwa ya mama kwa mtoto ni the best kwa afya bora ya mtoto kiakili na kimwili.

Watoto wengi wamekuwa zombies kutokana na kutumia hiyo mi -maziwa ya kutengeneza viwandani.
Ni wanna wachache wanaokataa kunyonyesha. Kuna sababu kadhaa ziazowalazimisha wengi kuwapa watoto maziwa ya formula kv kwenda kazini, maziwa machache, kuugua(mzazi mgonjwa akitumia antibiotics in maziwa kifuani hukata).
 
Wewe jamaa hauko serious yaani unakosa bidhaa Dar alafu unaagiza Mbeya utegemee kupata.. wakati hao wote wanachukua hapa mjini.
Sio kila bidhaa zinatoka Dar...

Mikoa ya mipakani kama Mbeya hupata nyingi ya imports toka nchi jirani...

Mathalani ukiwa Mbeya (Tunduma), unapata watu wanatumia sukari ya Zambia na bidhaa nyinginezo, ukiwa Kyela kukutana na bidhaa za Malawi ni kwa sana, huko Rombo kuna watu wanatumia vitu vinatoka Kenya kiasi hata hawajui kama Dar ni source ya vitu...
 
Wanawake siku hizi wanatumia pump hata kukamua maziwa kwenye vifua vyao wenyewe ?[emoji2][emoji2][emoji2]
Dunia ya leo si ya zamani mkuu...wamama wanatega mashine kwenye matiti kama ng'ombe wa Dodoma wale...
 
Ni wanna wachache wanaokataa kunyonyesha. Kuna sababu kadhaa ziazowalazimisha wengi kuwapa watoto maziwa ya formula kv kwenda kazini, maziwa machache, kuugua(mzazi mgonjwa akitumia antibiotics in maziwa kifuani hukata).

Nasema hivi, kama inawezekana kununua maziwa ya kopo au ya ng'ombe kwanini isiwezekane kuwepo na biashara ya maziwa ya binadamu??--- funny and hillarious!!🤣🤣

Wamama wanaonyonyesha wanaweza kuuza baadhi ya maziwa yao baada ya kukaguliwa kitabibu ili yatumike kwa ajili ya wamama wenye watoto na wanayo matatizo ya breasting, kifupi ni kwamba hatua zote zifuatwe ili jambo hili lifanikiwe kwa ajili ya afya za watoto wetu, Watoto wenye afya ni jamii yenye afya hatimaye ni taifa lenye afya na ustawi.

"Breast feeding is the best for the best results.
 
Naona mahouseboy wakipata kazi ya kukamua maziwa ya mtoto kutoka kwa mama, mambo haya aisee.....jambo lingine yale majamaaa yanayonyonya maziwa ya mtoto ili mtoto ashinde na njaa hivi akili zao huwa zimetimia kweli...
 
Nasema hivi, kama inawezekana kununua maziwa ya kopo au ya ng'ombe kwanini isiwezekane kuwepo na biashara ya maziwa ya binadamu??--- funny and hillarious!![emoji1787][emoji1787]

Wamama wanaonyonyesha wanaweza kuuza baadhi ya maziwa yao baada ya kukaguliwa kitabibu ili yatumike kwa ajili ya wamama wenye watoto na wanayo matatizo ya breasting, kifupi ni kwamba hatua zote zifuatwe ili jambo hili lifanikiwe kwa ajili ya afya za watoto wetu, Watoto wenye afya ni jamii yenye afya hatimaye ni taifa lenye afya na ustawi.

"Breast feeding is the best for the best results.
Mfumo huu wenzetu Kenya wameuanzisha. Wanaita Benki ya maziwa Kama ilivyo Benki ya damu. Mama akiwa na maziwa mengi anaruhuusiwa kwenda kujitolea hospital wanamkamua na kuhifadhi.
Ikitokea Mama akafariki wakati wa kujifungua au akapata matatizo yanayosababisha ashindwe kunyonyesha baada ya kujifungua yale maziwa yaliyo hifadhiwa Benki yanatumika kwa mtoto mchanga Hadi utakapopatikana mbadala.
 
Lactogen inatoka France na haitoki Kenya pia NAN inatoka Netherlands hizi ndizo zilizotambuliwa na kuruhusiwa kuuzwa hapa Tanzania kulingana na mazingira tunayoishi pia lactogen haijawahi kutengenezwa Kenya kama upo dar na unayataka nenda kawe beach road sikuhizi sijui mwai kibaki Kuna jengo limeandikwa infotech ingia hapo ulizia wahuzika wa hayo maziwa watakusaidia sehemu pa kuyapata na taarifa zaidi.

Pia hairuhusu kumpa au kutoa taarifa za ushawishi ili mtu anunue hayo maziwa Bali ushauri na uelekezi wa daktari ndio unakulazimu kumpa mwanao hayo maziwa ya kopo
 
Back
Top Bottom