Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Tetesi: Uhakiki: Maprofesa UDSM washindwa kuwasilisha vyeti vya sekondari,wawa wakali

Chukulia huyu ni usalama wa taifa na yupo sehemu nyeti unaanzaje kumfukuza, halafu kama mtu hakusoma form four anawezaje kumudu masomo ya form six hadi Chuo?
Hiyo haihalarishi kosa kwa vile yuko sehemu nyeti au aliweza kuyamudu masomo huko mbeleni.

Kama hao watasamehewa kwa vile ni maprofesa au wana PhD basi kigezo hicho hicho kitumiwe kwa walimu pia, Maana nao wameweza kufanikiwa kufaulu hizo diploma zao na kupata vyeti cha Ualimu. Hapo ni sawa na kusema kila mtu awakilishe cheti chake cha mwisho kilichomsaidia kupata hiyo ajira. Yaani kama nitaweza kupeleka cheti changu kuonyesha kuwa nimemaliza Bsc Eng na nimesajiliwa na Bodi basi sina haja ya kuonyesha vyeti vyangu vya huko nyuma.

Hawa watu kama hawana vyeti bado record zao za jinsi gani wamefika hapo zinaweza kupatikana. Binafsi sidhani kama uwakilishaji wa vyeti tu peke yake utasaidia kuwajua mafisadi wa elimu. Kuna watu ambao wameweza kufanya kazi kama Madakatari au Maenineer bila kuwa na hizo elimu. By the way, huko mitaani na Bungeni kuna PhD ngapi zenye utata, leo hawa watu wakibahatika kupa ajira vyuoni na kuwa Lecturers huoni kama wanaweza kutumia hiyo mbinu kujitetea.

Imagine kama mimi nalitumia cheti cha ndugu yangu leo nafanya kazi ya Ualimu huko Geita na ndugu yangu ni Engineer huko Lindi. Hivi kweli itakuwa vigumu kutumia cheti kile kile kuhakikiwa!!?
 
wakimaliza kuhakiki tuanze mchakato wa kubadilisha katiba, ili vilazwa visiingie bungeni..
wanatia aibu sana kwa kutoa hoja zisizo kua na mantiki na kupitisha mambo wasiojua maana wala madhara yake kwa wananchi wanaowawakilisha..
 
Kumwambia prof aonyeshe cheti cha frm four ni aibu na matusi makubwa sana kwake....ni sawa na wewe kumuuliza mkeo kabla yako alikua na wanaume gani wengine...
Mimi nadhani chamaana kabisa ambacho kingefanyika ni kuangalia utendaji wao wa kazi upo sawa ni wa weledi?
Kama haupo sawa nikumuondoa katika kazi hiyo akatafute kazi kwingine.
 
Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.

Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
na yule aliyesoma na mh mengi wamemhakiki?
 
Hehe mkuu mi si profesa, hainiingii akilini tu mtu kamaliza degree, masters hadi PhD alafu unasema unataka cheti cha form four, wanaotetea cheti cha form four ni wale ambao walifeli huku juu, kama mtu kafaulu vizuri huku juu cheti cha form four hakina maana yoyote.


Watanzania mko obsessed na vyeti, ofcoz vyeti ni muhimu kwenye academics peke yake, in this case maprofesa ni muhimu wakawa na vyeti ila sio vya sekondari, hadi mtu kua profesa lazima alikua anapasua A za kutosha kuanzia degree kwenda juu, huyo sio mtu wa kumuomba cheti cha form four kabisa.
Sijaona "logic" kwenye huu utetezi wako.Ni lazima uonyeshe vyeti vyote kwa nini wafiche.
 
Kumwambia prof aonyeshe cheti cha frm four ni aibu na matusi makubwa sana kwake....ni sawa na wewe kumuuliza mkeo kabla yako alikua na wanaume gani wengine...
Mimi nadhani chamaana kabisa ambacho kingefanyika ni kuangalia utendaji wao wa kazi upo sawa ni wa weledi?
Kama haupo sawa nikumuondoa katika kazi hiyo akatafute kazi kwingine.
Eti matusi waeke vyeti mezani.
 
Je anayehakiki amehakikiwa? Zoezi hili ni zuri sana, ila linatakiwa lianzie paleee Bungeni. Na lifanyike kwa uwazi na live ili iwe mfano kwa Taasisi zingine za Serikali.
Ni kweli,kama walivo hakiki silaha zao,basi na vyeti hivyo hivyo wahakiki
 
Ni kitu cha kushangaza sana. Halafu Mkapa na Kikwete wamefanya naye kazi huyu miaka chungu nzima na bila shaka walikuwa wanajua uwezo finyu wa kujieleza katika moja ya official language na hata utendaji wake lakini bado hawakujali maslahi ya nchi na kuangalia maslahi yao wenyewe tu.


12993368_582304351927746_863212580339588200_n-jpg.366441
Nafikiri hawakutaka mtu aliyewazidi uwezo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hapa atazimia mtu zimi, vyeti hadi ulaya mtu wanamjua ghafla unasikia alighushi
 
Hata mimi wala sikusumbuka kwenda kuchukua.

This is so ridiculously absurd.
Kwani kuwa pro.kubeba cheti cha form four kuna tatizo gani kam hukuforge?.....kama unakataa kuleta cha form four tutaaminije kama uprof.ni wa ukweli?....leteni vyeti vyenu vya form four na la saba.....uprof.ni kuwa smart kama unaona Hamna haja ya kuonesha cheti cha form four....hupaswi kuitwa prof....
 
Ukipima uwezo wa la saba kibajaji na PhD holder Prof viazi pale bungeni hata wewe utamtilia shaka Prof
 
Hee! wataombwa na vyeti vya kumaliza nursery.
Mwaka huu tutashuhudia mengi.
Hiyo sasa itakuwa ni kero ya kupindukia. Yaani mtu anacheti cha PhD unamuomba cheti cha shule ya msingi? Halafu hao wanaopitia vyeti elimu zao sasa utacheka.
 
Mimi nafikiri tuache mzaha. Haiwezekani professors wetu wanyanyaswe kisa tu cheti cha form four. Mfano unapoomba kusoma PhD ulaya, hawana muda wa kupitia sijui eti vyeti vya O-level na A- level. Wao wanataka bachelor na masters tu basi. Cha muhimu ni je vyeti vya taaluma alivyo navyo ni genuine?
 
Tatizo ni cheti cha form four au kichwani mwake elimu ya profesa anayo maana kama Hana cheti lakini elimu ya kiprofesa ipo tatizo nini
Kwa vile yupo vizuri kichwani na kafoji cheti kisichotambuliwa na NECTA basi aachwe kwa vile Dr au Profesa Hapana hiyo
 
Mimi nafikiri tuache mzaha. Haiwezekani professors wetu wanyanyaswe kisa tu cheti cha form four. Mfano unapoomba kusoma PhD ulaya, hawana muda wa kupitia sijui eti vyeti vya O-level na A- level. Wao wanataka bachelor na masters tu basi. Cha muhimu ni je vyeti vya taaluma alivyo navyo ni genuine?
Hii ndio Tanzania, kwa hiyo waachwe kwa vile maprofea?
 
Back
Top Bottom