Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo haihalarishi kosa kwa vile yuko sehemu nyeti au aliweza kuyamudu masomo huko mbeleni.Chukulia huyu ni usalama wa taifa na yupo sehemu nyeti unaanzaje kumfukuza, halafu kama mtu hakusoma form four anawezaje kumudu masomo ya form six hadi Chuo?
na yule aliyesoma na mh mengi wamemhakiki?Wakati zoezi la kuhakiki vyeti vya watumishi wa umma nchini likiendelea,kizungumkuti kimejitokeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Taarifa zitakazo sifa zinadokeza kuwa Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wengi wameshindwa kuwasilisha vyeti vyao vya sekondari:kidato cha nne na cha sita.
Taarifa zinaonesha kuwa Wahadhiri hao wametoa hoja,wakiwa wamecharuka, kuwa hawakuajiriwa kwa vyeti vya sekondari. Wamedai kuwa vyeti vyao vya Shahada,Stashahada na Astashahada vinatosha na kutisha. Wahadhiri hao,taarifa zinasema,wamekubaliwa kuhakikiwa kwa vyeti walivyoviwasilisha,bila ya vya sekondari.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Sijaona "logic" kwenye huu utetezi wako.Ni lazima uonyeshe vyeti vyote kwa nini wafiche.Hehe mkuu mi si profesa, hainiingii akilini tu mtu kamaliza degree, masters hadi PhD alafu unasema unataka cheti cha form four, wanaotetea cheti cha form four ni wale ambao walifeli huku juu, kama mtu kafaulu vizuri huku juu cheti cha form four hakina maana yoyote.
Watanzania mko obsessed na vyeti, ofcoz vyeti ni muhimu kwenye academics peke yake, in this case maprofesa ni muhimu wakawa na vyeti ila sio vya sekondari, hadi mtu kua profesa lazima alikua anapasua A za kutosha kuanzia degree kwenda juu, huyo sio mtu wa kumuomba cheti cha form four kabisa.
Eti matusi waeke vyeti mezani.Kumwambia prof aonyeshe cheti cha frm four ni aibu na matusi makubwa sana kwake....ni sawa na wewe kumuuliza mkeo kabla yako alikua na wanaume gani wengine...
Mimi nadhani chamaana kabisa ambacho kingefanyika ni kuangalia utendaji wao wa kazi upo sawa ni wa weledi?
Kama haupo sawa nikumuondoa katika kazi hiyo akatafute kazi kwingine.
Ni kweli,kama walivo hakiki silaha zao,basi na vyeti hivyo hivyo wahakikiJe anayehakiki amehakikiwa? Zoezi hili ni zuri sana, ila linatakiwa lianzie paleee Bungeni. Na lifanyike kwa uwazi na live ili iwe mfano kwa Taasisi zingine za Serikali.
Kina Bulembo na KibajajiWakimaliza huko
Waende kwenye vyama vya Siasa
Nafikiri hawakutaka mtu aliyewazidi uwezo.Ni kitu cha kushangaza sana. Halafu Mkapa na Kikwete wamefanya naye kazi huyu miaka chungu nzima na bila shaka walikuwa wanajua uwezo finyu wa kujieleza katika moja ya official language na hata utendaji wake lakini bado hawakujali maslahi ya nchi na kuangalia maslahi yao wenyewe tu.
![]()
Kwani kuwa pro.kubeba cheti cha form four kuna tatizo gani kam hukuforge?.....kama unakataa kuleta cha form four tutaaminije kama uprof.ni wa ukweli?....leteni vyeti vyenu vya form four na la saba.....uprof.ni kuwa smart kama unaona Hamna haja ya kuonesha cheti cha form four....hupaswi kuitwa prof....Hata mimi wala sikusumbuka kwenda kuchukua.
This is so ridiculously absurd.
Hiyo sasa itakuwa ni kero ya kupindukia. Yaani mtu anacheti cha PhD unamuomba cheti cha shule ya msingi? Halafu hao wanaopitia vyeti elimu zao sasa utacheka.Hee! wataombwa na vyeti vya kumaliza nursery.
Mwaka huu tutashuhudia mengi.
Kwa vile yupo vizuri kichwani na kafoji cheti kisichotambuliwa na NECTA basi aachwe kwa vile Dr au Profesa Hapana hiyoTatizo ni cheti cha form four au kichwani mwake elimu ya profesa anayo maana kama Hana cheti lakini elimu ya kiprofesa ipo tatizo nini
Hii ndio Tanzania, kwa hiyo waachwe kwa vile maprofea?Mimi nafikiri tuache mzaha. Haiwezekani professors wetu wanyanyaswe kisa tu cheti cha form four. Mfano unapoomba kusoma PhD ulaya, hawana muda wa kupitia sijui eti vyeti vya O-level na A- level. Wao wanataka bachelor na masters tu basi. Cha muhimu ni je vyeti vya taaluma alivyo navyo ni genuine?