Tetesi: Uhakiki vyeti TRA; 437 kupigwa chini

Daaah nimepata laana ya 'retired officer' wa TRA. lol

We jamaa unazeeka vibaya aisee. Haya piga sala nzito hao ndugu zako 'kikombe cha Vyeti feki' kiwaepuke.

-Kaveli-
Wote walio foji vyeti hawawezi kukiepuka kikombe hicho
 
Huyo Kidata si ndiye aliyeagiza kwamba wanahakiki vyeti kuanzia first degree na kuendelea as if TRA hakuna wafanyakazi wenye vyeti tu vya Form IV, VI na Diploma bila kuwa na first degree.

Hili zoezi lilishashindwa hata kabla halijaanza. Mark my words.
 
Mkuu naona umetema nyongo kweli mkuu


Mkuu kuna watu humu wa ajabu sana. Huyo jamaa yeye 'anasikitika' na 'anawaonea huruma' villaza wa TRA walioingia kimagumashi na vyeti feki.

Kwa maneno mengine ni kwamba anatamani sana wasitumbuliwe, waendelee kuwa ofisini na 'kupiga dili' kwa vyeti kagali.

Alafu anajiita yeye ni 'retired officer'.

-Kaveli-
 
Siku hizi makabila yote wamesoma bhana sio kila mara wachaga ohh mara wahaya kwa nn ??.km wamesoma mbona kila sehemu wakiwekwa wao ni kuharibu na kuiba au ndo usomi huo. Ni taaasisi gani imeshikwa na makabila hayo usisikie ukabila wao .mimi naoana tuache kuona makabila mengine kua hayana wasomi
 
Wote walio foji vyeti hawawezi kukiepuka kikombe hicho


Na iwe hivyo Mkuu. Binafsi naunga mkono sana hizo juhudi za serikali kurejesha nidhamu & real professionalism kwenye utumishi wa umma.

Ni hatari sana Taifa likiwa na incompetent work-force ilojaa villaza, vyeti feki, na magumashi. Ni msiba!

"Lazy Affair Life" is no more!

-Kaveli-
 
Binafsi naomba mtu pole wale tutakaoenguliwa kwene hili sakata au huu mkasa kwasababu zilikuwa ni harakati katika kuyamudu+kujikimu na kujikwamua maisha,tuko tayari kuwajibika ila mtufariji nasio kutunanga.
 
Wewe jamaa na zile habari zako za dogo janja na Muitaliano hata sina imani na wewe
 
Sasa mtoto wa maskini hii inamsaidiaje mana watoto wa maskini hata elimu ya chuo wengi hawana au ndio ile roho za kimaskini kufurai mwenzako akiwa chini, ungesema zoezi hili linasaidia kupata watu wenye sifa na vyeti shahili sio italeta matunda kwa watoto wa maskini maana watoto wa maskini sio criteria ya kupata kazi
 
Jamani tuache ukabila unaharibu nia nzuri ya Hilo zoezi la vyeti feki Kama linalenga Kabila au Dini moja wakati kunaweza kuwa na hao wa Dini na makabila mengine
 
Kuna wakati zaidi ya robo tatu ya wafanyakazi wa TRA walikuwa wachagga. Sijui kama wote walikuwa na vyeti halisi
Mkuu Lizaboni mm suala la ukabila huwa naliogopa sana kulitamka tamka,halina afya sana kwa mustakabali wa Taifa letu,tuangalie hili la vigezo, kama hawana ni kuchinjilia mbali basi!
 
Sikupingi wala sikubaliani na wewe kwa wakati mmoja. Si kwa sababu mimi ni mhusika ila ni kwa sababu napenda fact zaidi

Huo uhakiki ndio kwanza umeanza, wewe umejuaje wako 400+ au kama wanajulikana kuna haja gani kupoteza muda na rasilimali zingine kuhakikia wote wakati wanaotafutwa wanafahamika, si wawaite tu wawambie leteni vyeti vyenu then wawatimue coz ni feki/hawana

Pili kwa nini tuna maisha ya wasiwasi sana hii inatuadhiri kutokuamini wengine, kwa nini tusiamini kwa sababu baba ana tabia njema na ni mkali hataki uzembe hivyo watoto watakuwa na nidhamu.

Tatu hii nchi ni yetu sote na ni muhimu kuijenga sote kwa pamoja, badala ya kuandika hapa tena kwa jina bandia huoni utamsaidia sana Kidata na Taifa kama utavaa ujasiri wa kwenda ofisi ni kwake na kumwambia huo mpango(kama usemacho ni kweli).

Am either of the part but i just want to think critically.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…