Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Wadau matokea ya kidato cha nne kwa mwaka 2012 yametoka tembeleeni website ya 'NECTA' nimejaribu saana naona web ipo bzy ila matokea ya jitegemee ni mabovu sana....
Maana...
Div 1 - 1
Div 2 - 2
Div 3 - 26
Div 4 - 210
Failed - 443
Hiyo ni Jitegemee..je zile za Kina sisi....za kata itakuwajeee
 
Mwamgunda umetoa point, huku lindi, wazazi hawatoi msukumo wa kutosha kwa watoto wao walioko sekondari, mfano nipale kijana wa kiume anapokuwa na mke wakati anasoma, kijana huyo anakaa na mke kwao na wazazi wanafahamu. kwa upande wa wasichana wao wameendekeza sana mapenzi, wengine wanaamua kutoenda shule na wazazi wanashindwa kuchukua hatua yoyote
 
TERRIBLE! yapo matatizo mengi tu. maabara sawa lakini sio sababu kubwa kwani yapo masomo mengine ambayo yangeweza kuwainua wanafunzi. pamoja na matatizo meng kuna shida ya nidhamu na kutokujitambua kwa wanafunzi. wengi sana hupenda starehe na masualaya mapenzi. wengine wanasoma kwa shida bila lishe ya kutosha. wanafundishwa pia na walimu waliokata tamaa. ziko shida nyingi wanaofeli zaidi naamini wanatoka shule za serikali ambazo wakubwa wamezikana na kutafuta za kwao.mjadala wa kiitaifa kuhusu elimu uwepo kwani ni aibu zaidi ya nusu ya wanafunzi kupata sifuri.
 
Secokata is keeping children out of street ili angalau waongezeke urefu.
 
Kimsingi ni kichefuchefu kutaja matokeo ya mtihani wa form four yaliyotangazwa leo .zaidi ya nusu ya wanafunzi wamepata sifuri.sasa cha kujiuliza hapa ni je mgomo wa walimu umeisha?
 
Hili ni tatizo na sio changamoto tena. Lazima tutafute njia mbadala ya kulitatua.
 
Na kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini, hata wananchi wanailaumu serikali kwa majukumu ambayo hata wao kama wazazi wangepaswa kuyatekeleza (mfano kulipa ada, kununua daftari, kuhimiza attendance, kuhakikisha homeworks zinafanyika)
 
Too bad. yaani mtu asome miaka minne halafu apate sifuri.Hali ni mbaya. Hatupaswi kucheka...tunapaswa kutafakari kama Taifa
 
kati ya watahiniwa 397,136 waliofanya mtihani, walifaulu ni 126,847 (daraja i-iv)

daraja I- 1,641 (0.4%)
daraja II- 6,453 (1.6%)
daraja III- 15,426
(3.9%)
daraja IV- 103,327
(26.0%)
daraja 0- 240,903
(60.7%)

sasa wanaoweza kwenda form 5 na 6 ambao ni kuanzia daraja la I-III jumla yao ni 23,520 (elfu ishirini na tatu mia tano na ishirini) kati ya wanafunzi 397,136 (laki tatu tisini na saba elfu mia moja thelasini na sita)
hii ni sawa na 5.9224%.

HII NDIO NCHI YETU NA VIJANA WAJAO WA KUJENGA TAIFA, TUNAWAITA TAIFA LA KESHO.
Pamoja ya kwamba hujaajiriwa kwa kazi hiyo, lakini tunaomba tu utusaidie na analysis ya performance rate kati ya shule za akina Kayumba na zile za Private. Na hapo ndo utakapojua ni kwanini serikali inawakejeli walimu wa serikali wakiomba maslahi bora ya kazi. Kwa hakika, hawana shida maana hao 26000 wanaokwenda A level, asilimia 80 wanatoka shule za private ambako watoto wa wakubwa ndiko wanakosoma. Sisi na ujinga wetu tunabaki kuimba kidumu chama cha mapinduzi. Uongo mbaya napata hasira sana, mtu akijaribu kwa namna yoyote kunishawishi nishabikie CCM.
 
Ndio maaana jamaa kaamua kujiuzulu kwani kaona mfumo uliopo itakuwa vigumu kupunguza ziro zote hizo kaka ...inamana mpaka mzazi mtoto anapata ziro unakuwa hujajua tu kama mwenendo wake ki-masomo sio mzuri.unakuta mwalimu na mwanafunzi wanaangalia movies vibandani sasa hapo anayefundishwa na anayefundisha kuna kitu hapo.unakuta mwalimu hayuko tayari kufundisha na mwanafunzi hayupo vile vile kufundishwa!!
 
Mimi nilidhani kuwa tatizo ni lugha ya kiingereza, lakini nashindwa kumwelewa mwanafunzi anayeshindwa kufaulu hata somo la kiswahili(angalau kwa alama D)
 
Matokeo ya form four yanadhihirisha kuwa watoto wetu wanaenda sekondari kukua na sio kujifunza. Wamefanya mtihani wanafunzi 397,136, wamefaulu (walipata daraja la I, II na III kwa ujumla wao) 23,520 ambayo ni asilimia 5.9. Yaani kila watoto 100, ni watoto sita tu wamefaulu. Hali imezidi kuwa mbaya maana mwaka jana walifaulu asilimia kati ya 9 hadi 11, (sikumbuki vzr).

Hili ni zaidi ya bomu. :nono::nono:

source - Rafiki wa Elimu aliyechambua taarifa ya waziri

 
Ndio wanavyotaka sasa sie tufanyeje, ngoja na sisi tusaidie kulichochea hilo bomu kama nikufa wafe wao. I have nothing to loose my dear
 
Back
Top Bottom