Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

Uhalisia wa matokeo ya kidato cha nne 2012: Nini kimepelekea kufeli huku?

napita tuu, naona mada haijawagusa wengi means watu bado wapo kwenye mshtuko na matokeo. wil b bak:A S shade:
 
Kweli watu ni kama wapo kwenye mshangao, na hata yale mahosteli yatakuwa na watu wachache, na zinginhata wanafunzi watakuwa waoga au wanaweza fanyiwa kitu mbaya kirahisi zaidi
 
nitatoa ajira milioni moja .......JK
Karibia Robo ya milioni imeshindwa endelea mbele yaaan ihi nchi
 
Lakini hawa watoto nao wamezidi muda wote nikuchat tu na hii digitali ndio balaa
 
hawa wanafunzi hawako serious na shule kabisa hata wao ni wa kulaumiwa pia
 
Matokeo haya ya 4m4 yashakua mtaj kwa w2. Sahv kila shule naona inajitangaza kuwa na program ya reseters, twishen za uchochoron nazo zishapandisha ada. Ama kwel kufa kufaana
 
Wanjamvi nimeuliza swali hili ni katika hali ya kufikisha ujumbe kwa serikali ya CCM kwamba huwa ni viongozi wasiokuwa na VISION kabisa ndo maana leo tunaweza piga hatua 3 mbele kesho wakaturudisha mara 10 nyuma.

Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na shule za sekondari zilizokuwa zikimilikiwa na TEWW (Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima), utakumbuka kuwa kipindi hicho kulikuwa na shule chache za sekondari za serikali na binafsi pia, vilevile zilikuwa ni shule za gharama nafuu sana (sh. 35,000/=) kwa mwaka hivyo watoto wa maskini ndo likawa kimbilio letu. Pia ikumbukwe kua shule hizo zilikuwa hazina majengo hivyo zikawa zinaendesha shughuli zake kwenye shule za serikali kubwakubwa au vyuo vy ualimu vya serikali hasa kuanzia muda wa mchana au asubuhi kuliongani na uwepo wa vyumba vya madarasa na walimu.

Si siri shule hizi zilikuwa hazifanyi vizuri sana katika mitihani ya kitaifa (form two na form four) kwa sababu hasa ya changamoto zilizokuwepo, niseme tu kwamba leo hii kunawatu wamesoma hadi ngazi ya masters wakitokea katika shule hizo za TAASISI (kwa ninowafahamu).

Waziri wa elimu wa wakati huo (june 2002) akiwa J. J. Mungai, pamoja na mabadiliko mengine ya kiipuzi kwenye sekta ya elimu, na badala ya kutoa suluhisho ni jinsi gani shule hizi ziboreshwa (kama tunavyoweza fanya sasa kwa shule za kata) akaamuru shule hizo zifutwe zote, kwa vigezo tu kwamba hazifaulishi vizuri na wanafunzi wake wanaharibu thamani za shule au vyuo, hapa niseme tu kwamba hata mimi nilikuwa mhanga wa sakata hilo hivyo nililazimika kusota mitaani karibu miaka mitatu bila kwenda shule kwa kukosa ada za shule binfsi. Pia ikumbukwe kuwa Mungai alikuwa anamiliki shule nyingi na ilisemekana kuwa shule za Taasisi zilimpunguzia mapato.

Hivyo ndugu zangu tusije shangaa mtu anaamka kesho akisema shule za kata zifungwe badala ya serikali kuwekeza vy kutosha kuzikomboa shule hizi.
 
Suala la matokeo ya mwanafunzi ni matokeo ya mchanganyiko wa sababu. 1.Idadi ya walimu katika shule nyingi ni ndogo sana. Uwiano wa mwalimu kwa mwanafunzi inatisha. Unaweza kukuta Shule ina waalimu wawili, na wakisafiri Mwalimu wa zamu huachiwa Kiranja Mkuu, 2.Shule haina vitabu, hivyo hawana kitu cha kufanya wakati wakaapo peke yao bila mwalimu. 3.Shule haina hata chaki, za wao kufanya angalau mazoezi mwalimu anapokuwa hayuko nao, 4.Waalimu wenyewe wako kwenye mgomo, baada ya mkuu wa kaya kuwataka wasioridhika na mishahara waache kazi, walimu wote walikwisha acha kazi, wamebaki na ajira tu. 5.Hebu pitia walimu uone kama walipata vyeti kihalali, wapo waalimu ambao wao wenyewe wakifanya mitihani na watoto, utashangaa watapata F kwenye masomo wanayofundisha wenyewe. 6.Hata wazazi, hawana muda wa kuhoji, tunakuja kushtuka tunapoona matokeo, kana kwamba yamepikwa leo wakati tangu wameanza form one, tuko nao.
"TUSILAUMU TULIPOANGUKIA, TUCHUNGUZE TULIPOJIKWAA"
 
Wazifute wakati ndo wamewekeza kwenye ujinga!!!!!!!
Unachokiona na kusikia ni matokeo ya mipango madhubuti ya serikali. Zunguka Nchi nzima kuanzia kaskazini-kusini, mashariki -magharibi, uniambie kama utamkuta mtoto wa kiongozi yeyote wa serikali ya Tanzania anaesoma s.t Kayumba au hata shule za kata. Hii ina maanisha shule za serikali hazina mchungi, zinajiendea zenyewe! Na kwa mantiki hiyo serikali haiwezi kuona umuhimu wa kuboresha elimu kwa shule zake, ili iweje ili hali watoto wao hawasomi huko???

Ili uwe sehemu ya suluhisho, lazima kwanza uwe sehemu ya tatizo. Kwa serikali, elimu kushuka kwa kiasi kikubwa namna hiyo, sio issue kwao. The big issue ni kuiba na kupeleka watoto wao nje wakapate elimu bora na matibabu bora. Watanzania waliowengi watateseka sana na mfumo uliopo kwa leo. Sio chadema wala ccm wenye uwezo wa kuboresha elimu yetu. Nikitazama upande wa pili wa shilingi, hakuna kiongozi yeyote wa upinzani anaesomesha mtoto shule zetu za serikali, hili halina ubishi sababu nao sio sehemu ya matatizo ya Watanzania!!!! Watapiga kelele pale madhara yanapotokea, lakini sio kutatua tatizo.

Watasema, fulani ajiuzulu, fulani apishe uchunguzi.........etc. Lakini swali ni je, kwa nini hawakuyapigia kelele kabla ya matokeo??? Ni ukweli usiopingika kwamba, viongozi wetu wanatafuta cheap popularity sana kutoka kwa watanzania. Ni dhahiri kuwa wanajua mfumo wa elimu yetu ni mbovu na ndio maana watoto wao hawapelekwi shule za kata. Na kwa kujua hilo, wanatambua wazi kuwa matokeo hayataweza kuwa mazuri hata kwa gharama za uchawi!!! Ila wanasubiri bomu likishalipuka, nao wanaibuka kila mtu na jukwaa lake.

Lakini pia kuna swala lingine ambalo lipo wazi kabisa. Mwaka huu mwanzoni, serikali ililazimika kuchelewesha matokeo ya darasa la saba kutokana na kuanguka kwa watoto wetu. Kilichotokea, kila mtu anakijua. Badala ya kupeleka sekondari waliopata vigezo vya kujiunga na sekondari kama sheria inavyosema, wao walilazimika kupunguza alama za ufaulu. Which means idadi ya wajinga imeendelea kujiunga na kidato cha kwanza.
Katika hili wadau tuwe na subira kwani huu ni mwanzo wa matokeo mabaya. Sipendi anguko hili kwa sababu miaka michache ijayo hatutaweza kuwajibu hawa jamaa watakapoamua kujua ni kwa nini elimu imeporomoka kwa kiasi kikubwa na sisi tukanyamza kimya wakati tatizo lilikuwa na dalili toka mwanzo!!!!!!!!!!

Mleta mada, kwa kifupi sana; ccm haiwezi kuzifuta shule za kata kwani wao wanafurahia haya matokeo. Kwao wanapendezwa sana na watu wanapokuwa wajinga sababu ni rahisi sana kuwaburuza na kuwarubni na kanga, pombe, t-shirt................etc.
Hawa watu miaka ijayo hawana kazi, so hata wakinunuliwa kwa 5000 ili wawape kura inawezekana kabisa.
 
ndugu zangu watanzania huwezi kunyanyua elimu ya nchi pasipo kuangalia maslahi ya walimu, mahitaji ya wanafunzi kwa maana ya maabara na vitabu, madarasa na mazingira kuwa mazuri ya walimu na wanafunzi kwa ujumla sasa serikali ya tanzania ina washurutisha walimu kufanya kazi kwa lazima pasipo sikiliza mahitaji yao na kuandaa mazingira mazuri kwa mwanafunzi.
 
Na zile shule za taasisi nadhani zitaprosper maana wanafunzi wengi watahitaji kurisiti.
 
Hakuna shaka kuwa idadi ya wanafunzi wa kidato cha nne waliofeli ambayo ni zaidi ya 200,000 ni bomu ambalo litalipuka wakati wowote.Idadi hii haina tofauti kubwa na idadi ya mwaka jana na wengi wao wakitoka shule za kata maarufu kama st kayumba.Haya ni matokeo ya serikali kujipiga kifua kuwa imefanyikiwa kupanua elimu ya sekondari huku ikiziba masikio kuhusu ubora wa shule hizo.Bila shaka wanafunzi hawa ambao kwa kiasi kikubwa hawana nafasi katika soko la ajira huku matumaini ya wazazi masikini na walipa kodi yakienda na maji.Swali ni nani bomu hili litamlipukia?
 
naweza kukwambia kuwa wanafunzi wote walikuwa wanatumia mambo hayo yafuatayo,na hakuna asie elewa matatizo ya mitandao ya kijamii haswa inapogeuka kuwa ni mitandao ya kutongozeana na kutafuta wapenzi,matokeo yake kwa mwanafunzi ni kufeli,na kwa mwanamke ni kuacha na mumewe,au mke kutoroka,na anaefanya kazi maofisini akiiendekeza sana,si ajabu akafukuzwa kazi.
1: htc-opera-ul-facebook-phone-0.jpg2:twitter-logo-bird.gif3:whats.jpg4:New-Android-Launch.jpg
 
HIZI ZAWEZA KUWA SABABU ZA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUFANYA VIBAYA MTIHANI WAO WA MWISHO MWAKA 2012


1. Aina ya vitabu vya kujifunzia (Unyangwine)
2. Uhaba wa walimu.
3. Uhaba wa vitabu vya kiada na ziada.
4. Walimu wa muda mfupi aka Voda Fasta
5. Mtihani wa kidato cha pili kufutwa.
6. Kutowajibika wa wazazi/walezi kwa watoto. Watoto wamebinafisishwa.
7. Mazingira mabovu ya walimu.
8. Mazingira ya shule za kata, hakuna hosteli kwa vijijini wanafunzi wamepanga, shule ziko mbali na mazingira ya nyumbani.
9. Utokuwepo wa maabara
10. Ukosefu wa maktaba, imesababisha kutokuwepo kwa kuondoa utamaduni wa kujisomea.
11. Alama za ufaulu wa darasa la saba ziko chini.
12. Uvunjifu wa sheria za mitihani husan darasa la saba.
13. Kubadilika kwa mihutasari mara kwa mara.
14. Walimu kupewa semina mbalimbali ili kupata maarifa mapya.
15. Utandawazi kama sio utandawizi
 
HIZI ZAWEZA KUWA SABABU ZA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KUFANYA VIBAYA MTIHANI WAO WA MWISHO MWAKA 2012


1. Aina ya vitabu vya kujifunzia (Unyangwine)
2. Uhaba wa walimu.
3. Uhaba wa vitabu vya kiada na ziada.
4. Walimu wa muda mfupi aka Voda Fasta
5. Mtihani wa kidato cha pili kufutwa.
6. Kutowajibika wa wazazi/walezi kwa watoto. Watoto wamebinafisishwa.
7. Mazingira mabovu ya walimu.
8. Mazingira ya shule za kata, hakuna hosteli kwa vijijini wanafunzi wamepanga, shule ziko mbali na mazingira ya nyumbani.
9. Utokuwepo wa maabara
10. Ukosefu wa maktaba, imesababisha kutokuwepo kwa kuondoa utamaduni wa kujisomea.
11. Alama za ufaulu wa darasa la saba ziko chini.
12. Uvunjifu wa sheria za mitihani husan darasa la saba.
13. Kubadilika kwa mihutasari mara kwa mara.
14. Walimu kupewa semina mbalimbali ili kupata maarifa mapya.
15. Utandawazi kama sio utandawizi


Hapo kwenye red! Kha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaa!

Hasara ya chama kimoja kwa miaka 51 ya uhuru!
 
mimi sijashawishika kwamba mwaka huu F4 wamefeli sana. ninachoamini ni kuwa haya ndiyo matokeo halisi baada ya ndalichako kubana mianya ya kuvuja kwa mitihani.period.
 
KATUNI(725).jpg

Maoni ya Katuni


Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ya mwaka 2012 yaliyotolewa na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) na kutangazwa juzi na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, yamedhihirisha kuwa kiwango cha elimu nchini kinazidi kuporomoka.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, asilimia 60 ya watahiniwa wamefeli. Wanafunzi waliofeli kwa maana ya kupata sifuri ni 240,903. Waliopata daraja la nne ni 103,227, waliopata daraja la tatu ni 15,426, waliopata daraja la pili ni 6,4,53 na waliopata daraja la kwanza ni 1,641.

Pamoja na kusema kuwa waliopata daraja la nne nao wamefaulu, huko ni kujidanganya kwa kuwa kiuhalisia kupata daraja la nne kwa miaka ya sasa ni sawa

na kufeli kwa kuwa mhitimu wa aina hiyo ni nadra sana kupata nafasi ya ajira au nafasi ya masomo zaidi katika vyuo. Kimsingi, tunaweza kusema ukweli kwamba waliofeli ni daraja nne na daraja sifuri ambao jumla yao ni 344,230 kati ya 367,750, yaani asilimia 93.6 wamekwama.

Wadau kadhaa wametoa maoni yao kuhusiana na matokeo hayo mabaya hususan kwa upande wa shule za serikali wengi wao wakisema kuwa yamechangiwa na

mfumo mbovu wa elimu nchini na kutowajali walimu kwa maana ya kuwapa maslahi mazuri. Wapo baadhi waliosema kuwa aibu hiyo imechangiwa na uhaba wa walimu na ukaguzi wa kina kutofanyika katika shule.

Wengine wamesema ni sababu ya mfumo mbovu wa elimu hususan mtaala ambao umesababisha elimu kuwa mahututi. Wakati wadau wa elimu wakibainisha sababu za wanafunzi wengi kufeli, akitangaza matokeo hayo, Dk. Kawambwa alitaja sababu ya kutofanya vizuri kwa shule nyingi hasa za vijijini kuwa ni kukosekana kabisa kwa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na upungufu wa walimu wa masomo mengine.

Aidha, alitaja sababu nyingine kuwa ni kukosekana kwa maabara kwa shule za mikondo ya sayansi na maktaba za kujisomea pamoja na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada katika baadhi ya shule.

Kadhalika, matokeo hayo yamebainisha kuwa shule za sekondari za serikali, zimefanya vibaya kwenye kundi la shule zenye watahiniwa 40 au zaidi, baada ya shule 18 kati ya 20 zilizofanya vizuri kuwa za binafsi.

Kwa ujumla, matokeo hayo yametuachia changamoto kubwa; kwamba sisi kama taifa tunapaswa kuketi chini na kujiuliza ni sababu zipi zimechangia hali hiyo na kupanga mikakati ya kukabiliana na aibu hiyo.

Hali inaonyesha kuwa serikali haiwezi kuendesha elimu peke yake hivyo ni jukumu la kila mmoja kuanzia watu binafsi, asasi na vyama vya siasa kutoa mchango wake kuokoa elimu yetu. Juzi, Dk. Kawambwa alitaja baadhi ya mikakati ya serikali katika kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo.

Mikakati mingine alisema ni ile ya kuboresha miundombimu iliyoko katika shule kwa kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara na kuendelea kutoa ruzuku ya Sh. 25,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka, nusu yake ikitumika kununua vifaa vya

kufundishia na kujifunzia. Aidha, alisema wizara itaendelea kuzishauri halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule na kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa shule na kuwawezesha waratibu elimu kata na wakuu wa shule kufanya ukaguzi wa ndani katika shule za sekondari kwenye maeneo yao.

Hata hivyo, mwenendo mzima wa uendeshaji elimu nchini unaonyesha kuwa serikali imekuwa ikitamka mikakati ya kubiliana na changamoto hizo bila kuzitekeleza kwa kutoa kisingizio cha uhaba wa fedha.

Kwa mfano, mwaka juzi, idadi kubwa ya walimu waliopangiwa ajira katika halmashauri nchini walikutana na mateso baada ya kusota kwa miezi kadhaa bila kulipwa fedha za kujikimu, hali iliyosababisha wengi kuzikimbia ajira hizo.

Vilevile, mkakati wa kujenga nyumba za walimu katika maeneo ya vijijini sambamba na kuboresha mazingira ya shule hususan za kata umeshindikana kwa muda mrefu, hali inayosababisha walimu wengi wanaopangiwa ajira katika maeneo hayo kutokwenda ama kwenda na baadaye kuzikimbia ajira hizo.

Hatuna budi kukubali kwamba elimu yetu ni mahututi na inahitaji tiba ya kudumu, hivyo kila mmoja ajipange kwa kutoa mchango wake ili tuzikabili changamoto hizo ambazo zinatuathiri wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Kwa matukio yalitokea kwenye Mkutano wa Bunge wa hivi karibuni, kwa serikali kukwepa kuwajibika kuhusiana na mwenendo mzima wa sekta ya elimu na kujificha katika kichaka cha kutaka iachwe ijisafishe yenyewe ikisaidiwa na wabunge wa chama tawala kuwa

sehemu ya kuficha udhaifu huo, matokeo haya yanaifichua na kutaka hatua za haraka kukomboa elimu ya taifa hili. Kinachotakiwa sasa ni uwajibikaji wa kweli na si ghiliba za kisiasa za kuwepa wajibu. Uwajibikaji huu wafaa uanze na uongozi wa juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kama kweli tunataka kutoka katika mkwamo huu.



CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom