Uhamiaji hawaoni aibu kutoa passport laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Uhamiaji hawaoni aibu kutoa passport laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Uhamiaji wanakuuliza unataka Passport ya nini?

Unawaambia ya kusafiria

Unaulizwa safari ya Masomo , kazi au matembezi

Unawajibu matembezi

Wanakwambia ambatanisha barua ya Mwaliko wa huyo aliekualika

Hahahah zama hizi tena mualiko binafsi wa kirafiki mtu akutumie barua posta ya kukualika?

Kuna baadhi ya mahitaji unalazimisha watu wakatengeneze vitu vya kughushi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimbele mbele chote hicho kumbe hauna passport!!

Kweli passport ni kitu kikubwa sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninayo napigania Haki za vijana wanaoshindwa kupata passport ili waombe scholarship,vijana wanaoshindwa kufanya mitihani British council kwa kukosa passport
Hivi unajua kuwa asilmia kubwa ya scholarship za Tanzania asilimia tisini na Tisa ni wahindi wa Tanzania ndio huzipata?

Nenda kaangalie siku mitihani ya British council ikifanywa ambacho ndicho kigezo.muhimu.cha kupata scholarship.wanaofanya Ni watoto wa wahindi watupu huoni mswahili .

Ajira nje Ziko kibao Hadi za kulima nje Kama kanada nk issue vijana hawawezi omba online sababu passport hawana.Passport asilimia kubwa unakuta wanazo maafisa wa Serikali na familia zao, wahindi na waarabu

Waambie uhamiaji watoe takwimu za breakdown hao laki mbili waliowapa waweke maafisa serikali Ni wangapi na familia zao ,wahindi Ni wangapi na waarabu Ni wangapi na waswahili vijana ambao sio wazee wamewapa wangapi?
 
Uleanzisha uzi kichwa chako kibovu, hivi unajua unyeti na gharama yakutengeneza passport1? Ishu za passport si za kukurupuka! Na hakuna nchi duniani inayotegemea pesa kwenye miradi kama ya passport, passport ukitaka kuifanya biashara yataibuka mengi haswa swala la rushwa na urasimu, nawapa kongole kwa wanachokifanya uhamiaji, mnataka passport zipatkane hovyo alafu mkafanye matukio nchi za watu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukimpata pasi ndio umepata tikiti ya kisafiri? Kila nchi ina utaratibu wa kuingia, nikiwa na pasi nitaenda ubalozini na wao ndio wana jukumu la kunikubalia(kunipa visa) au kunikatalia kulingana na vigezo walivyojiwekea. Uhamiaji wananiuliza naenda wapi kwani wananipa visa??
 
Tanzania is a failed state.

( Kilichopo ni Genge la CCM na watoto wao, kujipa na kutafuna Keki ya Taifa )

Wewe kajamba nani ukionekana unasumbua, unapewa Rushwa ya Vyeo ( Vya Kuteuliwa ).

Ukionekana Hata Vyeo Hutaki, Unavimba Yatakupata Ya Tundu Lissu.

In short, Nchi Imesimama "Hakuna anayewaza kwamba itapigaje hatua"

Hata Wanajeshi wanaowasaidia CCM kubaki madarakani "Wametelekezwa". Wanalipwa Kiduchu Mno.

Kilichobaki Wanapewa Maisha Fake Tu ( Kupanda Dala Dala Bure - "Kibabe Tu, Maana Wamiliki Wa Dala Dala Kodi Wanalipa Kama Kawaida )
 
Uleanzisha uzi kichwa chako kibovu, hivi unajua unyeti na gharama yakutengeneza passport1? passport ukitaka kuifanya biashara yataibuka mengi haswa swala la rushwa na urasimu

Sent using Jamii Forums mobile app

wewe jamaa ni pimbi sana kutengeneza kile kijitabu chenye vikaratasi vichache vile unasema kuna unyeti na gharama sasa wale wanaotengeneza bomu la nyukilia waseme nini. ebu fikiria upya rushwa na urasimu unatumika muda gani. alafu kukusahidia tu wabongo wachache ndio wanaojua humuhimu wa passport chek swala la NIDA watu wanalazimishwa kuchukua Id na no free sasa hizo passport unadhan ni kila mtu atazichukua . watu wenye nia yabkusafiri ndio wenye passport lakin wasiokuwa na fikra hizo wala awawazi kuwa nayo. ni serikali ingeweka mlango wazi kwa wenye maono ya kusafiri nje ya mipaka ya Tz wawe nazo. sasa hiv ni urasimu na rushwa kwa kwenda mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichoandika kinaonyesha kichwani kwako uko mweupe.Kule Kuna serikali,Polisi na mahakamani pia utashughulikiwa ukikosea huko huko

Kwa hiyo mumejibesha jukumu.la Polisi na mahakama ya dunia uwiii mbavu zangui Mimi.Hamuamini nchi zingine kuwa Ziko vizuri kupambana na wahalifu?

Mambo ya kimataifa yanatakiwa kuaminiana Mfano wewe umempa mtu passport anaenda marekani.Wewe hujampa Visa ya kuingia Marekani unaogopa Nini?

Wao ndio waliompa baada ya kujiridhisha wenyewe kuwa Ni mtu Safi.Sasa akiuza bangi kule wewe yanakuhusu Nini wewe hukumpa visa .Hata ukihojiwa unasema Mimi nilitoa passport sio visa
Lakini ukijitia ohhh mimi najua aliniambia anakuja huko na ushahidi fomu hii hapa aliyojaza Ina maana akidakwa na marawa ya kulevya wewe ndio mbeba lawama Kama facilitator kwa kukiri Mwenyewe

Nchi nyingi Wana avoid Hilo kuepuka
Hilo.Wewe toa passport usiulize anaenda nchi gani kufanya Nini sukumia Risk ubalozi unaotoa Visa

Unamuelekeza kichaa Mkuu.

Hajui anachokisema. Hajui tofauti ya Passport na Visa.
 
Kaka umeyaandika ninayoyawaza siku zote, sina hoja umenifirisi. Hoja nzito
Hivi ni sahihi Uhamiaji kutoa Passport mpya laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Nchi za wenzetu mfano Marekani passport na visa ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.

Mfano uhamiaji wangepewa lengo mfano la kutoa Passport milioni moja tu kwa mwezi kwa bei ya Passport ya shilingi laki moja na nusu serikali ingeingiza pato la shilingi bilioni 150 ambazo zingesaidia mno nchi.

Kikwazo kikubwa cha watu kupata Passport ni kuwa Afisa Passport hatakiwi kumuuliza mtu anaenda wapi kufanya nini akitaka kumpa. Hilo atapambana nalo Ofisi ya Ubalozi anakoenda akienda kuomba Visa. Wewe kila Mtanzania mpe passport mengine mwachie akapambane na hali yake mbele kwa mbele

Passport ni kitambulisho tu cha kawaida kama cha NIDA tofaiti iliyopo ni kuwa cha NIDA kinatambuliwa ndani ya nchi wakati passport ni kitambulisho cha raia cha Kimataifa .Mtu ruksa kuwa na passport hata kama hasafiri ni kitambulisho chake cha kimataifa.

Mtu anakiwa kuwa na vitambulisho viwili cha NIDA na passport

Uhamiaji wanaona passport kama kitu kikuubwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu Rwanda hapo mtoto akizaliwa anapewa vyote akitaka anapewa cheti Cha kuzaliwa na passport huulizwi unakwenda wapi kufanya Nini,Kenya na Uganda hivyo hivyo

Rwanda passport inspatikana ndani ya massaa matatu.macimum toka uwakilishe ombi lako

Haya masharti yaliyopo ndio yanazalisha rushwa ingekuwa mfano sharti Ni kitambulisho Cha taifa au cheti Cha kuzaliwa tu Nani akuombe rushwa kwa sababu ipi wakati umempa hati zote

Haya yaliyopo ndio yanazalisha urasimi na rushwa wewe utakuwa mmoja wa wafaidika unajua yakiondolewa rushwa hutapata
Hamia rwanda mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni sahihi Uhamiaji kutoa Passport mpya laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Nchi za wenzetu mfano Marekani passport na visa ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.

Mfano uhamiaji wangepewa lengo mfano la kutoa Passport milioni moja tu kwa mwezi kwa bei ya Passport ya shilingi laki moja na nusu serikali ingeingiza pato la shilingi bilioni 150 ambazo zingesaidia mno nchi.

Kikwazo kikubwa cha watu kupata Passport ni kuwa Afisa Passport hatakiwi kumuuliza mtu anaenda wapi kufanya nini akitaka kumpa. Hilo atapambana nalo Ofisi ya Ubalozi anakoenda akienda kuomba Visa. Wewe kila Mtanzania mpe passport mengine mwachie akapambane na hali yake mbele kwa mbele

Passport ni kitambulisho tu cha kawaida kama cha NIDA tofaiti iliyopo ni kuwa cha NIDA kinatambuliwa ndani ya nchi wakati passport ni kitambulisho cha raia cha Kimataifa .Mtu ruksa kuwa na passport hata kama hasafiri ni kitambulisho chake cha kimataifa.

Mtu anakiwa kuwa na vitambulisho viwili cha NIDA na passport

Uhamiaji wanaona passport kama kitu kikuubwa!
Nafikiri passport inaombwa na haigaiwi kwa hiyo sielewi hii post inalenga wapi kama watu Watanzania laki mbili wameomba na kupewa tukalalamikia hao milioni 55 ambao hawajaomba bado.
 
Nafikiri passport inaombwa na haigaiwi kwa hiyo sielewi hii post inalenga wapi kama watu Watanzania laki mbili wameomba na kupewa tukalalamikia hao milioni 55 ambao hawajaomba bado.
Inaombwa ndiyo ila wengi wanaoshindwa kuomba sababu ya hivyo vigezo vya Visa vya hovyo vilivyowekwa hivyo kuwanyima haki ya kuomba pia Wako wanaokataliwa sababu ya hivyo vigezo vya kuombea Visa ambavyo uhamiaji wamejigeuza maafisa ubalozi wa. Visa!!!! Mfano mtu anataka kuomba passport ili aombe scholarship au kazi online anajibiwa hatutoi kigezo hicho hatuna kwenye taratibu zetu!!!!! Kalete barua ya mwaliko na uthibitisho wa safari!!!! Ujinga mtupu
 
Uhamiaji wanakuuliza unataka Passport ya nini?

Unawaambia ya kusafiria

Unaulizwa safari ya Masomo , kazi au matembezi

Unawajibu matembezi

Wanakwambia ambatanisha barua ya Mwaliko wa huyo aliekualika

Hahahah zama hizi tena mualiko binafsi wa kirafiki mtu akutumie barua posta ya kukualika?

Kuna baadhi ya mahitaji unalazimisha watu wakatengeneze vitu vya kughushi

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na wewe 100% - kadiri wanavyoweka ugumu usio wa lazima wa upatikanaji wa Passport (Na huduma nyingine toka serikalini) automatically wanatengeneza mazingira ya watu kutumia njia mbadala; ikiwemo rushwa ofcourse, na kughushi. Mfano: Nakumbuka wakati fulani nilisikia kuna watu unawapa 50k tu then within 24 hours wanakukabidhi passport. A kind of arbitrage in social services, some guys are smart enough to exploit that gap.
 
Uleanzisha uzi kichwa chako kibovu, hivi unajua unyeti na gharama yakutengeneza passport1? Ishu za passport si za kukurupuka! Na hakuna nchi duniani inayotegemea pesa kwenye miradi kama ya passport, passport ukitaka kuifanya biashara yataibuka mengi haswa swala la rushwa na urasimu, nawapa kongole kwa wanachokifanya uhamiaji, mnataka passport zipatkane hovyo alafu mkafanye matukio nchi za watu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanao taka kufanya uhalifu nje hawawezi kukosa passport kwa swali la unaenda wapi kufanya nini.
Kuna fursa zinatokea ghafla ukitaka passport inachukua muda na mlolongo mrefu hadi unapitwa na fursa.
Kuna wagonjwa ambao hawawezi kuzunguka kufuatilia passport wanatakiwa wakatibiwe nje, kunakuwa na usumbufu mkubwa sana kwa mgonjwa na watu wanao muuguza wakati wanafuatilia passport na wakimaliza hapo waende kuzunguka kwenye foleni za visa ubalozi wa nchi aendayo.

Tubadilike tuache urasimu usio na lazima, laki moja na nusu kutengeneza passport ni pesa nyingi sana, hakuna cha ajabu kinachofanyika useme gharama kubwa.
 
Sema mimi kuna jambo limenitisha kidogo; Nilipata passport yangu miaka 12 iliyopita. Na by that time nilikuwa under 18, so mlezi wangu ndiye aliyefanya process zote. Tulikuwa na safari ya nje ya nchi then baada ya ile safari sikuwahi kutumia tena ile passport na apparently ilikuja kupotea mwaka 2016. Unfortunately, sikukariri namba ya ile passport (uzembe ofcoz😉) - wala mlezi wangu. Nilitoa taarifa polisi kama kawaida, na taratibu zinataka mtu apeleke tangazo kwenye gazeti la serikali kabla hajapewa nyingine.

Now here comes the issue; mimi nilisahau namba ya passport yangu iliyopotea. Kwa hiyo haiwezekani kutangaza gazetini mpaka niipate namba ya passport. Sehemu pekee ninayoweza kuipata namba ni uhamiaji. Kilichonitisha ni kuwa, uhamiaji pia hawana records zangu kabisa - as if sijawahi kupewa passport at all. Sababu inayotolewa ni moja; mabadiliko ya mfumo, kutoka zile 'za mkono' kuja hizi mpya 'mashine readable'.

Nilipopewa jibu hilo ofisi za uhamiaji mkoani, sikushangaa sana - maana wao walishauri nifike Dar nitasaidiwa. Ishu ni kuwa hata nilipoenda pale mambo ya ndani hawana records zangu!!! I was like,.. WTF 😳🙄😡 Nilicho-notice ni kuwa, mfumo huu mpya hauna taarifa za wamiliki wa passport zile za zamani otherwise uwe ume-upgrade personally.

Mimi ni mzembe bila shaka, lakini kwa hili uhamiaji nao dizaini ni wazembe zaidi yangu!😎
*I stand to be corrected*
 
Uhamiaji wanakuuliza unataka Passport ya nini?

Unawaambia ya kusafiria

Unaulizwa safari ya Masomo , kazi au matembezi

Unawajibu matembezi

Wanakwambia ambatanisha barua ya Mwaliko wa huyo aliekualika

Hahahah zama hizi tena mualiko binafsi wa kirafiki mtu akutumie barua posta ya kukualika?

Kuna baadhi ya mahitaji unalazimisha watu wakatengeneze vitu vya kughushi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mambo ya ajabu sana haya.
Kwani siwezi kuwa na pesa zangu nikahamua niende kutembea kama kutalii ughaibuni au kuangalia na kujifunza kuhusu masoko ya bidhaa flani au fursa flani ya kibiashara au ajira?
 
mawazo ya zamani sana uliyonayo. Ni yale walioambiwa watu TV na Fridge ni vyombo vya anasa. Utajuaje kama laki 2 wote ni saafi.
Baadhi ya wateendaji serikalini hovyo na wanafanya kazi Kama miroboti tu wakiwemo wa kitengo Cha passport

Nakumbuka Kuna kipindi kabla ya vyama vingi kwenda Zanzibar ulikuwa lazima uende na passport utake usitake.Na unagongewa visa ya kuingia Zanzibar .

Mtu binafsi ndiye alibadili Hilo anaitwa Mchungaji Mtikila.

Vyama vingi vilipoanza ilitakiwa kwa Sheria ya vyama iliyopo Hadi sasa kuwa ili Chama Chako Cha siasa kisajiliwe inatakiwa kuwa na wanachama Tanzania bara na Zanzibar.Mtikila akasajili wanachama Tanzania bara akagoma kwenda kusajili Zanzibar akasema kule Ni nchi nyingine ambayo kuingia lazima uende na Passport na Visa akasema hayuko tayari kusajili raia wa nchi nyingine kuwa wanachama wa Chama ili asajiliwe

.Akasema kwenda uingereza unahitaji passport na Visa inawezekanaje Chama kisajil raia Mfano wa uingereza kuwa wanachama wa Chama Tanganyika? Akaenda mahakamani passport zikafutwa na visa za kuingia Zanzibar zikafutwa

Msajili wa vyama akaona Ni kweli.Uhamiaji ndipo wakaamka usingizini na kufuta habari ya kwenda Zanzibar na passport!!!!

Hili la wao pia kudai vitu vinavyodaiwa mtu akiomba visa ubalozini kuvifanya ndio vigezo vyao vya kumpa mtu passport bado wako usingizini wanakoroma wakifanya kazi kea mazoea.Wanahitaji wa kusaamusha kuwa ohhhh you uhamiaji wake up acha kufanya kazi kwa mazoea!!!!
 
Back
Top Bottom