Uhamiaji hawaoni aibu kutoa passport laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Uhamiaji hawaoni aibu kutoa passport laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Idara ya UHAMIAJI ni jipu kubwa. Rushwa imetamalaki. Usipotoa rushwa utaulizwa maswali ya ajabu. Ndio maana wengine huenda nje ya nchi bila pssipoti wakirudishwa wanafungwa jela. UHAMIAJI wajirekebishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hao 200,000 wamepataje? Ni uhitaji na juhudi zao. Wewe lialia, ona shida kupanga foleni,ona shida kutafuta national ID utabaki kulalamika passport zimetolewa kwa wachache
 
Uleanzisha uzi kichwa chako kibovu, hivi unajua unyeti na gharama yakutengeneza passport1? Ishu za passport si za kukurupuka! Na hakuna nchi duniani inayotegemea pesa kwenye miradi kama ya passport, passport ukitaka kuifanya biashara yataibuka mengi haswa swala la rushwa na urasimu, nawapa kongole kwa wanachokifanya uhamiaji, mnataka passport zipatkane hovyo alafu mkafanye matukio nchi za watu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha wehu passport Nikitambulisho Kama Cha nida hata wew unahaki nacho kuwa nacho ndio maana hata ukienda katika mabank utakuwa wanainisha viambatanisho na passport ikiwemo

Tatizo watu mnachukulia passport Ni kitu Cha anasa Sana kumbe Cha kawaida saana yaan

kilicho akilini kitumie
 
😂 😂 😂
 
Kwani hao 200,000 wamepataje? Ni uhitaji na juhudi zao. Wewe lialia, ona shida kupanga foleni,ona shida kutafuta national ID utabaki kulalamika passport zimetolewa kwa wachache
Mtanzania asipolalamika maisha yake hayaendi.
 
Vibabu na vibibi mnaofanya kazi kwa mazoea kuwa toka enzi za Mwalimu tumekuwa tukifanya hivi. Hayo masharti nchi za wenzetu walishabadilisha miaka mingi nyinyi ni hayo hayo toka Tanzania ipate Uhuru .Hamstaafu tu? Mpishe vijana Wenye mawazo mapya?

Passport dunia ya Leo sio cheti Cha safari ni kitambulisho unachotumia kuomba kazi online ukiomba nje Kuna sehemu unatakiwa kujaza passport namba au ukiomba scholarship unatakiwa sehemu ujaze passport namba au ukitaka kufanya mitihani ya kimataifa online unajaza passport namba

Mfano mimi nataka kuomba labda scholarship au kazi online nakuja kukuomba unipe passport ili nitumie kuomba scholarship au kazi online unaniambie nilete barua ya mwaliko na uthibisho wa safari ninakoenda ili unipe passport hivi kichwani afisa passport wewe una akili au mjinga Fulani? Upo unafanya kazi Kama robot tu si ustaafu upishe Wengine au unasubiri redundancy ikupitie halafu uje kubweka humu kuwa umeonewa wewe ni mchapakazi?
Kada haya ndio Madhara ya Kuikumbatia serikali dhalimu ya CCM.

Je uko tayari kuinyima KURA ili sasa hayo yafanyike?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kada haya ndio Madhara ya Kuikumbatia serikali dhalimu ya CCM.

Je uko tayari kuinyima KURA ili sasa hayo yafanyike?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaninhiki ulishawahi sikia hata chadema wakiliongelea popote hata bungeni? Hoja nianzishe Mimi halafu nyie mdandie be original sio kudandia dandia tu hoja
 
Credit to Uhamiaji though. Basically hawataki kuwe na msululu mreeeeefu wa kila "tom and Jerry" anayetaka kuomba passport bila safari ya uhakika, in the process kuwacheleweshea wenye safari za ukweli. Kwa uzoefu wangu, hilo swali la "unaomba passport kwenda wapi" unaweza kulijibu kirahisi tu kwamba "ninajiandaa kwenda Kenya/Uganda/Rwanda/Burundi" kwa safari binafsi. End of story. Unapowapa majibu ya mashaka kwamba unataka passport sijui kwenda shule Canada, hapo unawapa nafasi ya kukudai vitu vingine kama invitation/admission letters etc.

Sidhani kama kuna mtu ambaye ameshanyimwa passport kwa kushindwa kujibu vizuri swali linalohusu lengo la kuomba passport.
Unaongea theory passport hawakupi hao uandike natarajia kusafiri.Lakini watakudai vidhibitisho vya hiyo safari .

Lakini pia bado hata kujibu hivyo hakufai sababu kuhitaji passport sio lazima uwe na safari Mfano kufanya mitihani ya kiingereza kwa wageni British council Tanzania kujaza form tu online Kuna sehemu.lazima ujaze passport number Sasa fikiria unataka passport unaanza kujaza unatarajia kwenda Sijui nchi gani .What for?
 
Kwani hao 200,000 wamepataje?
Asilimia kubwa hapo kwenye hiyo laki mbili

Kundi la kwanza kubwa Ni wanasiasa na familia zao

Kundi kubwa la pili wafanyakazi wa serikali na taasisi zake

Kundi kubwa la tatu wahindi na waarabu

Asilimia kiduchu iliyobaki ndio waswahili

Waweke na takwimu za passport zilizokataliwa na sababu za kukataa
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu msamehe
Vibabu na vibibi mnaofanya kazi kwa mazoea kuwa toka enzi za Mwalimu tumekuwa tukifanya hivi. Hayo masharti nchi za wenzetu walishabadilisha miaka mingi nyinyi ni hayo hayo toka Tanzania ipate Uhuru .Hamstaafu tu? Mpishe vijana Wenye mawazo mapya?

Passport dunia ya Leo sio cheti Cha safari ni kitambulisho unachotumia kuomba kazi online ukiomba nje Kuna sehemu unatakiwa kujaza passport namba au ukiomba scholarship unatakiwa sehemu ujaze passport namba au ukitaka kufanya mitihani ya kimataifa online unajaza passport namba

Mfano mimi nataka kuomba labda scholarship au kazi online nakuja kukuomba unipe passport ili nitumie kuomba scholarship au kazi online unaniambie nilete barua ya mwaliko na uthibitisho wa safari ninakoenda ili unipe passport hivi kichwani afisa passport wewe una akili au mjinga Fulani? Upo unafanya kazi Kama robot tu si ustaafu upishe Wengine au unasubiri redundancy ikupitie halafu uje kubweka humu kuwa umeonewa wewe ni mchapakazi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongea theory passport hawakupi hao uandike natarajia kusafiri.Lakini watakudai vidhibitisho vya hiyo safari .
Watakudai uthibitisho wa safari kama utawaambia unaenda kufanya shughuli maalumu - invitation ya mkutano, admission letter ya shule, medical treatment etc. Sina uhakika sana kama kukudai hivyo vitu is to your advantage ili wakupatie passport haraka ama la. Lakini ukiwaambia ninajiandaa kwa mfano kwenda safari binafsi tu hapo Uganda hawatakudai chochote kuhusu safari zaidi ya those other key supporting documents. Nina uhakika 200% na hiki ninachokisema.

All in all, passport hi haki ya kila raia na hakuna evidence kuwa kuna Mtanzania yeyote amewahi kunyimwa passport kwa kushindwa tu kuelezea vizuri madhumuni ya safari yake. Kimsingi Uhamiaji wala hawaconcentrate saaana kwenye madhumuni ya safari, zaidi huwa wanataka uthibitisho wa uraia na mara nyingi wale wanaotokea mipakani (Kigoma, Ngara etc) usumbufu wake huwa ni mkubwa zaidi.
 
Tatizo ni Pale uhamiaji wanapoanza kufanya kazi za ubalozi. Kuuliza maswali yasiyowahusu labda Tatizo ni wale wanaokwenda nchi zisizohitaji visa kama South. Ila wanaokwenda nchi za magharibi hawa kimbembe ubalozini
Ubalozini tumbo laweza kukukoroga
 
Vibabu na vibibi mnaofanya kazi kwa mazoea kuwa toka enzi za Mwalimu tumekuwa tukifanya hivi. Hayo masharti nchi za wenzetu walishabadilisha miaka mingi nyinyi ni hayo hayo toka Tanzania ipate Uhuru .Hamstaafu tu? Mpishe vijana Wenye mawazo mapya?

Passport dunia ya Leo sio cheti Cha safari ni kitambulisho unachotumia kuomba kazi online ukiomba nje Kuna sehemu unatakiwa kujaza passport namba au ukiomba scholarship unatakiwa sehemu ujaze passport namba au ukitaka kufanya mitihani ya kimataifa online unajaza passport namba

Mfano mimi nataka kuomba labda scholarship au kazi online nakuja kukuomba unipe passport ili nitumie kuomba scholarship au kazi online unaniambie nilete barua ya mwaliko na uthibitisho wa safari ninakoenda ili unipe passport hivi kichwani afisa passport wewe una akili au mjinga Fulani? Upo unafanya kazi Kama robot tu si ustaafu upishe Wengine au unasubiri redundancy ikupitie halafu uje kubweka humu kuwa umeonewa wewe ni mchapakazi?
Have a drink... Nakuja kulipa
 
Hivi ni sahihi Uhamiaji kutoa Passport mpya laki mbili kwenye nchi yenye watu milioni 55?

Nchi za wenzetu mfano Marekani passport na visa ni chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.

Mfano uhamiaji wangepewa lengo mfano la kutoa Passport milioni moja tu kwa mwezi kwa bei ya Passport ya shilingi laki moja na nusu serikali ingeingiza pato la shilingi bilioni 150 ambazo zingesaidia mno nchi.

Kikwazo kikubwa cha watu kupata Passport ni kuwa Afisa Passport hatakiwi kumuuliza mtu anaenda wapi kufanya nini akitaka kumpa. Hilo atapambana nalo Ofisi ya Ubalozi anakoenda akienda kuomba Visa. Wewe kila Mtanzania mpe passport mengine mwachie akapambane na hali yake mbele kwa mbele

Passport ni kitambulisho tu cha kawaida kama cha NIDA tofaiti iliyopo ni kuwa cha NIDA kinatambuliwa ndani ya nchi wakati passport ni kitambulisho cha raia cha Kimataifa .Mtu ruksa kuwa na passport hata kama hasafiri ni kitambulisho chake cha kimataifa.

Mtu anakiwa kuwa na vitambulisho viwili cha NIDA na passport

Uhamiaji wanaona passport kama kitu kikuubwa!
majanga
 
Mtanzania asipolalamika maisha yake hayaendi.
Kudai huduma Bora ni malalamiko?
Akitokea mtu akasikiliza madai yetu haya halafu akakisambaratisha kitengo chote Cha uhamiaji Cha passport na wengine kuwatumbua kwa kufanya kazi kimazoea na kutokidhi matakwa ya wateja waomba passport msije kupiga yowe humunkuwa ohhhh sisi hizo taratibu tulizikuta miaka na miaka mnatuonea!! Endeleeni hivyo hivyo kufanya kazi kama robot
 
Back
Top Bottom