Sema mimi kuna jambo limenitisha kidogo; Nilipata passport yangu miaka 12 iliyopita. Na by that time nilikuwa under 18, so mlezi wangu ndiye aliyefanya process zote. Tulikuwa na safari ya nje ya nchi then baada ya ile safari sikuwahi kutumia tena ile passport na apparently ilikuja kupotea mwaka 2016. Unfortunately, sikukariri namba ya ile passport (uzembe ofcoz😉) - wala mlezi wangu. Nilitoa taarifa polisi kama kawaida, na taratibu zinataka mtu apeleke tangazo kwenye gazeti la serikali kabla hajapewa nyingine.
Now here comes the issue; mimi nilisahau namba ya passport yangu iliyopotea. Kwa hiyo haiwezekani kutangaza gazetini mpaka niipate namba ya passport. Sehemu pekee ninayoweza kuipata namba ni uhamiaji. Kilichonitisha ni kuwa, uhamiaji pia hawana records zangu kabisa - as if sijawahi kupewa passport at all. Sababu inayotolewa ni moja; mabadiliko ya mfumo, kutoka zile 'za mkono' kuja hizi mpya 'mashine readable'.
Nilipopewa jibu hilo ofisi za uhamiaji mkoani, sikushangaa sana - maana wao walishauri nifike Dar nitasaidiwa. Ishu ni kuwa hata nilipoenda pale mambo ya ndani hawana records zangu!!! I was like,.. WTF 😳🙄😡 Nilicho-notice ni kuwa, mfumo huu mpya hauna taarifa za wamiliki wa passport zile za zamani otherwise uwe ume-upgrade personally.
Mimi ni mzembe bila shaka, lakini kwa hili uhamiaji nao dizaini ni wazembe zaidi yangu!😎
*I stand to be corrected*