Credit to Uhamiaji though. Basically hawataki kuwe na msululu mreeeeefu wa kila "tom and Jerry" anayetaka kuomba passport bila safari ya uhakika, in the process kuwacheleweshea wenye safari za ukweli. Kwa uzoefu wangu, hilo swali la "unaomba passport kwenda wapi" unaweza kulijibu kirahisi tu kwamba "ninajiandaa kwenda Kenya/Uganda/Rwanda/Burundi" kwa safari binafsi. End of story. Unapowapa majibu ya mashaka kwamba unataka passport sijui kwenda shule Canada, hapo unawapa nafasi ya kukudai vitu vingine kama invitation/admission letters etc.
Sidhani kama kuna mtu ambaye ameshanyimwa passport kwa kushindwa kujibu vizuri swali linalohusu lengo la kuomba passport.