Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Mkuu it doesn’t matter kikubwa ubinaadam
 
Acha kukurupuka hatujalaumu kuhusu ukamataji.

You are out of point.Check your side
Hamjalaumu kuhusu ukamataji, mmelaumu kuhusu nini ?

Kama unakubali kwamba alivyokamatwa ni sawa hapa tunabishania nini cha zaidi ???
 
Imebidi nirudi kusoma upya. Wenda alikosema kuandika lakn barrier ya kuingia tarime ni kirumi pale darajani. Samahan kwa hilo.

Kuhusu njia ya kuingilia Musoma sio moja ndio maana nimekwambia labda kama unazungumzia main road na njia fupi ndio ipo moja ila kuna njia nyingine za kuingia musoma sema niza vumbi na mzunguko.
 
Ukiandika kiingereza ndo unakuwa wa ovyo zaidi.
 

Siwapendi baadhi yao wanapokuwa kazini kwa kujifanya wakali bila kosa kumbe ni mbinu za kuomba rushwa

Lakini katika hii kesi ni tofauti walikuwa wapo kwenye majukumu yao na kulinda amani

Kama alikatisha bila vibali maalumu hilo ni kosa lake ila sio atetewe kwa sababu ni mjamzito

Wajawazito wangapi wanakamatwa wakiwa na madawa ya kulevya?
Huruma iwepo ila sio kuvunja sheria
 
Kiubinadamu si sahihi.Na hawana fungu la kuhudumia wahamiaji dharura kama hizo labda atoe ya kwake mfukoni
 
Kiubinadamu si sahihi
Sio kiubinadamu tu, pia ata kiusalama sio sahh. Vipi kama alikuwa ni jasusi wa nchi jirani alaf baada ya kumterekeza hospital na yeye anapata mwanya wa kufanikisha adhima yake kwa uhuru zaidi baada ya kupona au ata akiwa hapo hapo hospital?

.Na hawana fungu la kuhudumia wahamiaji dharura kama hizo labda atoe ya kwake mfukoni
Vipi wale waethiopia wanaokamatwa kila siku wakiwa kwenye hali mbali na njaa huwa hawapewi chakula? Na vip gharama za kuwarudisha nchin kwao huwa zinagharamiwa na nan?

Vip kwan haiwezikan akahudumiwa mda wanawasiliana na watu wa ubalozi wa nchi aliyotoka ili wajue wanasaidiaje?
 
Kwanza kabisa namshukuru huyo mama kama kajifungua salama. Mungu amtangulie yeye na mwanae wawe salama. Kama kuna namna ya kumtumia kakitu weka namba za simu au akaunti.

Kuhusu uhamiaji nao sijaona walipokosea. Walikuwa kwenye majukumu yao. Sheria huwa lazima ifuatwe na huruma ndo huwa ni hiari.

Hakuna nchi utaingia bila kuwa na makaratasi. Kwa nchi baadhi ya nchi za jirani huwa kuna border pass kwa wakazi wa sehemu za jirani sana na mpaka. Lakini pia bado zile passport za dharura huwa ni rahisi kuzipata.

Border ya Ngara walifanya makosa kumruhusu bila documents. Watanzania tuamke na kuacha kulalamikia mambo yenye manufaa kwa usalama wa taifa zima.

Uhamiaji wakishirikiana na NIDA waendelee kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu haya mambo. Ikiwezekana waanzie mashuleni huko. Hata TRA nao wapambane kutoa elimu ili kuwa na wananchi wazalendo wanaojua wajibu wao kwa nchi. Itapunguza kulaumiana.

Mwisho kama unajua kipato chako hakiruhusu usitoe papuchi yako ovyo kwa mgeni. Pia wanaume tuache ngono zembe ili kutowaleta viumbe wasio na hatia kuja duniani kuteseka bila sababu.
 
Nadhan hlo jambo ni sahihi. Na sehemu ya mafunzo ni hapo kwenye tukio. Wakati mwingine unaweza kumwambia mtu kitu kupitia vyombo vya habari lakininsi wote utaweza kuwapata maana si kila mtu ana hulka ya kuangalia taarifa ya habari.

Hivyo kupitia ugaguzi wa njiani ni jambo linaloweza kukupa imani kuwa kumbe ni muhimu kuwa na kitambulisho. Na pia huwezi jua siku hiyo mnasimamishwa kama kuna mtu alikuwa anatafutwa.

Usalama wa nchi yetu ni jukumu letu raia. Askari wa majeshi yetu wote wanafanya kazi kubwa sana ya kutulinda huku sisis tukiwa tumelala usingizi fofofo. Tuheshimu kazi za watu jamani.

Mwisho, hao askari walipaswa kuwajibika kwa huyo mama kupitia mamlaka zao, maana kama huyo mama angeruhusiwa kienyeji then tukio la kihalisi likafanyika kupitia yeye, lawama zote zingerudi tena kwa hao askari na tena ingeweza kuhatarisha kazi zao.

Lakini pia je, serikali ilipaswa kuwa na fungu la dharura kwa kesi kama hizi. Maana wanafanya majukumu yao kwa sheria lakini wakipata shida wanaachwa wao kuwajibika, kwa mshahara gani?

Tuache lawama jamani. Hao ni binadamu kama sisi tu.
 
Toa location ya ofisi ya uhamiaji Kuna wadau wanaweza kutoa msaada
 
Zamani nilikuwa nachukia sana wazungu na waasia wavyotubagua, Mara watuite nyani Mara sokwe!

Lakini baadae nilikuja gundua hakuna majitu mabaguzi Kama maafrica, hasa matanzania, eti unamkamata msomali kwenye Lori, anaenda Malawi, kwao anakimbia Vita, we unamfunga jela!! Si usokwe huo?
 
Mbaya zaidi mfano unatoka Dar kwenda Mbeya, bus ikifika Msamvu Terminal ambapo pana huduma zote hutawaona, ila bus ikitoka Msamvu ikikaribia maeneo ya Mindu ndiyo unawakuta wanawashusha abiria na kuwapotezea muda.
 
Aisee
 
hata hapa tz kuna upuuzi mmoja unakuta mume yuko dsm anamsafirisha mkewe akajifungue kijijini
 
Waje kujibu hapa.
 
Soma vizuri habari, acha kukurupuka lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…