Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchungu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Mkuu it doesn’t matter kikubwa ubinaadam
 
Acha kukurupuka hatujalaumu kuhusu ukamataji.

You are out of point.Check your side
Hamjalaumu kuhusu ukamataji, mmelaumu kuhusu nini ?

Kama unakubali kwamba alivyokamatwa ni sawa hapa tunabishania nini cha zaidi ???
 
Ni wapi Umeitaja KIRUMI kwenye Uzi wako??? Wewe umetaja KURUMLI ambayo ni barrier iliyoko Mbele ya Chuo cha Buhare kuelekea Ginnery Mugango.
Acha kujimwambafai kuwa unajua maeneo na barabara Mkuu, kuna member humu kazi yetu ni kutembea naweza kukutajia barabara ya kuanzia Nangurukulu Mtwara nipite Songea, nitokee Mbeya, Nipite Chunya, Ipole Tabora, Bunda, mpaka, Kibara Mpaka BurendaBufe mpaka Kekombyo naikuta Musoma ambayo unaweza usijue ipo.
Kubali kwamba Mji wako wa Musomo unaingilika kwa Barabara Moja tu hakuna nyingine.
Imebidi nirudi kusoma upya. Wenda alikosema kuandika lakn barrier ya kuingia tarime ni kirumi pale darajani. Samahan kwa hilo.

Kuhusu njia ya kuingilia Musoma sio moja ndio maana nimekwambia labda kama unazungumzia main road na njia fupi ndio ipo moja ila kuna njia nyingine za kuingia musoma sema niza vumbi na mzunguko.
 
I think you are right, the immigration officer did a commendable job. We must have a law and order society.

The unidentified woman with no papers could be a covert agent of the Kagame regime, for all we know. They are known for operating well beyond their borders.

The Tanzanian officials did everything by the book. Thumbs up.
Ukiandika kiingereza ndo unakuwa wa ovyo zaidi.
 
Mkuu acha kutetea Uhalifu. Umewahi kufika japo hapo Zambia tu ukakumbuka na Askari wake wewe raia wa kigeni???
Halafu jaribu kuwa Mkweli, huyo Mama wa Burundi unayesema alikuwa anatokea Ngara kwenda Kenya akamatiwe Barrier ya Kurumli ni Chenga na Uongo. Kumbuka Mji wa Musoma au PENINSULA TOWN umezungukwa na Maji na Njia ya Kuingia ni Barabara 1 pekee yaani Mwanza to Musoma, haipo nyingine, hiyo Barrier unayosema huyo mama alikamatiwa inatokea Vijiji vya Ndani ya Musoma haina Connection na Mkoa ama Wilaya yoyote ndani ya Tanzania sasa hebu fafanua hiyo njia ya Kurumli ina uhusiano gani na Ngarra???
Huyo mama ni Mkimbizi na Mhalifu kama walivyo wahalifu wengine, linapokuja suala la Sheria za Uhamiaji tuweke pembeni huruma na siasa tuache Askari wafanyekazi.

Siwapendi baadhi yao wanapokuwa kazini kwa kujifanya wakali bila kosa kumbe ni mbinu za kuomba rushwa

Lakini katika hii kesi ni tofauti walikuwa wapo kwenye majukumu yao na kulinda amani

Kama alikatisha bila vibali maalumu hilo ni kosa lake ila sio atetewe kwa sababu ni mjamzito

Wajawazito wangapi wanakamatwa wakiwa na madawa ya kulevya?
Huruma iwepo ila sio kuvunja sheria
 
Shida sii kwamba huyo mama kaingiaje nchin, shida ni kitendo cha kumkamata alafu wakamtelekeza hospital baada ya kuona kapata uchungu.
Swali ni je ndivyo kanuni za kuendesha shughuri zao zinawataka waterekeze watuhumiwa ambao wapo kwenye hali hatarashi za kiafya?
Je akipona watarudi tena kumshikilia kama mtuhumiwa baada ya kumtelekeza akiwa kwenye hali mahututi?
Hapo tusiozungumzie swala la kifo maana ajafa.
Kiubinadamu si sahihi.Na hawana fungu la kuhudumia wahamiaji dharura kama hizo labda atoe ya kwake mfukoni
 
Kiubinadamu si sahihi
Sio kiubinadamu tu, pia ata kiusalama sio sahh. Vipi kama alikuwa ni jasusi wa nchi jirani alaf baada ya kumterekeza hospital na yeye anapata mwanya wa kufanikisha adhima yake kwa uhuru zaidi baada ya kupona au ata akiwa hapo hapo hospital?

.Na hawana fungu la kuhudumia wahamiaji dharura kama hizo labda atoe ya kwake mfukoni
Vipi wale waethiopia wanaokamatwa kila siku wakiwa kwenye hali mbali na njaa huwa hawapewi chakula? Na vip gharama za kuwarudisha nchin kwao huwa zinagharamiwa na nan?

Vip kwan haiwezikan akahudumiwa mda wanawasiliana na watu wa ubalozi wa nchi aliyotoka ili wajue wanasaidiaje?
 
Kwanza kabisa namshukuru huyo mama kama kajifungua salama. Mungu amtangulie yeye na mwanae wawe salama. Kama kuna namna ya kumtumia kakitu weka namba za simu au akaunti.

Kuhusu uhamiaji nao sijaona walipokosea. Walikuwa kwenye majukumu yao. Sheria huwa lazima ifuatwe na huruma ndo huwa ni hiari.

Hakuna nchi utaingia bila kuwa na makaratasi. Kwa nchi baadhi ya nchi za jirani huwa kuna border pass kwa wakazi wa sehemu za jirani sana na mpaka. Lakini pia bado zile passport za dharura huwa ni rahisi kuzipata.

Border ya Ngara walifanya makosa kumruhusu bila documents. Watanzania tuamke na kuacha kulalamikia mambo yenye manufaa kwa usalama wa taifa zima.

Uhamiaji wakishirikiana na NIDA waendelee kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu haya mambo. Ikiwezekana waanzie mashuleni huko. Hata TRA nao wapambane kutoa elimu ili kuwa na wananchi wazalendo wanaojua wajibu wao kwa nchi. Itapunguza kulaumiana.

Mwisho kama unajua kipato chako hakiruhusu usitoe papuchi yako ovyo kwa mgeni. Pia wanaume tuache ngono zembe ili kutowaleta viumbe wasio na hatia kuja duniani kuteseka bila sababu.
 
Imekuwa kadhia siku hizi eti nchini kwako ni lazima usafiri ukiwa na nyaraka zinazothibitisha wewe ni raia; tulisimamishwa Chalinze pale na hao makonstebo wakaomba kila mtu atoe kitambulisho cha taifa...ilikuwa fujo kwenye gari wengi hawana ufahamu kwamba ni lazima uwe na utambulisho safarini, sielewi kwanini hawajapeleka elimu kwanza kwenye jamii!!. Pole sana kwa huyo Mama; by birth kijana ni mtanzania sasa 👏😁
Nadhan hlo jambo ni sahihi. Na sehemu ya mafunzo ni hapo kwenye tukio. Wakati mwingine unaweza kumwambia mtu kitu kupitia vyombo vya habari lakininsi wote utaweza kuwapata maana si kila mtu ana hulka ya kuangalia taarifa ya habari.

Hivyo kupitia ugaguzi wa njiani ni jambo linaloweza kukupa imani kuwa kumbe ni muhimu kuwa na kitambulisho. Na pia huwezi jua siku hiyo mnasimamishwa kama kuna mtu alikuwa anatafutwa.

Usalama wa nchi yetu ni jukumu letu raia. Askari wa majeshi yetu wote wanafanya kazi kubwa sana ya kutulinda huku sisis tukiwa tumelala usingizi fofofo. Tuheshimu kazi za watu jamani.

Mwisho, hao askari walipaswa kuwajibika kwa huyo mama kupitia mamlaka zao, maana kama huyo mama angeruhusiwa kienyeji then tukio la kihalisi likafanyika kupitia yeye, lawama zote zingerudi tena kwa hao askari na tena ingeweza kuhatarisha kazi zao.

Lakini pia je, serikali ilipaswa kuwa na fungu la dharura kwa kesi kama hizi. Maana wanafanya majukumu yao kwa sheria lakini wakipata shida wanaachwa wao kuwajibika, kwa mshahara gani?

Tuache lawama jamani. Hao ni binadamu kama sisi tu.
 
Kuna ofisi moja ya uhamiaji wakiwakamata watu wa namna hiyo (wasio raia) huwapiga sana na kuwanyang'anya fedha zao wanazokuwa wamezipata katika kufanya kazi aidha wakiwa wanarudi nchini kwao au wakiwa wameingia nchini kwetu katika utafutaji.
Sasa ninapofanyia kazi ni karibu na ofisi hiyo Sasa wakiwa wanawapiga wanatoa kilio cha uchungu sana utakuta mtu anapigwa zaidi ya masaa matatu roho yangu huwa inaugua sana kwa kusikia vilio vile.
Baada ya kuwapiga huwapora fedha zao na kuwaachia warudi nchini kwao huku hawana nauli wala hela ya chakula, uhamiaji fuateni taratibu zenu za kazi tafadhari
Toa location ya ofisi ya uhamiaji Kuna wadau wanaweza kutoa msaada
 
Zamani nilikuwa nachukia sana wazungu na waasia wavyotubagua, Mara watuite nyani Mara sokwe!

Lakini baadae nilikuja gundua hakuna majitu mabaguzi Kama maafrica, hasa matanzania, eti unamkamata msomali kwenye Lori, anaenda Malawi, kwao anakimbia Vita, we unamfunga jela!! Si usokwe huo?
 
Imekuwa kadhia siku hizi eti nchini kwako ni lazima usafiri ukiwa na nyaraka zinazothibitisha wewe ni raia; tulisimamishwa Chalinze pale na hao makonstebo wakaomba kila mtu atoe kitambulisho cha taifa...ilikuwa fujo kwenye gari wengi hawana ufahamu kwamba ni lazima uwe na utambulisho safarini, sielewi kwanini hawajapeleka elimu kwanza kwenye jamii!!. Pole sana kwa huyo Mama; by birth kijana ni mtanzania sasa [emoji122][emoji16]
Mbaya zaidi mfano unatoka Dar kwenda Mbeya, bus ikifika Msamvu Terminal ambapo pana huduma zote hutawaona, ila bus ikitoka Msamvu ikikaribia maeneo ya Mindu ndiyo unawakuta wanawashusha abiria na kuwapotezea muda.
 
Kuna ofisi moja ya uhamiaji wakiwakamata watu wa namna hiyo (wasio raia) huwapiga sana na kuwanyang'anya fedha zao wanazokuwa wamezipata katika kufanya kazi aidha wakiwa wanarudi nchini kwao au wakiwa wameingia nchini kwetu katika utafutaji.
Sasa ninapofanyia kazi ni karibu na ofisi hiyo Sasa wakiwa wanawapiga wanatoa kilio cha uchungu sana utakuta mtu anapigwa zaidi ya masaa matatu roho yangu huwa inaugua sana kwa kusikia vilio vile.
Baada ya kuwapiga huwapora fedha zao na kuwaachia warudi nchini kwao huku hawana nauli wala hela ya chakula, uhamiaji fuateni taratibu zenu za kazi tafadhari
Aisee
 
hata hapa tz kuna upuuzi mmoja unakuta mume yuko dsm anamsafirisha mkewe akajifungue kijijini
 
Hata Kama huyo Mama ni mtuhumiwa wa kutokua na vibali,bado anabaki chini ya uhamiaji kwa hali yoyote ile kuliko mnamkamata alafu mnamtelekeza bila ya msaada wowote ule kutokana na hali yake ya ujauzito!! Kwa hiyo Sasa uhamiaji ndiyo wamesha maliza kazi yao!?
Waje kujibu hapa.
 
Mkuu usi walaumu kabisa watu wa uhamiaji,hivi wewe ulisha wai kuingia inchi za watu bila utaratibu? Ukiwa kwenye inchi za watu bila kufuata utaratibu lazima utasulubiwa tu,usiwalaumu kabisa wana timiza majukumu yao,pia ni ngumu kumtambua mtu muovu eti kisa kajitetea.
Soma vizuri habari, acha kukurupuka lol
 
Back
Top Bottom