Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Passport ni haki ya kila Mtanzania hata kama hana Safari kwani passport haipatikani bure ni lazima uilipie cash tshs 150,000 , Serikali inaingiza mapato makubwa kupitia passport na endapo wataanza vigezo vya Safari ndiyo iwe kigezo cha kupata passport watambue kuwa watakosa pesa na passport zitarundikana huko Uhamiaji zitakosa wahitaji na Serikali kukosa mapato, watambue kuwa passport ni muhimu kuwa nayo mda wote kwani Safari zingine huja ghafra pasipo kutarajia
 
Hao jamaa wasumbufu sana hata uwe na dhumuni la safari wanasumbua
Passport ni tshs 150,000 bado wanasumbua je? Passport ingekuwa bure si wangekuwa na mashariti magumu kama kuomba Viza USA na UK
 
Kufanikiwa kwa tanzania ni dili au jambo la ajabu,kuna maisha tanzania tunaishi kama zama za mawe.alafu tunashangalia tukisema wakombozi.
Uchumi wa kati wa mlipa kodi ya mwaka shilingi 20k
Tanzania sasa ni Nchi ya vioja matamko ya kusaka uteuzi vyeo sifa za kijinga jinga hayaishi
 
Jipya hapo ni hayo malipo ya Sh. 500,000, huko nyuma hayakuwepo na Passport zilikuwa zinapotea, mengine yote yalikuwepo toka Passport za Tanganyika kwa sababu hiyo ni Hati ya Kusafiria nchi za nje kama husafiri inahitaji ya nini? Labda Wafanyakazi wa Uhamiaji wangekuwa wanaeleza watu wakaelewa maana hata kama mtu ana Passport na nauli ya kwenda Marekani anaweza asiende kwa sababu wakati anapoomba Visa ataulizwa maswali yaleyale anakwenda kufanya nini na hiyo Passport baada ya miaka 10 ni ya kutupwa.
Hata ukienda kukata tiketi ya Safari za nje lazima watakuomba passpor , mipango ya Safari bila passport ni migumu kutekelezeka, hakuna Nchi watakupa Viza bila passport passport
 
Kwanza kipindi hiki cha corona Safari zimepungua sana walipaswa wahimize watu kwenda kuchukua passport kwa wingi mno
 
Huu ujinga wa Uhamiaji ndiyo huchangia wananchi kuzidi kuichukia Serikali ya awamu ya tano
 
Hapana. Kuna wakati unatakiwa kusafiri ghafla na hamna muda wa kuomba na kupata pasi. Mwisho tutaambiwa hupewi leseni ya kuendesha gari kama huna gari.

Amandla...
Kwa utawala huu wa chato lolote linawezekana
 
Wanatengeneza mazingira ya kupokea hongo. Badala ya kulipa Tsh 150,000/ watu wanalipishwa Tsh 300,000 ndio wapate passport.
Jana huko Babati Afisa wa Uhamiaji ameshachukua miezi 3 jela kwa kula rushwa.
 
Utaratibu wa kusumbua watu siyo kwa masilahi ya Taifa kwani Taifa linakosa mapato makubwa sana watu hawatasafiri na pia passport hazitanunuliwa kwani hawatoi bure, kila Nchi ina utaratibu wake lakini utaratibu wa Tanzania ni hatari na wa hovyo ndiyo maana haukubaliki na ni hatari kwa uchumi wa Nchi kwani unaikosesha Serikali mapato makubwa, Serikali ndiyo mlezi wa wananchi lakini ulezi huo wa kuweka mashariti yasiyo na tija kwenye kuomba passport ni Ulezi usiofaa kamwe na ni hatari kwa uchumi
 
WANATENGENEZA MAZINGIRA YA KUPOKEA HONGO. BADALA YA KULIPA TZS 150,000/ WATU WANALIPISHWA TZS 300,000/ NDIO WAPATE PASSPORT.
JANA HUKO BABATI AMESHACHUKUA MIEZI 3 JELA RUSHWA.
Rushwa Uhamiaji ndipo makao makuu hata Takukuru walishanawa mikono hawapawezi kamwe
 
Ujue HUU NI UPUMBAVU.
passport ni haki ya kila raia kuwa nayo.haijalishi una safari au hauna .passport sio mali ya uhamiaji.
Acheni UKOLONI.
Yaani siku nikipata safari ndo nianze kuhangaika kutafuta passport?

Passport ni haki ya kila Mtanzania hata kama hana Safari kwani passport haipatikani bure ni lazima uilipie cash tshs 150,000 , Serikali inaingiza mapato makubwa kupitia passport na endapo wataanza vigezo vya Safari ndiyo iwe kigezo cha kupata passport watambue kuwa watakosa pesa na passport zitarundikana huko Uhamiaji zitakosa wahitaji na Serikali kukosa mapato, watambue kuwa passport ni muhimu kuwa nayo mda wote kwani Safari zingine huja ghafra pasipo kutarajia
Passport za kitanzania bado zatumika vibaya huko nje na watu bado wanazipata kwa magendo na kuzitumia kwenye uhalifu kama usafirishaji wa ngada.

Hivyo hatua ya kwanza ni kudhibiti utoaji wake maana kuna wengine wanazo safari ambazo ni genuine lakini wanaharibiwa na wale wachache wanozitumia vibaya.

Maelezo mengine yametolewa na uhamiaji wenye kuhusu maombi kufanywa bila kuwepo uthibitisho wa safari.

Passport si haki bali ni upendeleo au "privilege" ambapo hutolewa kulingana na uthibitisho wa vigezo vya mwombaji hata kama wailipia.

Pia passport ni mali ya serikali na huweza kuihitaji wakati wowote.
 
Hicho si kigezo cha kuwasumbua watu kupata passport kwani wahalifu wapo kila Nchi na hakuna usumbufu wa kutoa passport kama Tanzania, Watoe passport kwa usumbufu bado wahalifu wapo na hawatakwisha kwani wanazidi kuzaliwa kila siku , Uhamiaji waache visingizio visivyo na mashiko kuwanyima watanzania passport matokeo yake ni kuinyoma Serikali mapato
 
Usumbufu wa kupata passport Tanzania ni usumbufu usio na tija na sasa Uhamiaji wamezidi kuja na usumbufu usio na utadidiza mapato kwenye malipo ya passport.
 
Hicho si kigezo cha kuwasumbua watu kupata passport kwani wahalifu wapo kila Nchi na hakuna usumbufu wa kutoa passport kama Tanzania, Watoe passport kwa usumbufu bado wahalifu wapo na hawatakwisha kwani wanazidi kuzaliwa kila siku , Uhamiaji waache visingizio visivyo na mashiko kuwanyima watanzania passport matokeo yake ni kuinyoma Serikali mapato
Naibu waziri amewaambia uhamiaji waache kusumbua wananchi.

Na wananchi wahakikishe wana vielelezo vyote muhimu- kitambulisho cha taifa, barua ya m/kiti wa serikali ya mtaa, cheti cha kuzaliwa na affidavit ya mmoja wa wazazi.

Hilo la sababu ya safari liondolewe.
 
Ujue HUU NI UPUMBAVU.
passport ni haki ya kila raia kuwa nayo.haijalishi una safari au hauna .passport sio mali ya uhamiaji.
Acheni UKOLONI.
Yaani siku nikipata safari ndo nianze kuhangaika kutafuta passport?
Hapo kwenye Haki,Hakuna Haki isiyofuata utaratibu.
Utaratibu ni huo sio kwamba inaanza sasa miaka yote ipo hivyo.
 
Back
Top Bottom