Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Uhamiaji Tanzania: Bila dhumuni la safari hakuna kupewa pasi ya kusafiria (Passport)

Sasa utaombaje passport kama huna matumizi nayo?

Si unakua na mpango wa safari ndio unatafuta passport!? Au nakosea ndugu zangu😃😃😃😃
Upo sahihi sana.
Unatakiwa uwe na uthibitisho wa huo mpango sasa,
Na siku hizi wanatoa macho kwelikweli hao mabwana.
 
Acha stereotyping mkuu
Wengine tuwasamehe tu kwakuwa hawajitambui.
Sasa mwanamke anaingiaje hapo?
Utaratibu upo hivyo siku zote.
Wengine hawajawahi kufuatilia au pengine ni wale wakuhonga na kupelekewa nyumbani kama yapobao hayo mambo.
 
kwani ukimpa mtu passport akakaa nayo unapungukiwa na nini? Kwani unampa bure?
tanzania pekee ndo tunaona passport NI MALI.nchi nyingi haya mambo hayapo.
Kuna watu hata kusaidiwa mawazo angalau mjitambue kidogo tu inashindikana kwa 'mawazo tupu' kama haya.

Passport ya wapi ndio Mali ya Mtu mfano tuanzie hapo?
Taja tu Nchi nikuumbue.

Mnakariri kwa kukurupuka.
 
Mshangae huyo alielitoa hilo tamko sasa ila utaratibu unalazimisha iwepo sababu ya safari miaka yote sio leo wala jana.
Jiki kitu ndicho kinaitwa kufanya kazi kama robot kwa mazoea ohhh miaka yote sisi huwa tunafanya hivi hivi!!!! AKILI INAKUWA ROBOT NA UTENDAJI KAZI WA KIROBOTI

Ndio maana Raisi anakuwa mkali kila siku kuwa watendaji kazi serikalini wabadilike waache kufanya kazi kwa mazoea
 
Hata mimi namshangaa kwa kweli.
Hicho si kigezo cha kuwasumbua watu kupata passport kwani wahalifu wapo kila Nchi na hakuna usumbufu wa kutoa passport kama Tanzania, Watoe passport kwa usumbufu bado wahalifu wapo na hawatakwisha kwani wanazidi kuzaliwa kila siku , Uhamiaji waache visingizio visivyo na mashiko kuwanyima watanzania passport matokeo yake ni kuinyoma Serikali mapato
 
Najua sana lakini kwanini iwe hivyo?
Kwanini passport ya Tanzania iwe mali kiasi hicho?
Kama dhana ni kupunguza uhalifu wa kuuza madawa ya kulevya mbona tangu zamani mpaka leo madawa ya kulevya yapo tu, yamepungua ?
Hapo kwenye Haki,-Hakuna Haki isiyofuata utaratibu.
Utaratibu ni huo sio kwamba inaanza sasa miaka yote ipo hivyo.
 
Passport ni tshs 150,000 bado wanasumbua je? Passport ingekuwa bure si wangekuwa na mashariti magumu kama kuomba Viza USA na UK
Wakijua una safari ya muhimu au haraka lazima wakusumbue ili utoe posho kidogo
 
Tanzania pekee ndo kuna upumbavu huu.
Picha yangu,hela natoa mimi.utasemaje passport ni yako?
Kuna watu hata kusaidiwa mawazo angalau mjitambue kidogo tu inashindikana kwa 'mawazo tupu' kama haya.

Passport ya wapi ndio Mali ya Mtu mfano tuanzie hapo?
Taja tu Nchi nikuumbue.

Mnakariri kwa kukurupuka.
 
Huu ujinga wa Uhamiaji ndiyo huchangia wananchi kuzidi kuichukia Serikali ya awamu ya tano
Hili naunga mkono.Pia kukomesha rushwa TAKUKURU iingilie kati hili.Wanalifuga ili waendelee kula rushwa.Unaenda wapi lete uthibitisho wa safari ndio sehemu kitengo cha passport hula rushwa,Kikiondolewa Rushwa kitengo cha passport inafunga virago

hapo wa kuambatanisha viambatanisho vya safari na kujieleza unaenda kufanya nini.Hayop maswali ni ya kuulizwa ubalozini mtu ukienda kuomba visa sio na kitengo cha passport!!! Lakini wamejipachika kuhoji hayo maswali ya kibalozi wapige pesa!!!! Kitengo cha passport sio ofisi ya ubalozi inayotoa VISA!!!! UKIENDA UBALOZI HUKO NDIO UNATAKIWA UPAMBANE NA HAYO MASWALI NA MIDOCUMENTS YA KU ATTACH IKIWEMO MITICKET YA NDEGE NK
 
Foji (jiandikie) barua ya kualikwa kutembelea ughaibunj then peleka Uhamiaji wakupe passport.

Hua kuna sharti lingine linaitwa "show money"...yaani ili Uhamiaji waamin utakwenda ng'ambo na utarudi wanataka uwaoneshe fedha za kutosheleza safari. Hapo ndo kazi ilipo
 
Kwanza kipindi hiki cha corona Safari zimepungua sana walipaswa wahimize watu kwenda kuchukua passport kwa wingi mno
Kitengo cha passport ni wahujumu uchumi kifumuliwe chote wawekwe wengine

Passport ni shilingi 150,000 watanzania tuko milioni 60
Wangerahisisha utoaji passport mfano kwa mwaka huu wawe na lengo la kutoa passport hata milioni 2 tu Serikali ingeingiza mapato ya shilingi bilioni 300 watu wawe wanasafiri au la shauri yao serikali ingeweka kibindoni bilioni 300

NI eneo zuri la kupata mapato kuliko hata kukimbizana na machinga kuwataka nao walipe kodi!!!
Tungeweza ondoa vikodi korofi vya machinga na watu wadogo wadogo wanaofikia hadi kuichukia TRA!!

Serikali kama ilivyokuwa ikihamasisha wananchi kupata cheti cha kuzaliwa na kitambulisho cha NIDA wangeanzisha kampeni ya mwananchi pata passport ni haki yako .Lakini sidhani hata wana malengo yeyote ya mwaka kuwa mwaka huu watoe passport ngapi.
 
Cha muhimu kwenye kusafiri ni visa. Kwa hiyo watoe passport kwa kila anaetaka watakusanya kodi nyingi tu.
Asiye na uthibitisho wa safari alipe zaidi kuliko mwenye safari!!
Ku-renew kwa mtu ambae hakusafiri fee iwe zaidi kuliko aliyesafiri!!
Hapo utakuta passport rahisi kupata na watu wasio na safari hawaombi.
 
Dhumuni la safari ni world standard ya passport application, even USA wanatumia the same, hata ukiomba visa lazima ueleze unaenda kufanya nn?
Uongo mtupu vigezo vya kupata passport USA ni hivi hapa

  • Proof of U.S. citizenship (such as a birth or naturalization certificate)
  • Government-issued photo ID (such as a driver's license or military ID)
  • Color passport photo.
  • Fee payment (check or money order)
source WEBSITE ya serikali ya Marekani Getting or Renewing a U.S. Passport | USAGov


Tuje Africa

Vigezo vya kupata passport Kenya hivi hapa

During the Submission you will need the following

  1. An eCitizen pre-filled passport application form and three receipts.
  2. Original birth certificate and photocopy.
  3. Original National ID Card & copy.
  4. Three Current passport size photos.
  5. Recommender’s ID Card copy.
  6. Consent letter for minors.
  7. Old passport for replacement
  8. Parents National ID cards and copy.
  9. Passport fees receipts
Source Tovuti ya serikali ya Kenya eCitizen - Gateway to All Government Services





Rwanda wao vigezo vyao hivi hapa

REQUIREMENTS​


APPLICANTS OF 16 YEARS AND ABOVE​


* Rwandan identity card


* Payment of required application fees

Source website ya serikali ya Rwanda ORDINARY E-PASSPORT

Malawi vigezo vya kupata passport ni hivi hapa tu

Eligibility​


A passport or travel document can only be issued to an applicant who has convinced an Immigration Officer at the counter that he/she is a bonafide citizen of Malawi and that he/she has produced proof of identity as required.

Source website ya serikali ya malawi Passports – Department of Immigration. Republic of Malawi
 
Idara inaongozwa na mwanamke, maamuzi kama hayo siyashangai
Kuongozwa na mwanamke sio swala kabisaaaa kwenye fomu ya maombi kuna sehemu ya dhumuni la safari ambalo unaweza kujaza masomo ,biashara, matibabu etc. sio kitu kigeni kwahiyo Mama Anna Makakala aka single lady mnamuonea kabisaaaa mama wa watu na macho yake yale . point yako imekaa kimfumo dume zaidi.
 
Back
Top Bottom