Katika dhana za kipuuzi ni hii ya kusema kiongozi fulani ndio nguzo ya chama. Matokeo yake ndio haya kiongozi anakaa madarakani zaidi ya miaka 10, hata yale mazuri yake yanaanza kuharibika.
Kwa utafiti wangu niliofanya ambao sio rasmi, kiongozi yoyote wa kuchaguliwa akikaa madarakani zaidi ya miaka 10, ubora wake huanza kupungua na mazuri yake hufifia. Mfano wa viongozi hao ni
- Nyerere
- Moi
- Mugabe
- Gadaffi
- Paul Biya
- Museveni
- Albashir
- Saddam Hussein
Kiongozi kama Mandela amebaki bora na kuwa kiongozi mzuri kwani hakukaa madarakani mrefu. Mbowe alipaswa kukaa pembeni baada ya blunder ya Lowassa, au kama hakuona sawa kuachia baada ya kosa lile, basi hakupaswa tena kugombea uwenyekiti wa CDM uchaguzi uliopita. Mbowe alishafanya vizuri miaka yake 10 ya kwanza, alipoanza kukaa zaidi ya miaka 10, ndio anafikia huku ambapo anakosa ufanisi, na kuishia kuingia kwenye miafaka sijui maridhiano ya kihuni.