Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Tindo !
Halafu tukiwaambia UKWELI mnaishia kututukana matusi mazito humu.
Chadema kama chama bado kinaendeshwa kiuanaharakati zaidi badala ya taasisi.
Mambo mengi makubwa bado maamuzi yake yameachwa kwa mtu mmoja tu.
Huko huko kuna wanachama ambao wao wanajiona kama Superior quality na wengine kuonekana kama wafuasi fuata upepo.
Kuna watu kama Lema na Lissu ambao pia sio watiifu kwa wanachama wenzao kwa kujiona kuwa wajuaji wa kila jambo zaidi hata ya viongozi wenzao wengine ndani ya chama.
Kuyaona madhaifu ya chadema sio lazima niwe mwanachama,bali kila mtanzania ana macho na ufahamu wake,jinsi ya kuchanganua mambo mbalimbali yanayojiri ndani ya mipaka ya nchi yetu,katika nyanja mbalimbali ikiwemo hii ya kisiasa.
Umeathirika na neno kutukanwa, ndio maana unalitumia kama fashion! Haya mapungufu unayoyasema dhidi ya CDM, ungekuwa sahihi zaidi kama ungekuwa umefanikiwa kuyamaliza ndani ya CCM.
Ni kweli CDM ina mapungufu kama yalivyo mapungufu ya taasisi nyingine, lakini ccm ina mapungufu mengi zaidi ya CDM. Mbeleko ya vyombo vya dola, ndio pekee uhakika wa CCM kuendelea kuwepo.