Uharaka unahitajika kwenye maamuzi ya CHADEMA

Heading ya mleta mada nakubaliana nayo, lakini content zilizobeba maudhui ya title sikubaliani nazo 100%

- Suala la kuteuliwa Katibu Mkuu, Dr. Mashinji.

Hapa nakubaliana na Chadema kuchukua muda mrefu kabla hawajampata mtu waliyeamini alitakiwa kuja kuvaa viatu vya Dr. Slaa, au ikiwezekana avuke viwango.

Kwangu ilikuwa fair kwa Chadema kuchukua muda mrefu kufanya uchunguzi, na ndipo wakaibuka na jina la Mashinji, ambalo kimsingi kulingana na vyeti vyake alionekana yupo vizuri, lakini bahati mbaya kwenye utendaji akawa mbovu, kwangu hili sio kosa la Chadema, naamini hii ndio sababu iliyowafanya sasa kumchukua kijana wao wa ndani na kumpa hilo jukumu.

- Suala la maamuzi ya baraza kuu kuchukua muda mrefu [zaidi ya mwaka] kabla ya kuwafukuza kina Mdee na wenzake.

Ikumbukwe, wakati ule palikuwepo na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, mikusanyiko mingi ilizuiliwa, hivyo Chadema wasingeweza kukutana kwa wakati ule na kwenda kinyume na maelekezo ya Wizara ya Afya.

- Kuziba nafasi ya Mwenyekiti Bawacha.

Hapa nakubaliana nawe, sijui ni nini kinachochelewesha kuchukuliwa huo uamuzi, japo nakumbuka kuna uchaguzi ulifanyika ukampa cheo Catherine Ruge, sasa kama ule uchaguzi ndio ulimteua mtu wa kukaimu nafasi ya Mwemyekiti Bawacha, huo kwangu ni udhaifu wa chama.

Binafsi ningekuelewa vizuri zaidi kama ungezungumzia Chadema kuchelewa kuzungumzia issue kama tozo, ripoti za CAG, malalamiko ya kufelishwa wanafunzi Law School nk.

Vyema wajue, wanatakiwa kuzungumzia jambo likiwa bado lina trend, wasingoje mpaka lipoe.
 
Ulichokiandika hapo juu ni mfano wa mawazo mgando, sio tu kwasababu fulani na fulani walikosea after 10 yrs ndio unaishia hapo, unatakiwa uende mbele zaidi ya hapo.

Ndani ya hiyo miaka 10 unayoitaka utakuwa umefanya kile viongozi walichotaka ukifanye ili kufikia malengo ya chama mliyojiwekea? au utakuwa umekaa pembeni tu unawahesabia miaka 10 ili ikifika waondoke?

Kama ni kukaa tu na kuwahesabia miaka 10 ikifika waondoke, huu ndio ubinafsi wenyewe, na utaendelea kuwahesabia wote hii miaka, wakati mabadiliko ya kweli yanayohitaji ushirikishwaji wa wanachama na wapenzi yakiwa hayajafikiwa, na hayatafikiwa kama akili zipo kwenye kubadilisha sura viongozi tu.
 
Mbowe alikuwa na umuhimu wake katika chama kwa wakati maalum. Sasa nyakati ni tofauti, hawezi kuendelea kuwa na umuhimu ule ule katika nyakati mbalimbali.
Kwako ni mazingira yapi ya kisiasa yaliyobadilika yanayomfanya Mbowe asifae kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM?

Nina wasiwasi wengi wenu mmeichoka sura ya Mbowe, lakini kwakuwa hamuwezi kusema wazi, basi mnatafuta sababu zisizo na mashiko ili kutimiza malengo yenu.

Nawashangaa, iweje kama tatizo la Chadema ni kusuasua kutoa taarifa kwa wakati, badala ya kusema Mbowe abadilishe wasaidizi wake, nyie mnamtaka aondoke, kwani huyo mwenyekiti mpya atakayekuja na wasaidizi wasiokosea mtaotoa sayari ipi? naona nae after some days mtamtaka aondoke!.

NB.
Haya ni mawazo huru, simpigii debe Mbowe wala mwingine yeyote awaye.
 

Ingekuwa taasisi zetu zinaongozwa zaidi na katiba zetu hapo kubadili sura ya kiongozi isingekuwa lazima, lakini inapokuwa taasisi inaongozwa sehemu kuwa na utashi wa kiongozi, basi kubadili sura ni jambo lisiloepukika.

Tuchukulie kubadili sura sio jambo la msingi, lakini unapokaa miaka 15+ huku kukiwa na makosa ambayo huko awali hayakuwepo, ni kwanini hiyo sura isibadilike ili kupatikana mtazamo mpya? Hebu jaribu kuingia uone kama hata tovuti siku hizi inafunguka, sasa jambo dogo hivyo limekwama, hayo mengine makubwa inakuwaje?
 
Kwanini taasisi zisiongozwe na katiba wakati ndio iliyopo na msajili wa vyama aliipitisha? unataka kusema huyu msajili wa vyama wa CCM anaipendelea Chadema kwa kwenda kinyume na Katiba yake?

Hebu tuwekee hapa mifano inayoonesha vile Chadema inavyokwenda kinyume na Katiba yake.

Suala la makosa madogo au makubwa tumeimbiwa binadamu, na kukosea hakuchagui miaka, hapa sema tu umeichoka sura ya Mbowe, kwasababu zako ulizojiwekea siku zote kiongozi akifika miaka 10 anakuwa amechoka, japo unakuwa huna uthibitisho wa kueleweka.
 

Nimeweka mifano halisi ya viongozi waliokaa madarakani zaidi ya miaka 10, na ubora wao ukapungua. Huyo Mbowe nimemuweka kwenye kundi hilo maana ufanisi wake kwa sasa umepungua.

Kwahiyo kutaka kiongozi abadilike ndani ya miaka 10 ni ubinafsi, lakini akikaa zaidi ya muda sio mbinafsi?! Sina tatizo na unachoamini, lakini kwangu kwa sasa Mbowe ni sahihi kupisha nafasi hiyo apewe mwingine. Labda kama CDM hakuna succession plan ya kueleweka.
 

Imebidi nicheke tu, mengine hata sio ya kuongelea hapa maana hata ni aibu boss.
 
Binafsi siwezi kuwa mwana CCM hata ikibidi kufa nachukia dhuruma
 
Na. 3 ndiyo inashangaza zaidi au pengine katibu mkuu na mwenyekiti wanajua wazi wanawaonea wale wadada. wale wadada hawana kosa lolote na hivyo walijua watakwenda mahakamani na mahakama itapindua kisha watawarudisha kundini na nyadhfa zao kwa kigezo cha kutii mahakama
 
Unamuita vipi Mbowe mbinafsi wakati anawekwa kwa kupigiwa kura na wanachama wa chama chake? naona hutaki agombee ili uridhishe nafsi yako, vipi wale wanaomtaka agombee? ubinafsi

Kitendo chako cha kumuweka Mbowe kundi moja na wakina Saddam Hussein na Gaddafi unaonesha vile hukielewi kabisa kile unachopigania.

Wewe ndie mbinafsi usiyetaka Mbowe anayechaguliwa na wanachama aendelee kukiongoza chama chao, unalazimisha kutaka mawazo yako ndio yafuatwe na wengine, dikteta mdogo.
 
Upo sahihi sana

Baraza Kuu la Chama 2019 liliazimia zifanyike Chaguzi za Mabaraza za Kanda. Lakini mpaka leo hazijafanyika Mnyika amepwaya sana. Ni Kiongozi mzuri lakini sio mtendaji kabisa. In short hafai kabisa kuwa Katibu Mkuu

Hata BAVICHA baada ya Nusrat kuondoka wameshindwa kufanya Uchaguzi kwa mujibu wa Katiba tokea 2020 baada ya usaliti wa Nusrat mpk Leo nafasi inakaimiwa na Naibu Katibu Mkuu BAVICHA.

Sisi tunaokipenda Chama ndio tunaumia. Ukienda pale Ofisini Makao Makuu ya Chama sasa hivi hakuna mtu na wakati hiki ndio Chama pekee kilichobeba matumani ya watanzania lakini kila mmoja afanye survey aende Makao Makuu ya CHADEMA siku za kazi halafu atakuwa walinzi wawili labda na Afisa mmoja.

Haya mambo yanasikitisha sana
 
Tindo !
Halafu tukiwaambia UKWELI mnaishia kututukana matusi mazito humu.

Chadema kama chama bado kinaendeshwa kiuanaharakati zaidi badala ya taasisi.

Mambo mengi makubwa bado maamuzi yake yameachwa kwa mtu mmoja tu.

Huko huko kuna wanachama ambao wao wanajiona kama Superior quality na wengine kuonekana kama wafuasi fuata upepo.

Kuna watu kama Lema na Lissu ambao pia sio watiifu kwa wanachama wenzao kwa kujiona kuwa wajuaji wa kila jambo zaidi hata ya viongozi wenzao wengine ndani ya chama.

Kuyaona madhaifu ya chadema sio lazima niwe mwanachama,bali kila mtanzania ana macho na ufahamu wake,jinsi ya kuchanganua mambo mbalimbali yanayojiri ndani ya mipaka ya nchi yetu,katika nyanja mbalimbali ikiwemo hii ya kisiasa.
 
Nafurahi kuwa Chama kikuu Cha upinzani KINAJIKOSOA na KUJISAHIHISHA peupe.

Jambo hili linajenga chama na kuleta balance.

Nashauri atafutwe mbadala wa mkt wa BAVICHA Taifa, Pambalu amepwaya.

Nafasi yake angepewa ndugu MWITA Kutoka musoma, anaweza uharakati.

Kuhusu Mbowe kama mwongoza Dira ya chama akae mpaka mwisho wa uhai wake kama Nyerere.

Ameeeen.
 
Hakuna aliyekukataza, lakini usione nongwa unapoambiwa uanaposimamia hapafai.

Sijawahi kuwa na tatizo na unachoamini, hivyo sikuzuii kutoa maoni yako dhidi ya ninachokiamini.
 
Afisa habari aliyekua anajitambua ni Kafulila na baadae Mnyika, baada ya hapo kitengo kikamfia Makene. Yaani hata kampeni za Lissu kupata feedback ilikua inachukua masaa 6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…