Uharaka unahitajika kwenye maamuzi ya CHADEMA


Umeathirika na neno kutukanwa, ndio maana unalitumia kama fashion! Haya mapungufu unayoyasema dhidi ya CDM, ungekuwa sahihi zaidi kama ungekuwa umefanikiwa kuyamaliza ndani ya CCM.

Ni kweli CDM ina mapungufu kama yalivyo mapungufu ya taasisi nyingine, lakini ccm ina mapungufu mengi zaidi ya CDM. Mbeleko ya vyombo vya dola, ndio pekee uhakika wa CCM kuendelea kuwepo.
 
Aisee unaweza dadavua Hilo tatizo mkuu
 

Boss iko hivi, kwa huku Afrika, kiongozi au chama kikikaa madarakani zaidi ya miaka 10 mfululizo, chaguzi nyingine zinazofuatia hutawaliwa na vitimbi, uhuni, ulaghai na ujanja ujanja ili kubaki madarakani. Ushahidi wa haya upo bayana. Inshort chaguzi chini ya mazingira hayo huwa ni kufuata formalities tu na sio zaidi ya hapo.

Tofauti ya Mbowe na hao akina Gaddafi ni kutokuwa na dola tu, lakini sioni tofauti yoyote nje ya hao.

Mbowe anaweza kukaa madarakani hata miaka 100 hapo CDM kwa kuchaguliwa na wanachama kama usemavyo, lakini usitegemee ubora tena toka kwake. Hiki ndio ninachoamini, hivyo utanisemehe kutokuwa upande unaoamini, na ninaheshimu unachoamini pia.
 
Hapana si kweli, Ile combination ilikua kifo cha CCM kilichowaokoa ni tume tu ila sidhani kama Dr Slaa angeleta challenge kubwa kiasi kile.
CCM ingeondoka sawa, lakini mwananchi wa kawaida angenufaika vipi na utawala wa lowasa?

Utawala wa lowasa ungekuwa mbovu zaidi ya ule wa kikwete kwa mbali sana (kiuhalisia ingekuwa ni ccm inatawala kwa jina la chadema ukizingatia timu ya wasakatonge aliyokuja nayo).

Kenya walifanikiwa kuiondoa KANU, lakini wanaotawala leo ni haohao KANU, sera zilezile, tofauti majina tu.

Kilio cha wapinzani Kenya kimebaki kilekile tangu Moi akiwa madarakani.
 
Momentum of Lowasa ndio iliwapa wabunge wengi hadi wahuni kama Lijualikali nao wakapata ubunge kirahisi tu.

Sijui huwa mnatumiaga vigezo gani kujuwa mchango wa mtu ni nini?

Sio kweli kuwa Lowassa ndio aliwapa cdm viti vya ubunge ama udiwani. Lowassa ni sawa na mtu aliyekuta chakula mezani akaishia kugawa mapaja ya kuku na vidari, lakini hakuwa mpishi wa chochote. Kama Lowassa alileta ushindi ule akiwa na miezi miwili, alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili?

Ifahamike baada ya uchaguzi wa 2010-2015, CDM ndio chama cha siasa kilichofanya kazi ya kisiasa kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo CCM. Ndio chama kilichotembea nchi nzima na kufanya mikutano mingi kuliko chama chochote. Wakati hayo yote yakifanyika Lowassa hakuwepo, iweje yeye ndio alete ushindi ule? Angeenda TLP, UDP nk na kupata ushindi kama ule hapa ungekuwa na hoja. Jitahidi kuepuka upotoshaji unaofanywa na CCM. Na. Kwa taarifa yako, kama kuna kosa kubwa CDM walifanya ni kumpokea Lowassa, kisha wakampa nafasi kubwa kabisa ya kugombea urais. Lowassa ndio aliua siasa na brand ya CDM. Hiyo ni mada ya siku nyingine.
 
Naheshimu maoni yako lakini hujui ukweli na huzijui vizuri siasa au yawezekana nyinyi ni wale wafuasi wa moyoni wa Dr Slaa ndio wana imani kama hizi.

Pamoja na wizi wote uliofanyika mwaka 2015 kama siyo system kuivunja Ukawa na kumnyofowa Dr Slaa na Ibrahim Lipumba Ccm ilikuwa imeshaelekezwa kibra inachinjwa.

Walichokuwa wanahitaji watu ni kuiondowa kwanza Ccm ibaki historian tu kama KANU.
 
Kwa taarifa yako, kama kuna kosa kubwa CDM walifanya ni kumpokea Lowassa, kisha wakampa nafasi kubwa kabisa ya kugombea urais. Lowassa ndio aliua siasa na brand ya CDM. Hiyo ni mada ya siku nyingine.
Huo ndio ukweli ambao viongozi wanaufumbia macho, lakini ndani ya nafsi zao hata wao wanaufahamu.

1995 Mrema alikuwa na nguvu kubwa kisiasa. Alipoondoka ccm, chadema walifanya naye mazungumzo ili aungane nao. Waliachana naye akaenda nccr alipotoa sharti la kuwa mgombea wao wa urais.

Hawa kina Mtei walikuwa viongozi waliolenga mafanikio makubwa ambayo hayanyeshi kama mvua. Yanachukua muda. Mrema kweli angewasaidia kupata mafanikio fulani, lakini walijua yatakuwa short-lived kama ilivyokuwa kwa nccr.

Mbowe 2015 alijua urais kwa mazingira yaliyokuwepo wasingeshinda. Lakini akajua kwa mahesabu ya idadi ya wabunge watakaopatikana, ruzuku isingekuwa haba.
 

Honestly katika vitu ambavyo sikuwaelewa CDM ni kumpokea Lowassa na kumpa nafasi adhimu ya kugombea urais. Ifahamike Lowassa hakuwa na itikadi wala mapenzi na CDM, bali aliutaka uraisi tu. Na ndio maana alivyokosa urais akawa useless kwa cdm.

Kibaya zaidi Lowassa akaondoa brand ya CDM, ambayo wanaccm huita siasa za kiharakati. Matokeo yake CDM ikaachana na aina ya siasa ilizoipandisha ikaiga siasa za CCM, ambazo wala haziibebi CCM kwani hata yenyewe inategemea zaidi vyombo vya dola kubakia hai kisiasa. Aina ya siasa za CDM ni hizo afanyazo Tundu Lisu, ndio maana wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2020 CDM ilirejesha vibe laki hadi kupelekea Magufuli kuagiza uchaguzi unajisiwe.
 

Mkuu huenda ww ni SI unit ya kuijua siasa, hivyo yoyote aliye nje ya unachoamini huyo haijui siasa. Ni kweli mimi nilimkubali Slaa kwa aina ya siasa alizofanya na vibe aliloleta. Sikukubaliana na kuzira kwake baada ya Lowassa kupokelewa kimokosa na CDM, japo niliheshimu maamuzi yake.

Kuitoa CCM ilikuwa na hadi leo ni lengo letu wananchi, na hasa sisi waumini wa siasa mbadala za CCM. Lakini kuitoa CCM kwa karata ya kumtumia Lowassa haikuwa mbinu sahihi, maana hatari ya kupoteza vyote iwapo asingepata uraisi ilikuwa na madhara ya muda mrefu. Matokeo yake Lowassa hakuwa rais, na kwa bahati mbaya akapandikiza siasa za kikondoo ndani ya CDM, huku CDM ikipoteza hata taswira yake ya chama kinachopambana na wezi.

Bado CDM ilikuwa na uwezo wa kupata urais bila kumtegemea Lowassa, achia mbali wabunge na madiwani ambao ni dhahiri ingewapata bila uwepo wa Lowassa. Kubwa kuliko yote CDM bado ingebaki na taswira yake ya kupambana na wezi, jambo ambalo lingeendelea kuibeba CDM kwa muda mrefu. Leo hivi vyote havipo, sio urais au haiba ya kupambana na ufisadi, kisa Lowassa. Je unajua ni kwa kiasi gani haiba ya CDM imeipotea kwa kumpokea Lowassa ambaye hakuendelea kuwa msaada baada ya kuukosa uraisi?

Ifahamike Lowassa aliutaka urais sio kwa ajili ya mageuzi kama CDM tulivyotaka, bali yeye aliutaka kama yeye, na wala CDM kama chama wasingeweza kumdhibiti Lowassa iwapo angekuwa rais. Kama tu aliweza kukaa high table akiwa hana cheo chochote cha kikatiba ndani ya chama ndio wangeweza kumdhibiti akiwa rais kwa katiba hii mbovu? Pale ndio Nilimdharau Mbowe na genge lake.
 
Bwana Zitto utakuwa una usahaulifu tu, sisi CHADEMA kwa taarifa yako tunaongoza kwa maamuzi ya haraka na magumu ...
Rejea tulovyomfukuza Zito na kundi lake na kubwa kuliko ni tulivyomkaribisha Lowasa.
 
Rejea tulovyomfukuza Zito na kundi lake na kubwa kuliko ni tulivyomkaribisha Lowasa.
Zitto ni binadamu, kama binadamu wengine naye anao udhaifu wake. Lakini hakuna anayeweza kuufuta mchango wa Ztto katika kuijenga chadema hasa kwenye kundi la vijana.

Ni bahati mbaya sana kuwa alikuja kusukiwa zengwe lililoratibiwa na kundi lililokuwa na Mrema nccr na baadaye tlp wakati Zitto akihangaika kuijenga chadema.

Baadhi ya wasuka zengwe kama kubenea, komu... washatafunwa na karma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…