Uhasama wa kisiasa, kugawanyika na kusambaratika kwa CHADEMA kutaimarisha vyama vingine vya siasa nchini

uoga wako na kujitenga kwako kushiriki mambo ya siasa ndiyo umaskini wako gentleman πŸ’
 
kati ya mahasimu wa kisiasa wanaolumbana kwasabb ya uenyekiti wa Chadema Taifa nani pilipili na nani tomato kwa mfano?

Kama mtaalamu mbobevu wa masula ya siasa na demokrasia, Lazima niwafafanulie wadau mambo hayo bila choyo.

ukileta mihemko na makasiriko yako humu, binafsi sihusiki nayo ni muhimu ukatafuta suluhisho la kibinafsi πŸ’
 
🀣 🀣 🀣
 
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema: 'Binadamu angekuwa,hana tumbo angekuwa mtu mzuri'.

Kiini hasa cha ugomvi sio siasa ni maslahi binafsi ya kiuchumi hasa upigaji kupitia shughuli za CHADEMA. Kundi la Lissu ambalo limeungana na wanaharakati, diaspora wana mikakati yao ya upigaji wa hela za wafadhili kupitia programs kadhaa kwa kupitishia CHADEMA,; kabla ya hili la uchaguzi ilikuwepo mipango ya mapinduzi kama tulivyosikia wakati Mbowe akiwa jela.

Hivyo mgogoro huu ulikuwa unafukuta chinichini huku kwa nje wakionekana kama wamoja. Kama isingekuwa njama za kumpindua Mbowe pengine uchaguzi huu Mbowe asingegombea ila baada ya kuona chama kinatekwa nyara na watu wasio CHADEMA kinda Kindiki ndipo Mbowe akaona aendelee na uenyekiti ili kukilinda chama.

Uhosama wa Lissu na Wenje ndio uliochochea hii Vita ya sasa tunayoiona ambayo ni ya kufa na kupona maana atakayeshinda ndio itakuwa nwisho wa aliyeshindwa. Wenje alimtonya Mbowe hizo njama za mapinduzi ambapo awali naye alishirikishwa.


Kiuhalisia hakuna kiongozi wa chama chochote cha siasa hapa nchini hata CCM ambaye amefanikiwa kukijenga chama kama Mbowe lakini hata hilo Lissu, Lema, Diaspora na wanaharakati na wafuasi wao wanajidai hawalioni. Sio bure ni tamaa ya pesa imewafanya wawe vipofu.

Jiulize hivi hao watu wenye uelewa ( wanaharakati; Diaspora na wasomi ( ukiondoa hawa mashabiki wa grassroot ambao ni mbumbumbu) hawaelewi kuwa Tanzania CCM haitaki na haitaruhusu reforms za Tume ya uchaguzi na sheria zake kwa sababu ni kitanzi kwao? Hawaelewi kuwa CCM wanajua fika kuwa wananchi wa nchi hii wamelala usingizi, hawajali na ni waoga hivyo hawawezi kuleta shinikizo lolote litakalofanya CCM wakubali mabadiliko? Hawajui kuwa mwanasiasa wa nchi hii hata awe nani hata akitoka CCM hana watu wa kumsaidia kuweka shinikizo tofauti na nchi zingine kama Kenya, Afrika kusini nk? Katika mazingira hayo Lissu akichaguliwa ataweza kufanya nini ikiwa hana back up ya watu wanaoweza kuingia barabarani? Tena bora Mbowe ambaye anaweza kushawishi CCN wakalegeza japo kidogo hivyo wakapata wabunge na madiwani..

Ni wazi Lissu na timu yake wanajua hili ila kwa sababu lengo ni upigaji ndio maana wanatumia mbinu chafu za kumchafua Mbowe ili wateke nyara chama.

Lema anahoji kwa nini Mbowe aliwakaribisha Halima Mdee na wenzake katika party yake huko kwao nyumbani lakini Lema huyo huyo hajiulizi mbona yeye aliwekwa jela na Gambo muda mrefu akateseka na mateso yale ya jela, wababe wa jela hatujui kama hata walijaribu kummendea, lakini baada ya kutoka amekuwa akizungumza na Gambo na kupanga mambo ya kisiasa , kuna wakati Gambo alitoa siri kuwa Lema alimuomba amuunganishe aongee na Rais , lakin Lema anamkosoa Mbowe kumualika Mdee!.

CHADEMA haitakufa ila itayumba kidogo, na hakutakuwa na impact sana katika nchi hii kwa sababu CCM itaendelea kutawala kwa miaka mingi ijayo hata kama kusingekuwa na mgogoro CHADEMA.
 
uoga wako na kujitenga kwako kushiriki mambo ya siasa ndiyo umaskini wako gentleman πŸ’
Kama unawashabikia wanaoiba na kujilimbikizia matrilioni kwa rasilimali zetu, na unawatukana wanaokemea wizi huo na unataka wafe, Tanganyika yetu itapata wapi msaada.
 
Kama unawashabikia wanaoiba na kujilimbikizia matrilioni kwa rasilimali zetu, na unawatukana wanaokemea wizi huo na unataka wafe, Tanganyika yetu itapata wapi msaada.
unaweza kua na matrilioni ukifanya kazi kwa bidii na uaminifu hata kwa kilimo tu,
na ukaondokana na dhana ya wizi au kuibiwa mambo ambayo huna ispokua uvivu wako tu unakusumbua.

vaa ujasiri, uthubutu na bidii ili uweze kujitegemea kiuchumi na kuondokana na kutegemea masaada unaodai
 
Rasilimali zetu, zinaibiwa na Viongozi mnawashabikia. Hapo ndio mgogoro ulipo. Binafsi sihitaji msaada wa mtu. Nchi yoyote ambayo watu hawana uchungu na mali za nchi hutaona lolote la maana.
 
Rasilimali zetu, zinaibiwa na Viongozi mnawashabikia. Hapo ndio mgogoro ulipo. Binafsi sihitaji msaada wa mtu. Nchi yoyote ambayo watu hawana uchungu na mali za nchi hutaona lolote la maana.
uanaibiwaje kama sio uvivu na kung"aa macho kwako kizembe gentleman?

mgogoro uanao pekeyako gentleman huenda na familia yako tu.
Tanzania hakuna mgogoro wowote miongoni mwa waTanzania, labada hapo chadema ndiyo kuna vita ya maneno na tamaa ya madaraka ya uongozi wa chama.

waTanzania wazalendo wenye nia na dhamira ya kulinda na kugawanya rasilimali za nchi kwa usawa, haki na uwazi ni viongozi wa chama na serikali sikivu ya ccm pekee
 
Wakati nakata ya CCM ulikuwa hujazaliwa. Yanayofanyika nchi hii na rasilimali zinavyoibiwa unajua. Mfumo wa kulinda rasilimali sio kukaa barabarani. Ni hoja na demokrasia huru, ukweli na uwazi ambayo mnaipiga vita.
 
Wakati nakata ya CCM ulikuwa hujazaliwa. Yanayofanyika nchi hii na rasilimali zinavyoibiwa unajua. Mfumo wa kulinda rasilimali sio kukaa barabarani. Ni hoja na demokrasia huru, ukweli na uwazi ambayo mnaipiga vita.
kuibiwa saa zingine ni uzembe tu gentleman,

Lakini pia kuishi kwingi kwa malalamiko ni mzigo. Tanzania ni tulivu na kwakweli nchi yetu mambo yanafanyika kwa uhuru, haki na uwazi, ila wavivu wachache hawaoni hayo.

Demokrasia ya Tanzania ni imara na ina imarika siku hadi siku, na rasilimali za nchi zinagawanywa kwa wote na kwa maslahi mapana ya waTanzania wote πŸ’
 
Hili ni jukwaa huru. Unaweza kusema lolote, kusifu, kuongopa, kushangilia, kuabudu, mradi ufurahishe moyo wako mkuu.
 
Hivyo vingine vikiimarika kama chadema mtateka kuuwa na kubambikia kesi wapenzi wao? Au vyenyewe mtavikabidhi dola kibwerere?
 
Hili ni jukwaa huru. Unaweza kusema lolote, kusifu, kuongopa, kushangilia, kuabudu, mradi ufurahishe moyo wako mkuu.
muhimu zaidi kuambiana ukweli gentleman,

uvivu humfanyia mtu kulalamika maisha yake yote πŸ’
 
Yaani vyama vingine ni dhaifu kwakuwa cdm ni imara, na hakuna uwezekani wa vyama hivyo ikiwemo chama la majizi kuwa imara hadi cdm isambaratike?!
 
Yaanu vyama vingine ni dhaifu kwakuwa cdm ni imara, na hakuna uwezekani wa vyama hivyo ikiwemo chama la majizi kuwa imara hadi cdm isambaratike?!
kwakweli chadema ina umoja sana hadi mipasho wanapashana wao kwa wao tu, hakuna mpasuko 🀣
 
kwakweli chadema ina umoja sana hadi mipasho wanapashana wao kwa wao tu, hakuna mpasuko 🀣
Demokrasia iliyopo cdm ya kufunguka ingekuwepo ccm, leo hii wangekuwa wameshalishana sumu karibia wote.
 
Demokrasia iliyopo cdm ya kufunguka ingekuwepo ccm, leo hii wangekuwa wameshalishana sumu karibia wote.
mipasho ndiyo mnaita demokrasia sio chadema?🀣

hawa viongozi wenu si walisema hawajagawanyika lakini pia na hawana matatizo moyoni na unafiki usoni?🀣
 
CUF nayo Chali.
ACT Kwa sababu wapo wahafidhina wa Zanzibar
CHADEMA nayo ndio inakoelekea
 
mipasho ndiyo mnaita demokrasia sio chadema?🀣

hawa viongozi wenu si walisema hawajagawanyika lakini pia na hawana matatizo moyoni na unafiki usoni?🀣
Kugawanyika kwa maana ya kiccm ni kuongea ukweli hadharani. Huko ccm kufumbia macho wizi ndio uimara wa chama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…