Ni wazi matokeo yoyote ya ushindani, minyukano na uhasama wa kisiasa baina ya viongozi wanao gombea nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa, kutaidhoofisha chadema yenyewe na kuimarisha vyama vingine vya siasa nchini, ikiwa ni pamoja na chama tawala.
Hakuna atakaeshinda uongozi wa chadema Taifa, atafanikiwa kuongoza chama hicho kwa amani, ispokua kwa hujuma za makusudi za mara kwa mara, hususani kutoka kwa masalia ya viongozi na wafuasi wa mgombea uongozi alieshndwa katika uchuguzi huo kama kisasi.
Ndiyo maana kila mgombea hususani baina ya mafahali wawili wa nafasi ya uenyekiti anadai kwamba, asiposhinda uchaguzi huo chadema huenda chadema ikafa. Ni wazi hakuna utashi wa kisiasa baina yao, hakuna mwenye nia wala dhamira njema na chadema.
Aina ya vita ya maneno wanayopigana wagombea uenyekiti wa Chadema Taifa, inajenga uhasama na kuibua vidonda na majeraha yasiyosameheka baina yao na hivyo kuzidisha na kuchochea chuki ya kudumu ambayo inaweza kusababisha hatari zaidi, uharibifu na pengine hata maafa ya kisiasa.
Kutuhumiana kunakoendelea bila ushahidi kupitia mahojiano kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi baina ya wagombea kunaelekea kubaya zaidi hadi kugusa maisha binafsi na ya kifamilia ya wagombea hao, na hii ni hatari zaidi.
Vita hii haiwezi kuisha salama, na ikitokea basi itakua ni kwa unafiki wa kiwango cha juu sana, kama ambavyo mara zote wagombea uongozi hao wa chadema Taifa hutabasamiana kinafiki huku mioyoni mwao pakiwa na chuki binafsi ambayo sasa ndiyo wanaielezea kwa umma kwa maneno.
Kwa majeraha mabaya sana wanayo endalea kujeruhiana wagombea uongozi wa chadema ngazi ya Taifa, hayupo miongoni mwao atakae fanikiwa kuiongoza Chadema kwa amani na utulivu, kwasababu huyo mwingine atakua akihujumu jitihada za mwingine kama kisasi, na hiyo inaweza kua fursa na nafasi kwa vyama vingine vya siasa, kuvuna wafuasi wa chadema watakao kua wamechoshwa na vurumai na songombingo za Chadema na uongozi wake.
Una maoni gani kama mdau wa siasa za ndani ya chama kinachojiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo?🐒
Mungu Ibariki Tanzania
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema: 'Binadamu angekuwa,hana tumbo angekuwa mtu mzuri'.
Kiini hasa cha ugomvi sio siasa ni maslahi binafsi ya kiuchumi hasa upigaji kupitia shughuli za CHADEMA. Kundi la Lissu ambalo limeungana na wanaharakati, diaspora wana mikakati yao ya upigaji wa hela za wafadhili kupitia programs kadhaa kwa kupitishia CHADEMA,; kabla ya hili la uchaguzi ilikuwepo mipango ya mapinduzi kama tulivyosikia wakati Mbowe akiwa jela.
Hivyo mgogoro huu ulikuwa unafukuta chinichini huku kwa nje wakionekana kama wamoja. Kama isingekuwa njama za kumpindua Mbowe pengine uchaguzi huu Mbowe asingegombea ila baada ya kuona chama kinatekwa nyara na watu wasio CHADEMA kinda Kindiki ndipo Mbowe akaona aendelee na uenyekiti ili kukilinda chama.
Uhosama wa Lissu na Wenje ndio uliochochea hii Vita ya sasa tunayoiona ambayo ni ya kufa na kupona maana atakayeshinda ndio itakuwa nwisho wa aliyeshindwa. Wenje alimtonya Mbowe hizo njama za mapinduzi ambapo awali naye alishirikishwa.
Kiuhalisia hakuna kiongozi wa chama chochote cha siasa hapa nchini hata CCM ambaye amefanikiwa kukijenga chama kama Mbowe lakini hata hilo Lissu, Lema, Diaspora na wanaharakati na wafuasi wao wanajidai hawalioni. Sio bure ni tamaa ya pesa imewafanya wawe vipofu.
Jiulize hivi hao watu wenye uelewa ( wanaharakati; Diaspora na wasomi ( ukiondoa hawa mashabiki wa grassroot ambao ni mbumbumbu) hawaelewi kuwa Tanzania CCM haitaki na haitaruhusu reforms za Tume ya uchaguzi na sheria zake kwa sababu ni kitanzi kwao? Hawaelewi kuwa CCM wanajua fika kuwa wananchi wa nchi hii wamelala usingizi, hawajali na ni waoga hivyo hawawezi kuleta shinikizo lolote litakalofanya CCM wakubali mabadiliko? Hawajui kuwa mwanasiasa wa nchi hii hata awe nani hata akitoka CCM hana watu wa kumsaidia kuweka shinikizo tofauti na nchi zingine kama Kenya, Afrika kusini nk? Katika mazingira hayo Lissu akichaguliwa ataweza kufanya nini ikiwa hana back up ya watu wanaoweza kuingia barabarani? Tena bora Mbowe ambaye anaweza kushawishi CCN wakalegeza japo kidogo hivyo wakapata wabunge na madiwani..
Ni wazi Lissu na timu yake wanajua hili ila kwa sababu lengo ni upigaji ndio maana wanatumia mbinu chafu za kumchafua Mbowe ili wateke nyara chama.
Lema anahoji kwa nini Mbowe aliwakaribisha Halima Mdee na wenzake katika party yake huko kwao nyumbani lakini Lema huyo huyo hajiulizi mbona yeye aliwekwa jela na Gambo muda mrefu akateseka na mateso yale ya jela, wababe wa jela hatujui kama hata walijaribu kummendea, lakini baada ya kutoka amekuwa akizungumza na Gambo na kupanga mambo ya kisiasa , kuna wakati Gambo alitoa siri kuwa Lema alimuomba amuunganishe aongee na Rais , lakin Lema anamkosoa Mbowe kumualika Mdee!.
CHADEMA haitakufa ila itayumba kidogo, na hakutakuwa na impact sana katika nchi hii kwa sababu CCM itaendelea kutawala kwa miaka mingi ijayo hata kama kusingekuwa na mgogoro CHADEMA.