Uhujumu Uchumi: Idd Simba na wenzake waachiwa huru katika kesi ya kuhujumu shirika la UDA

Uhujumu Uchumi: Idd Simba na wenzake waachiwa huru katika kesi ya kuhujumu shirika la UDA

Kuna habari kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi Iddi Simba. Ni ile inayohusu ufisadi wa uuzaji UDA akiwa Mwenyekiti wa Bodi. Aliwekewa Shilingi zaidi ya milioni 300 katika akaunti yake. Nasikia imefutwa kwa mkono wa Ofisi Kubwa kuliko zote katika nchi hii kwa sababu mtoto wa mwenye ofisi ni rafiki wa mnunuzi wa UDA.

chanzo: Jamaa yangu aliyepo mahakamani
 
Yaani mtu anashitakiwa na biashara yenyewe ni ya bwana mkubwa, tena kwenye kesi yenyewe anashitakiwa na Kesena ambaye ni msimamizi wa biashara ya bwana mkubwa kabisa, huoni alimpiga makofi OCD lakini hakufanywa chochote, alafu bado unategemea ashindwe kesi, ingekuwa maajabu
 
Wametumia nafasi hii watu wakiwa wameconcentrate kwenye tukio la Arusha kufutiana mashtaka, wafanye na kwa Mramba na Yona
 
.............Nilijua tu!!.....Eti kesi ya ngedere hakimu ni nyani!!!!!!!!!!!!!!!
 
Du , hela ya umma anaingiza kwenye akaunti yake , halafu hana shitaka la kujibu?
Ufisadi at its highest.
Ningekuwa Hosea naenda likizo bila malipo!!!
Nyie si ndio mnaojifanya Misukule ya akina Mwigulu? Sasa unastuka nini!
 
Kwanza kosa la Uhujumu Uchumi, huwa halina dhamana, sasa nilishanga hata watu hawakushtuka baada ya hawa watu kupewa dhamana. Watanzania tulipaswa kuichukulia ile Dhamana waliyopewa kama red flag.
I saw this coming
Na yeye amerudisha hela ya umma aliyoiba au amewagawia fisadi wenzake? Je shirika la UDA ndio lishanyakuliwa kwa hiyo bei ya bure? Hivi nchi hii ishakua mikononi mwa hao mafisadi kiasi hicho? Inatia uchungu sana.
 
Hivi hakuna wanasheria binafsi wa kufufua kesi hii? Masikini UDA yetu!! Daa!
 
DPP yupo busy na kamanda Lwakatare haya mengine wala hayana maana kwa suluhisho la haya yote kila mwana JF mpenda mabadiliko ahamasishe watu eneo alipo ili 2015 tuwapumzishe magamba wamechoka mwili na akili!! tusikae kwenye key board tu mimi kila week angalau nahakikisha navua magamba mawili matatu na nyie fanyeni hivo!!
 
Kkkkkkkkk x 1000. Watz wote isipokuwa mccm ni wtumwa
 
Kiukweli kabisa,nimestaajabishwa na hii taarifa,maana haingii akilini kabisa,so ina maana jamaa hakuweka hela kwenye account yake binafsi?..

Ombi langu kwa wabunge makini wa CDM (Dar Es-Salaam),hasa kijana mwenzetu John Mnyika tunaomba ulifuatilie hili suala la Ufisadi UDA,sinema ya hii kesi,then utupe taarifa kamili na wayforward,.naamini ujumbe wangu umefika kwako kamanda
 
Duhhh, Mungu wangu, hii ofisi ya DPP kwali ni janga. Ndo maana hata Takukuru wanampiga madongo!
 
Angekuwa idi simba ndugu yako usingeliongea Haya

Kuwa na ndugu kama Iddi Simba haina maana una silika ya ufisadi. ila ni kweli unaweza usitoe maoni JF kama ndugu wa Iddi, lakini ukachukizwa na wizi wake.
 
Angekuwa idi simba ndugu yako usingeliongea Haya

Hii kulindana lindana na kuoneana aibu ninyi Magamba,ndio mmetufikisha hapa tulipo,..mtu anatuhumiwa kuhujumu shirika la usafiri la jiji,wewe unaleta za undugu,mimi angekuwa ndugu yangu na undugu ungekufa tu!!!
 
Halafu the same DPP anamwekea kipingamizi Lwakatare kwa issues za kizushi kama ufisadi anatumia mamlaka visivyo. He is politically operating
huyu dpp siku cdm ikiingia madarakani 'inshallah' awe wa kwanza kuhukumiwa.
 
Back
Top Bottom