Gazeti la Mwananchi la leo limeripoti kuwa Mwenyekiti wa bodi ya UDA, Bw. Iddi Simba na wenzake wamefutiwa kesi hiyo namba 3/2012 ya Uhujumu Uchumi. Katika kesi hiyo Iddi Simba na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa ubadhilifu ulioisababishia UDA hasara ya shilingi Bilioni 8.4. Kesi hiyo imefutwa na DPP kwa maelezo kuwa hakusudii kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao.
Mawazo yangu.
Nakumbuka Kesi hii ilifunguliwa na PCCB dhidi ya Iddi Simba na wenzake kufuatia hasara tajwa hapo juu. PCCB pengine walikuwa na mashahidi wa kuthibitisha tuhuma hizo Mahakamani ndio maana kesi ikafunguliwa. Ajabu sasa kabla haijaanza kusikilizwa DPP kaifuta, na mamlaka ya DPP hayahojiwi na mtu yeyote kwa mujibu wa Katiba na Sheria zetu.
Sasa nimemuelewa Dr. Edward Hoseah alipowalaumu wabunge wiki iliyopita kwamba wamempa mamlaka ya kupambana na rushwa lakini wamemnyang'anya kwa upande mwingine. Kabisa kwa mtaji huu amefungwa mikono. Ni mawazo yangu tu lakini.