Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,650
DPP akili yake nina Shaka nayo,weledi wake pia ninahofu nao. Elimu yake nayo naitilia Shaka mno! Kwa mabilioni yaliyoibwa UDA alafu ufute kesi kiulaini hivi ....you must be kiding!.
Hata kwa wana CCM this is a disgrace!Nimesoma na kurudia mara mbilimbili lakini sijashangaa; siwezi kushangaa kwa sababu hakuna cha kushangaza.
Kisidumu Chama Cha Mapinduzi!
Du , hela ya umma anaingiza kwenye akaunti yake , halafu hana shitaka la kujibu?
Ufisadi at its highest.
Ningekuwa Hosea naenda likizo bila malipo!!!
mahakama ya hakimu mkazi kisutu dar es salaam leo hii imemwachiria huru mwenyekiti wa bodi ya shirika la usafiri dar es salaam (uda), idd simba pamoja na mkurugenzi wa bodi hiyo ambaye alikuwa diwani wa kata sinza (ccm), salum mwaking'inda vile vile meneja mkuu wa shirika hilo victor milanzi na mkurugenzi wa kampuni ya simon group , simon kisena waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa shirika hilo.
Mahakama imewaachia huru washitakiwa kwa sababu mkurugenzi wa mashitaka (dpp), dk eliezer feleshi alliwasilisha hati ya kutokuwa na haja ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2002.
simba anayetetewa na wakili maarufu nchini alex mgongolwa walifikishwa na mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mei 27 28 mwaka jana wakikabiliwa na makosa ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka na kughushi na hujumu uchumi.
Hivyo kuanzia sasa, washitakiwa hao wapo huru.
Gazeti la Mwananchi la leo limeripoti kuwa Mwenyekiti wa bodi ya UDA, Bw. Iddi Simba na wenzake wamefutiwa kesi hiyo namba 3/2012 ya Uhujumu Uchumi. Katika kesi hiyo Iddi Simba na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa ubadhilifu ulioisababishia UDA hasara ya shilingi Bilioni 8.4. Kesi hiyo imefutwa na DPP kwa maelezo kuwa hakusudii kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao.
Mawazo yangu.
Nakumbuka Kesi hii ilifunguliwa na PCCB dhidi ya Iddi Simba na wenzake kufuatia hasara tajwa hapo juu. PCCB pengine walikuwa na mashahidi wa kuthibitisha tuhuma hizo Mahakamani ndio maana kesi ikafunguliwa. Ajabu sasa kabla haijaanza kusikilizwa DPP kaifuta, na mamlaka ya DPP hayahojiwi na mtu yeyote kwa mujibu wa Katiba na Sheria zetu.
Sasa nimemuelewa Dr. Edward Hoseah alipowalaumu wabunge wiki iliyopita kwamba wamempa mamlaka ya kupambana na rushwa lakini wamemnyang'anya kwa upande mwingine. Kabisa kwa mtaji huu amefungwa mikono. Ni mawazo yangu tu lakini.
Na kama hakuna ushahidi wa kutosha basi DPP angeiachia Mahakama ndio iseme hivyo kuwa ushahidi hautoshi. Vitu vingine vinakera sana.
Ikifutwa na mahakama kuna gharama za kusafisha jina la mtu na ni hela ya mlipakodi ingetumika!