Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Nilidhani watanzania wenye akili kama yako tayari wameisha kumbe bado upo! Hatari Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787]. Sasa maabara tu ya kupima Covid 19 mlitupilia mbali !!. Unataka na jirani yako afuate imani zako?!

Tunategemeana sana na hasa ukiangalia takwimu za uwekezaji Tanzania, utaona umuhimu wa Kenya na waKenya Tanzania.
 
Mkuu Paskali haelewi undani wa mioyo ya serikali ya Kenya,kwa ufupi hawatutakii mema.Hakuna maana ya kuendeleza undugu katika EAC yenye watu wasiotutakia Tanzania mema.
Wewe umefahamuje undani wa mioyo ya serikali ya Kenya?
 
Pascal Mayalla,

Mkuu P ahsante kwa kutupa chakula cha "patriotism"

NB: Ukiwa unaandika makala zako style hii zitakua zinavutia kusoma kwakua dunia inatumia sheria moja ambayo ni "less is more"

Vaveja sana.
 
Mpaka Mzee Kambarage kuwapachika jina la "Nyang'au" wale jamaa alikuwa na maana yake. Aliwafahamu vizuri, jirani akikuwashia moto wa mkaa wewe muwashie wa makaa ya mawe.
 
Hawa wakenya ni wababaishaji, kwann hawakuijumugisha Tz katika orodha ya nchi zitakazoingia Kenya? pili, kwanin wanasema Watz wakiingia kenya wakae sero siku 14? na kwann huu utaratibu wa kukaa siku 14 hawakuusema toka mwanzo badala yake tulipofunga mipaka ndipo wanaibuka na hiyo hoja, ningekuwa jpm siwafungulii mpaka watakapotuliza akili ili sikuingine wajifunze ujirani mwema na waache utoto.Kwanza kusema watatufungia siku 14 tukienda kwao tayari wametufukuza.
 
hua tunatumia temporary passport mkuu, mara ya mwisho nmetumia mwaka jana september

Good , wewe ndo unaujua ukweli, temporary passport ambayo unaipata Tz kwenye office za DC ndio unaipeleka upande wa Kenya kugongewa huku mkenya anakuuliza utakaa muda gani Kenya unapigwa week mbili, sasa mayalla ana danganya watu eti utaingia kwa kitambulisho cha NIDA which is not true.

Na kwa taarifa yenu tu Kenyatta ni mzuri sana kwenye kuongea lakini kutenda anayo sema ni ngumu, ndio maana huu umoja unasua sua
 
Tuna historia na kenya muda mrefu tatizo Tanzania tunapenda sifa ya kujiunga na jumuhiya tofauti bila kuangalia maslahi yetu.
Muungano watanganyika na Zanzibar ni shida, East Africa ni shida kabla ya kurudi tena East afrika tungewaambia Kenya warudishe mali walizozuia baada ya East Africa ilipovunjika mara ya kwanza halafu tumeacha kuungana na nchi za maana kama Congo DRC tukakileta kanchi kalaghai kama Rwanda ndio masna ajenda yao kuu ilikuwa ardhi na mambo ya utalii bila visa wakati kila siku kenya wanajitahidi kutangaza vivutio vyetu viko kwao na hata bidhaa za Tanzania zenye mvuto kama konyagi zinawekewa vikwazo vingi
 
Pascal Mayalla, ng'wilage giki ng'wanamhala Papamagamba anamuharibia reputation na sifa kwenye jicho la kiintaneshino.
Show ndogo Kama hizi anashindwa kuzi handle?

Mwana diplomasia gani anatoa macho utadhani anataka kupigana?
Kuonesha ubabe, kutoa macho na kufoka bila kutazama athari zilizopita enzi tulipokuwa na mahusiano mabaya na majirani ama athari zitakazofuatia NDIO UZALENDO WA KWELI!!!
 
Kenyans ni alama kamili ya ubeberu. Beberu akikuona umenuna yeye anakuchekea, akikuona umefurahi yeye ananuna, wanaenda kwa timing ili wakwapue kwa maslahi yao hawa
umeongea vema sana, tatizo la baadhi yetu ni unafiki mtu anakufanyia mambo ya hovyo umchekee tu eti kwa sababu jirani, mbona tulipo jibu akili imewakaa sawa kama wao sio jeuri ni nini? na dawa ya jeuri ni kiburi, Mayala ni msukuma wao huwa wana msemo wao ndoho tabuu hata kama anapingu mkononi anaelekea kwenye defender.
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huwa ninaandika kitu kupitia safu yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye kuhimiza patriotism kwa Watanzania kuwa wazalendo kwa taifa letu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Pia niliwahi kusisitiza humu kuwa unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani, ili uishi vema kwa raha na amani na majirani, ni lazima uwe na upendo kwa jirani yako hata kama unamuhisi hakupendi, wewe mpende tuu na muishi kwa ujirani mwema na jirani yako, na hata kukitokea sintofahamu yoyote baina yako na jirani yako, katika kutafuta suluhisho la simtofahamu hiyo, utangulize kwanza upendo na kuutatua mgogoro wowote na jirani yako kwa kutanguliza njia za kidiplomasia kwanza, diplomacy, zikishindikana ndipo tuje kwenye tit for tat ambayo nayo pia ni diplomacy ya kanuni ya reciprocity.

Kwavile amri kuu ni upendo, mpend jirani yako kama unavyojipenda wewe na umtendee vile unapenda kutenda, na hata ikitokea jirani akaghafilika, akikupiga kofi la shavu lako la mkono wa kushoto, kama una upendo, usimrudishie, bali utamgeuzia na shavu la mkono wa kuume na sio kumrudishia.

Hoja hii ni kufuatia hiki kinachoendelea sasa kati yetu na jirani yetu kuhusiana na yatokanayo na COVID-19 kulikopelekea back biting, kunyoosheana vidole na tit for tat.

Nimenote baadhi ya comments za baadhi yetu sio comments za upendo na ujirani mwema, zenye nia ya kutafuta suluhisho la amani na kidiplomasia bali ni comments zenye hatred na fuelling the situation instead of resolving.

Sasa kwa vile sisi waandishi wa habari, huwa tunauwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, na huwa tunapata access ya kuzungumza na marais wa nchi mbalimbali na katika kuzungumza huko, huweza kuusoma moyo mtu, na mimi niliwahi kupata access ya kuzungumza face to face na Rais Uhuru Kenyatta, hivyo...

Naomba kuchukua fursa hii kuwasisitiza Watanzania wenzangu kuwa nimeusoma moyo wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, anaupendo na Watanzania. Kenya ni jirani mwema. Rais Uhuru Kenyatta, anatupenda Watanzania na ndie yeye alianza kufungua mipaka yake kwa Watanzania sio tu kuingia Kenya bila viza, bali hata bila passport, kitambulisho tu cha taifa zinatosha, tena hadi aka joke mko huru kuwaoa wanawake wao!

Hebu msikilize kwa makini Uhuru Kenyatta anasema nini hapa, je unajua anayezungumziwa ni nani?
Msikilize.



Huyo anayezungumziwa hapo, sii mwingine, bali ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia track record yake kwenye ujenzi wa taifa letu.

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza upendo, Umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya Wakenya na Watanzania katika kujenga Jumuiya moja ya Africa Mashariki.

Pia amethibitisha anampenda Magufuli na anamkubali sana, kwa track record ya kuijenga Tanzania na kuna kitu rais Uhuru Kenyatta ametusisitiza dish Watanzania tukifanye hapo mwezi October, naomba nisikiseme hapa ila kama kuna mwenye
masikio na asikie!.

Namalizia kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, despite all the odds, bado tuwe na upendo kwa majirani wetu wote, leo kwako, kesho kwangu, tutumie njia za kidiplomasia kwanza katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu yoyote, ofcourse kwa kutanguliza mbele Tanzania kwanza na maslahi ya taifa, upendo kwa majirani, upendo kwa wote, tutakuwa na amani, na tutabarikiwa sana!

Nawatakia Jumapili njema

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Umesema vyema
 
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huwa ninaandika kitu kupitia safu yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa" zenye kuhimiza Patriotism kwa Watanzania kuwa wazalendo kwa taifa letu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.

Pia niliwahi kusisitiza humu kuwa unaweza kuchagua marafiki lakini huwezi kuchagua majirani, ili uishi kwa raha, ni lazima muishi kwa ujirani mwema na jirani yako, na hana kama kutatokea sintofahamu yoyote kati yako na jirani yako, katika kutafuta suluhishi, utangulize upendo na kuutatua mgogoro wowote na jirani yako kwa kutanguliza njia za kidiplomasia kwanza, diplomacy, zikishindikana ndipo tuje kwenye tit for tat ambayo nayo pia ni diplomacy ya kanuni ya reciprocity.

Kwavile amri kuu ni upendo, jirani akikupiga kofi la mkono wa kushoto, kama una upendo, utamgeuzia na mkono wa kuume na sio kumrudishia.

Hoja hii ni kufuatia hiki kinachoendelea kati yetu na jirani yetu kuhusiana na COVID-19 kulikopekea back biting na tit for tat.

Nimenote baadhi ya comments za baadhi yetu ni comments sio za upendo wala kutafuta suluhisho la kidiplomasia basi ni comments zenye hatred na fuelling the situation instead of resolving.

Sasa kwa vile sisi waandishi huwa tunapata access na marais wa nchi, na mimi niliwahi kupata access ya kuzungumza face to face na Rais Uhuru Kenyatta.

Naomba kuchukua fursa hii kuwasisitiza Watanzania wenzangu kuwa Kenya ni jirani mwema. Rais Uhuru Kenyatta, anatupenda Watanzania na ndie yeye alianza kufungua mipaka yake kwa Watanzania sio tu kuingia Kenya bila viza, bali hata bila passport, kitambulisho tu cha taifa zinatosha, tena hadi aka joke mko huru kuwaoa wanawake wao!

Hebu msikilize kwa makini Uhuru Kenyatta anasema nini hapa, je unajua anayezungumziwa ni nani?
Msikilize.



Huyo anayezungumziwa hapo, sii mwingine, anamzungumzia Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia track record yake kwenye ujenzi wa taifa letu.

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza upendo, Umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya Wakenya na Watanzania katika kujenga Jumuiya moja ya Africa Mashariki.

Pia amethibitisha anampenda Magufuli na anamkubali sana, kwa track record ya kuijenga Tanzania na kuna kitu rais Uhuru Kenyatta ametuhusia Watanzania tukifanye.

Mwenye masikio na asikie.

Namalizia kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, despite all the odds, bado tuwe na upendo kwa majirani wetu wote, leo kwako, kesho kwangu, tutumie njia za kidiplomasia kwanza katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu yoyote, ofcourse kwa kutanguliza mbele Tanzania kwanza na maslahi ya taifa, upendo kwa majirani, upendo kwa wote, tutakuwa na amani, na tutabarikiwa sana!

Nawatakia Jumapili njema

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Mayala bwana, kwahiyo unataka ile mambo ya unapingu mkononi na unapandishwa defender halafu una sema NDOHO TAABU.
 
Wachangiaji wengine bana kama macho** wewe yule kasema tusiende kwao wewe unataka kwanza kumbembeleza si ufala huo kwani ana figo yako yule au kakushikia nguvu zako za kiume......lazima tuwe negative kwenye ufala kama huu akileta fuvu unareta maiti isiyo kuwaa nandugu akireta nyoo unaweka nyoo akiweka ugoko unaweka chuma ......wakenye wanajikutaa starndand sana.....na hii ni mbaya kujiona bora kushinda mwenzako akati unataka na unauza mabilioni ya bidhaa zako kwake huo ni usen*** wa kiwango cha lami.......na hata mimi ningekuwa raisi ningefunga mpaka kabisa mwaka mzima wa uko wauko na uku ni uku ili kuikomesha huu ufala kabisa tunaoletewa.....unakazania corona ipo Tanzania mbona uku tuko sawa ........kama unaumwa ni wewe ulitaka kuwafata mabahasha wako wa kizungu ......haafu unazuia Tanzania unaruhusu china .......hakika kenyata nikikukuta peponi nakukimbiza na jiwe mpaka malaika washangae
 
Naunga mkono hoja, kwa maoni yangu Tanzania tume overreact, kulikuwa hakuna sababu, siyo jinsi ambavyo watu matured wanavyopaswa kutatua matatizo, inanikumbusha ex girlfriend wangu, ilikuwa nikikosea kidogo tu hata kama tumepishana kidogo sana hiyo revenge yake unaweza kujiua, alikuwa immature, ...
Hahahaha! wakati wowote unaweza kuwa msiba.
 
Back
Top Bottom