Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Uhuru Kenyatta jirani mwema, atupenda Watanzania, amkubali sana JPM. Asisitiza upendo, umoja na ushirikiano kati Wakenya na Watanzania tujenge EAC 1

Tanzania tungekuwa na bahati sana kama tungekuwa daima tunawapata viongozi wanaotushikanisha na Dunia kuliko kutubomoa kutoka kwenye Dunia.

Faida ya kuwa na mahusiano mazuri na Dunia ni nyingi kuliko kila mara kuwa na matendo yanayotutenganisha na Dunia.

Utawala wa awamu, kwa kiasi kikubwa, umeyumba na kulegalega kwenye mambo mengi ya msingi, ukiwemo ihusiano wetu na Dunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siyo kila uhusiano unafaa
 
Ushauri mzuri lakini hapo kwenye kupigwa kulia ugeuze kushoto nakataa. Kama kweli ni jirani mwema kwanini anipige kofi at the first place. Wakenya ni wajinga, atakupiga kulia utamgeuzia kushoto kesho atataka akupige vibao makalioni. Sometime ili ueleweke ua mende kwa nyundo.

Awamu ijayo piga chini Pakamaganda Kabundi teua February Makanda
 
Wanabodi,
Hebu msikilize kwa makini Uhuru Kenyatta anasema nini hapa, je unajua anayezungumziwa ni nani?
Msikilize.



Huyo anayezungumziwa hapo, sii mwingine, bali ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia track record yake kwenye ujenzi wa taifa letu.

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza upendo, Umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya Wakenya na Watanzania katika kujenga Jumuiya moja ya Africa Mashariki.

Pia amethibitisha anampenda Magufuli na anamkubali sana, kwa track record ya kuijenga Tanzania na kuna kitu rais Uhuru Kenyatta ametusisitiza dish Watanzania tukifanye hapo mwezi October, naomba nisikiseme hapa ila kama kuna mwenye
masikio na asikie!.

Namalizia kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, despite all the odds, bado tuwe na upendo kwa majirani wetu wote, leo kwako, kesho kwangu, tutumie njia za kidiplomasia kwanza katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu yoyote, ofcourse kwa kutanguliza mbele Tanzania kwanza na maslahi ya taifa, upendo kwa majirani, upendo kwa wote, tutakuwa na amani, na tutabarikiwa sana!

Nawatakia Jumapili njema

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Back
Top Bottom