Wanabodi,
Hebu msikilize kwa makini Uhuru Kenyatta anasema nini hapa, je unajua anayezungumziwa ni nani?
Msikilize.
Huyo anayezungumziwa hapo, sii mwingine, bali ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli kufuatia track record yake kwenye ujenzi wa taifa letu.
Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza upendo, Umoja, mshikamano na ushirikiano kati ya Wakenya na Watanzania katika kujenga Jumuiya moja ya Africa Mashariki.
Pia amethibitisha anampenda Magufuli na anamkubali sana, kwa
track record ya kuijenga Tanzania na kuna kitu rais Uhuru Kenyatta ametusisitiza dish Watanzania tukifanye hapo mwezi October, naomba nisikiseme hapa ila kama kuna mwenye
masikio na asikie!.
Namalizia kwa kuwasisitiza Watanzania wenzangu, despite all the odds, bado tuwe na upendo kwa majirani wetu wote, leo kwako, kesho kwangu, tutumie njia za kidiplomasia kwanza katika kutafuta ufumbuzi wa sintofahamu yoyote, ofcourse kwa kutanguliza mbele Tanzania kwanza na maslahi ya taifa, upendo kwa majirani, upendo kwa wote, tutakuwa na amani, na tutabarikiwa sana!
Nawatakia Jumapili njema
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali