Uhuru na Haki Haiwezi ikaleta Amani na Maendeleo ya Watu; Amani na Maendeleo ya Watu ni Tunda la Uhuru na Usawa

mkuu sijaelewa apo,kama haki ilikuwepo tangu mkoloni why tulitafuta uhuru ili hali " Haki inahusiana na uhuru"
 
Kwa hiyo huujui mkasa wa nyumba za Serikali?
 
mkuu sijaelewa apo,kama haki ilikuwepo tangu mkoloni why tulitafuta uhuru ili hali " Haki inahusiana na uhuru"
Haki ilikuwepo hata wakati wa uhuru. Kuna tukio moja liliwahi kumkuta Baba wa Taifa Hayati Mwl. J. K. Nyerere, 1942 wakati akiwa Tabora Boys... Alianzisha vuguvugu kupitia mdahalo wa kutaka walimu wa kiafrika wapatiwe nyumba za karibu na shule kama ambavyo walimu wa kizungu walikuwa wakipatiwa. Na yeye aliita ni haki ya walimu waafrika kwa kuwa ni walimu kama walimu wazungu. Lakini kumbe ni kitu asichokifahamu kuwa kwenye mikataba yao ya kazi wale walimu waafrika walifahamu kuwa haki yao ilikuwa si kuishi katika nyumba zile za shule, hiyo ilikuwa ni haki ya walimu wazungu.

Sasa baada ya kugundua hilo na hasa alipofika katika siasa za TAA, alifahamu kuwa Tanganyika tulikuwa hatuna usawa. Kwamba mzungu alipewa nafasi ya juu kuliko mtanganyika, na hivyo mzungu alikuwa na haki iliyozidi haki ya mtanganyika. Kwa hiyo hitaji la usawa na kuacha kunyonywa na wazungu ndio likawa hitaji la kitaifa na hata tukapata uhuru 1961, ambapo baada ya Tanganyika kuwa Jamhuri mtanganyika alihesabiwa kuwa mtu sawa na Muasia pamoja na mzungu.
 
Unaongea mambo meeeengi japo hujatwambia nani aliyesababisha hayo mambo yasiwepo mpaka leo nusu karne baada ya uhuru? Mkuu nchi hii haijawahi KUTAWALIWA na chama kingine zaidi ya hiking chama cha Wezi, wanafiki na waongo!
Hivi kiongozi mwadilifu anawezaje kutunga SHERIA INAYOZUIYA ASISHITAKIWE AWAPO/ ASIPOKUWEPO MADARAKANI?
Ivi mtu aliyekuwepo kiongozi kwa miaka yote leo anakuaje kusema kwamba yy ni wa mfano na yale yote yaliyotokea huko nyuma hakuwa sehemu YAke?
Unadhani uanhisi unaongea na watoto wasioelewa mambo! Pole sana
Ccm ni ileile hata wakikaa madarakani miaka 500 hawana uwezo wa kubadilisha kitu.
Anachokifanya wewe ni kuleta porojo porojo tu.
Watu wanalima wakivuna wanaporwa kama wale wa KOROSHO we unasema sijui heshima ya mtu?
Hivi mtu anayekunywa maji ya rope kule bahi hiyo heshima na usawa utaipata wapi?
 
Kinoamiguu:

Wewe umepaniki, nakushauri kanywe maji kisha uje tuendelee na mazungumzo mkuu.
 
Kinoamiguu:

Wewe umepaniki, nakushauri kanywe maji kisha uje tuendelee na mazungumzo mkuu.
Mm sijapaniki mkuu wewe tuendlee tu. Unayoongea wewe ni slogan zilzile. Wenzako tunaposema USAWA. Na haki TUNATAKA mtu mmoja raisi asipange mwenyewe Badala yetu hapana.
Mfano ni watz wangapi waliulozwa kupitia kwa wawakilishi wao kwamba
TUNATAKA ndege Badala ya Madawati?
Tukajenge uwanja wa ndege chato Badala ya musoma au kigoma?
 
Kinoamiguu:

Nimefurahi kusikia hujapaniki mkuu. Ni kweli kwamba tangu uhuru hata sasa, CCM kimeendelea kuwa ni chama tawala Tanzania, hata wakati ule wa TANU na ASP. Na kwa wakati wote huo, kimejitahidi sana katika kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi ili kuendana na mahitaji ya watanzania kutoka mahitaji yale ya wakoloni, ijapokuwa kimepitia wakati mgumu sana lakini kimefanikiwa.

Lengo la kutawala kwa chama kimoja mara baada ya uhuru lilikuwa ni zuri kwa maana kusudi lake ni kuwaunganisha watu kuwa wamoja katika falsafa moja kwa ujenzi wa nchi. Na hili limefanyika katika mataifa karibu yote duniani ambayo yalijikomboa kutoka ukoloni, ikiwemo Amerika yenyewe katika miaka ya 1780's. Lakini zilibadilisha mfumo ili kuongeza wigo wa ushiriki wa watu katika siasa za nchi na kuongeza demokrasia. Ndipo hapo mataifa mengine yaliingia katika vyama vingi huku zikitumia ama mfumo wa Serikali wa kibunge au Rais.

Mifumo yote hiyo, inaipa nguvu ama upande wa Bunge au Rais lakini nguvu hizo zitatoka kwa wananchi. Marekani yeye alichagua mfumo wa serikali wa Rais, badala ya ule wa kibunge kutoka kwa mkoloni wake Muingereza. Lengo ni kujipa uhuru kamili na kuachana kabisa na viashiria vya ukoloni, wa uingereza. Walichagua kumpa mamlaka Rais lakini waliipa nguvu Bunge kwa ajili ya kumshauri na kumsimamia Rais. Hii inamaana kwamba Urais ni dhamana ya wengi kwa ajili ya maslahi ya wengi. Tanzania tuliiga mfumo wa Serikali wa Amerika na wa uingereza tukaiweka pamoja na kupata mfumo ambao tunautumia sasa.

Tulifuata mfumo wa Serikali wa Rais na Bunge. Rais ni sehemu ya Bunge na kwamba mamlaka ya Rais na Bunge ni nusu kwa nusu. Serikali inafanya kazi zake kwa kushirikiana na Bunge. Kwamba katika utekelezaji wa majukumu ya serikali Rais ni kiongozi wa Serikali na Waziri Mkuu ni kiongozi wa Serikali Bungeni. Kwa hiyo Tangu uhuru hadi hivi leo hakuna jambo ambalo Rais amelitekeleza pasipo baraka za Bunge kwa maana ya wawakilishi wa wananchi kupitia wabunge. Ifahamike kuwa nchi yetu infuata mfumo wa demokrasi ya ushirikishwaji kwa kutumia wawakilishi wa wananchi, na huo ndio utawala wa sheria.

Kwenye kujenga uwanja wa ndege wa chato ushafahamu ni kwa namna gani ambapo serikali na Bunge limeweza kushirikiana vema. Hivyo basi ujenzi wa uwanja huo una baraka zote za Wananchi kupitia wawakilishi.

Nimekupa mfano huo wa stori ya Marekani ili tukalibiane katika kuifahamu hii mifumo ya serikali katika utendaji wake wa kazi. Kwamba katiba ya Tanzania imetoa mamlaka kwa wananchi kupitia bunge chini ya uongozi wa kiongozi wa Serikali Bungeni ambaye ni Waziri Mkuu.
 
Nimepoteza muda want kusoma utumbo mtupu kutoka Lumumba kwa wapiga magoti .
 
Acha kujichanganya na kujaribu kuchanganya wengine! Huwezi kuzungumzia usawa, bila haki kwani haki ndo inayoleta usawa! Maendeleo ya kweli hayawezi letwa katika nchi yoyote bila kwanza kuexercise haki na usawa kwa vitendo na sio kwa maneno matamu!
 
Yaani una subject haki kwenye usawa ?

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 

..basically unacheza-cheza na maneno au lugha.

..ngoja kwanza tujaribu Uhuru, Haki, na Maendeleo.

..wakituzingua tutajaribu wanaohubiri amani kama unavyotaka.
 
Kama hujui maana ya haki sidhani kama utaelewa kuwa Usawa upo kwenye haki.
Usawa hauwezi kuwa kwenye haki, ila haki itapatikana ikiwa watu watakuwa huru. Na uhuru utakuwa na maana ikiwa watu watakuwa sawa, na huko ndipo ilipo amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…