Uhuru wa Habari Tanzania: Kati ya Waparaji na Wakunaji Wazuri, Nani Watamsaidia Zaidi Rais Samia?. Tunakuomba Mama, Usiwaparure Waparaji!.

kabla sijaenda mbali wewe kaka mayala tuambiye mparaji at mparulaji?
 
kabla sijaenda mbali wewe kaka mayala tuambiye mparaji at mparulaji?
Mparaji ni mtu ambaye ameombwa kumkuna mtu, badala ya kumkuna vizuri, anamkuna vibaya kama kumpara samaki. Mama katoa onyo, ukimpara, atakuparura!, au utaparuriwa!.
P
 
Kuwaogopa waparaji ni kielelezo cha mtu asiependa challenges, anataka kufanya kazi kwa mazoea, na haya mazoea ndio yanaturudisha mikononi mwa wapigaji.
Naunga mkono hoja, maadam Mama ameishasema ana ngozi ngumu, it's good sisi media kujua preference yake ni kukunwa vizuri, ametoa promise ya zawadi ya media hizo na waandishi watakao mkuna vizuri, nao watakuwa vizuri, watapapaswa na kupulizwa ufuu...ufuu. Hivyo sasa kwenye news rooms, ni mashindano ya kukuna vizuri.

Tatizo ninaloliona ni ikitokea muwasho kwenye magaga, hata ukune vizuri vipi, haitasaidia, kwenye magaga ni lazima kusugua gaga, hivyo ni lazima umpare, baada ya kujua ukimpara atakuparura, jee kuna waandishi watathubutu kumpara?.
P
 
Bado sana kuwa katili. Yaan si character yake kabisa
Mkuu Detective J , asante for this
Hili pia lina thread yake
P
 
Dr. Bashiru Ali Kakurwa, amempara mtu, sasa watu wamemshukia na kutaka awajibishwe, hivyo wanasubiri kwa hamu aparuliwe!. Tunamuomba Mama, kwa vile alikiri kwa kinywa chake kuwa ana ngozi ngumu, tunamuomba huu ndio wakati wa kuthibitisha ana ngozi ngumu, Dr. Bashiru, kampara, tunamuomba asimparure!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…