tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Sasa ni rasmi uhuru wa habari na uandishi wa habari zenye tija umefika tamati. Tajiri na kada maarufu wa CCM, ambaye ni mfuasi wa siasa za mrengo wa kushoto, amelinunua gazeti la Mwananchi. Hapa nchini tulikuwa tumebakiwa na gazeti moja tu linaloandika habari zenye tija. Sasa gazeti hilo limenunuliwa na Rostam Aziz kwa 💯%.
Huu ulikuwa mkakati wa muda mrefu uliolengwa na serikali kuzima kabisa uhuru wa habari hapa nchini. Baada ya Rostam kushika hatamu za gazeti hili, usitegemee kwamba litaandika habari zenye tija tena. Ni rasmi sasa litakuwa linaisifia serikali ya Samia kila kukicha na kupindisha ukweli wa taarifa ili kuifurahisha serikali ya CCM na wafuasi wake.
Ukinunua gazeti la Mwananchi kuanzia sasa ni kama umenunua gazeti la Uhuru, Mzalendo, HabariLeo, Daily News, na magazeti mengine yenye mwelekeo wa kichawa. Tukumbuke Rostam aliwahi kununua kampuni ya magazeti iliyoitwa New Habari Corporation lakini ilikufa kifo cha mende baada ya Rostam kuingiza mambo yake ya kiCCM kwenye uandishi wa habari. Aliwafukuza waandishi wa habari mashuhuri, wakiwemo Generali Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Padri Karugendo, Majid Mjengwa, Joseph Mihango, Ayubu Ryoba na wengine waliokuwa wakiandika habari za uhakika. Baada ya kuwafukuza hawa waandishi nguli, aka recruit machawa wa CCM waliokuwa wakiandika habari za kuisifia CCM na kufumbia macho ufisadi. Matokeo yake, kampuni ilikufa kifo cha mende.
Utaratibu uleule uliotumika kuua kampuni ya New Habari ndio wanaotaka kuutumia kuiua kampuni ya Nation Media Group inayomiliki magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Tutarajie kampuni hii nayo itakufa muda mfupi ujao.
NMG ikifa na uhuru wa habari nao utakuwa umekufa 💯%. Habari zote zitatawaliwa na magazeti ya kichawa kama Nipashe, Wamachinga, na Mwanahabari pamoja na TV na redio za CCM kama vile TBC, Chanel 10, Uhuru FM, Magic FM, nk.
Pia tukumbuke kuwa baada ya vyombo vyote hivi kununuliwa na CCM, chombo pekee huru kitakachobaki ni JamiiForums. Ndio maana wanajitahidi kila siku kuipiga pin JF ili tukose mahali pa kukimbilia. Anyway, Mungu atawaadhibu wote wanaoshiriki mchezo huu mchafu sawasawa na matendo yao ovu. Mungu wetu hajawahi kushindwa.
www.thecitizen.co.tz

Tanzanian businessman Rostam Aziz buys Kenya's Nation Media Group
The Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED) has announced an agreement to sell its entire shareholding in Nation Media Group (NMG) to Rostam Aziz through his company, Taarifa Ltd.