Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Mbona january na makamba,zito na kinana walimtukana magufuli na hawakufanywa kitu?
 
Watu kueleza hisia zao ambazo ni tofauti na unachokiamini wewe ndio uchochezi? Alipofanya Magufuli hivyo mlilalamika weee, sasa mnamshauriana kurudi tena huko huko kwenye kuminya maoni ya watu! Kisa DPW! Jueni kuwa Watanganyika hatujapenda bandari yetu kugawiwa hivyo mlivyoigawa.
 
Nina wasiwasi na elimu yako.
Itakuwa ni ya kuunga-unga ndo maana hata kuandika Kiswahili fasaha hujui.
Wewe ni wa kupuuzwa tu maana udini umekujaa sana
 
Hizi kelele zote unazo ona watz wanapiga kulinda bandari yao ni matunda ya Magufuli kuwazindua watz juu ya kulinda rasilimali zao!

Baki na upumbavu wako wa kiarabu
Magufuli angekua analinda rasilimali za nchi hii ansingekubali kumuuzia migodi ya dhahabu Professor John lawson Thornton wa Barick PLC
 
Kwa kauli hiyo tujiulize, kama katiba ni hiyo hiyokinachomzuwia Rais wetu wa sasa kuwa "dikteta" ni nini? Hususan zinapoanza kejeli kwake, kwa Uzanzibari wake na hata kwa Uislam wake?
Bado hujabadilka chochote, hapa unafanya hadaa kwa sababu hali imebadilka.

Unataka kuweka mipaka ya kujieleza kwa kigezo cha nan. Chako?

Viongozi hutofautiana tabia, lakini matokeo ya kazi zao yakawa sawasawa kabisa.
Mmoja atatumia maguvu na kuumiza watu kwa kutumia vyombo vya dola na baadhi ya watu wakaumizwa.
Kiongozi mwingine atatumia njia tofauti kabisa, kama ya kubembeleza, huku akifanya madudu zaidi yanayoumiza raia wengi zadi na kuliweka taifa katika hatihati.
Wewe utaona huyu wa pili ni bora, kuliko yule wa kwanza; mimi naona wote ni wabovu, na pengine huyu wa pili ni mbovu zaidi.

Samia anaonyesha wazi kabisa kwamba hana mapenzi na nchi hii. Hata kama hii ni 'perception' tu, hivyo ndivyo anavyojionyesha kwa watu wengi sasa hivi.

Hakuna rais yeyote wa nchi hii aliyefikia kiwango hiki cha kutoaminika katika matendo yake kuliko huyu alipofikia.

Mwisho, inakuwa sasa kana kwamba unamhimiza Samia na yeye afanye kama alivyofanya Magufuli ili watu wanyamaze.
Sasa niambie, mtu kama wewe unao uhalali gani wa kuleta mada kama hii uliyoianzisha hapa!
 
DP World wanakuja kutawala Nchi na sio kufanya biashara.
Biashara gani ya kushusha makontena halafu unataka Bandari zote ziwe chini yako?
Kuna uhusiano gani wa kushusha makontena na kutawala Bandari zote.

Kwani Bandari kazi yake ni kushusha makontena tu.

Eti wasikatishwe kazi zao hadi mwisho wa shughuri za Bandari. Bandari inamwisho upi?
 
Ujutie kwa post yako isiyo na mshiko, kwan isingekuwa mkataba mbovu nan ungemuona anaongea haya yote, sis ajenda yetu ilikuwa katiba mpya
Mkataba upi unaouuzungumzia, mbona huo mkataba sisi hatuuoni mnauona nyinyoi tu? Su makubaliano ya mahusiano ya nchi mbili ndiyo yamekuwa "mkataba"?

Hizo "spinning" ndizo zinazoshangaza. Hakuna cha kujutia, na hapa nimeweka tahadhari kwa utu uzima wangu. Usifikiri chochoko zitawaumiza wanene huko, hizi zitatuumiza mimi na wewe. Zisipodhibitiwa mapema majuto yatakuwa mjukuu.

Huo mkataba ni upi unaouongelea wewe? Au kuna mkataba ambao wengine hatujauona?
 
Rais si ameamua kuwaacha eti Demokrasia ngoja wamuoneshe gani wanayoiweza ya kupiga Domo na mbaya zaidi Rais mwenyewe hajui kuongea hana mdomo Sasa sijui itakuaje..

Ni hivi wajinga huwezi kuwapa uhuru usio na mipaka watapeleka Hadi nguruwe msikitini eti ni sadaka.

Niliwahi kuandika mwaka Jana kwamba Kwenye Nchi ilivyojaa wajinga hutakiwi kuacha Kila mtu akaripoka watakuona dhaifu na hufanyi kitu..
 
Chuki uhasama ni mbegu inayopandwa na watu wanaowaita wenzao wajinga huku wao wanafanya ujinga ule ule.

Mfano Mwanasheria mmoja na kakundi kake ka wahuni anasimama mbele ya Camera anasema wananchi waelewe au wameamua ukijiuliza ni link hao wananchi tulimtuma au ametumia kipimo gani kusema wananchi hawaelewi ili awe na uhalali wa kutusemea.

Ni kweli Mkataba wa DPW unahitaji uchambuzi na ufafanuzi wa kutosha ingawa lazima itafika mahali makundi mawili yatatokea na kila kundi litabakia na msimamo kulingana na jinsi watakavyo elewa. Sasa kutokana na mabishano hayo ni lazima mwisho wake ni kukubali kutokukubaliana.

Wale Mawakili pamoja na upuuzi wao wa kutoa hukumu kabla kesi haijasikilizwa lakini wamefanya jambo jema kupeleka jambo hili mahakamani ili waliopewa dhamana ya kutafsiri sheria watusaidie na wakitekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kwa kumuogopa Mungu tutafikia muafaka ingawa unaweza kubashiri kwamba pande moja ikishindwa itazusha mambo kadha wa kadha lakini muhimu tutakuwa na Precedent ambayo vizazi na vizazi vitaendelea kuwalaumu endapo maamuzi yatakuwa yana athari kwa wa Tanganyika.

Siku zote tumekuwa tukielezwa kwamba jambo likiwa Mahakamani halitakiwi kujadiliwa linaweza kuathiri maamuzi ya Mahakama.

Ni muhimu sasa pande zote mbili zikusanye ushahidi na kuisaidia mahakama itoe hukumu ya haki na hiyo ndiyo Demokrasia kila mmoja anayo haki ya kupinga hoja kama ambavyo wale wanaojiona siyo wajinga wanavyotumia haki yao ya kuwaona wenzao ni wajinga.

Wengine wameanza kuaga eti wanatishiwa kuuwawa huku wanasahau kwamba waliwahi kusema kwamba wao ni super hawaogopi MTU na hakuna wa kuwafanya lolote!

Mwisho. kwangu Mimi pia ninahamu nifahamu undani wa mkataba kama kweli Serikali ilifanya kwa nia njema na kwa bahati mbaya terms za mkataba hawakuzielewa vema kutokana na Mazingira yaliyowatokea au walidanganywa yote haya yanaweza kupatiwa majibu na Mahakama baada ya hapo tutakuwa na haki ya kupongeza au kulaumu.
 
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
Kwakweli too much of everything is harmful !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…