Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Nenda pale kwenye twitter ya Lisu ameweka ushahidi namna kula zilivyoibiwa pale kawe kwa Halima. Acha ujinga
kwa hiyo haijui mahakama? Toa hilo kamasi la upumbavu km ana ushahidi angeenda mahakamani, Tundu ni mzushi anaweka data za kupika mpuuzi yule.
 
Hao ni kina bibi Faiza na babu The boss wao wanafikiri kwenye uislam zaidi kuliko hoja….,

Wao kila mwarabu wanaona ni ndugu yao wako radhi tumpe kila kitu
Kuna kubwa jinga umelisahau kila utakachomwambia mara sijui abdusyks nan cjui, sijui redio Tehran
 
..
Naamini Uhuru wa kujieleza una mipaka yake kisheria.

Nimekuwa nikifuatilia nyuzi na mijadala yako, kuhusu IGA tangu imeanza, unakuwa na jaziba hadi kutukana. Hiyo ni dalili ya kushindwa kujibu hoja, au nyuma yake una agenda binafsi?

Na wewe heshimu na AMINI UHURU WA KUJIELEZA (kwa kauli yako)
 
Kama hampendi Samia asemwe kwa maneno makali basi pia msipende anapopewa sifa za uongo uongo na za kujipendekeza.

Cut both ways.
Sifa za uongo uongo hata mimi siapatani nazo, hata za kweli zikizidi inakuwa ni karaha.

Kuna mambo mengine ni kazi na jukumu lake na mtu anaetenda kazi yake kiufanisi zaidi kumuenzi si lazima iwemisifa kedekede. Ahsante kwa kazi njema, inatosha.

Ni hoivyo hivyo anapoonekana kakosewa akosolewa kiweledi na kwa ushahidi na kwa heshima. Mbona ni ukweli kabisa kuwa ni msikivu, na anayafanyia kai malalamiko ya watu, tena kwa haraka sana, hana.

Nnachomkubali mimi hana longolongo nyingi kama tulizozizowea kwa wanasiasa wetu, iwe wa CCM au wa upinzani, wote wana longolongo nyingi, Yeye ni vitendo tu. Vitendo vyake na maamuzi yake yanadhihirisha uungwana wake.

Hawa "chawa" walishazowea kmwaga misifa kwa mwendazake, mtu kama yule aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani, alikuwa anamwaga misifa mpaka anakera, kumbe yeye mwenyewe fisadi.

Tena hao wenye kuzidisha sifa inafaa mama awafanyie uchunguzi maalum, isije kuwa wanahificha nyuma ya pazia la misifa.

"Pat on the back" inakubalika lakini isizidi mpaka ikawa "kick on the back".
 
Haakuna shaka yoyote, kwa sasa hivi tunaona Watanzania wengi, wanaojiita wasomi, wanaojiita mawakili wakitowa maoni yao kwa lugha ambazo ni za kuudhi, kukebehi, kukejeli mapa kutusi.

Haya yanayoendelea si maoni tena bali ni vunjifu wa amani uliokusudiwa. Uhuru wa maoni ni lazima uwe na mipaka.

Mtu anajiita mwanasheria msomi au wakili msomi , mwanasiasa, anasimama kwenye majukwaa ya habari na kurusha matangazo yaliyojaa chuki kuwa nchi inauzwa, au bandari inauzwa, Wazanzibari waniuza nchi. Na cha kushangaza sana waziri wa habari amekaa kimya. Waziri wa sheria amekaa kimya. Waziri wa mambo ya ndani amekaa kimya, waziri wa ulinzi amekaa kimya.

Nashauri, vyombo vya habari vyote vinavyorusha matangazo ya chuki vichukuliwe hatua kali za kisheria. Wale wote wanaosimama majukwaani na kufanya uchokozi wa makusudi wachukuliwe hatua za kisheria.

Mpaka sisi tuliozowea mitandao ya kijamii tunawashangaa moderators wapo kimya, watu wanaporusha matusi na kejeli mpaka kwa Rais na mawaziri wake. Hivi hatuyaoni? Au tunapenda huu uchokozi uendelee mpaka uzae madhara?

Kuuwasha moto ni kwepesi sana, kazi inakuja katika kuuzima.

Mimi nadhani wale wote wanaodai nchi imeuzwa waende mahakamani au kwa wao kupeleka madai au serikali iwaite mahakamani waje kuonesha nchi imeuzwa wapi na kwa lipi zaidi?

Nahisi kuna watu wapo nyuma ya pazia amabao wanadhani labda yataishia kiwepesi wepesi yakiachiwa yaendelee. Sasa hivi tayari chuki za wazi zinajionesha kati ya Wasio EWaisslam na Waislam, wasio Waarabu na Waarabu, Wabara na Wazanzibari. watu wa pwani na wasio wa pwani.

Hivi hayo yote kweli yamesababishwa na makubaliano ya Dubai na Tanzania yaliyopitishwa bungeni au kuna yanayoendelea nyuma ya pazia ambayo hatuyaelewi?

Tunaionmba serikali ichukuwe hatua za dhati, kila anaerusha au kuongea chuki akajieleze kwa ushahi wa hayo ayasemayo, kama hana ushahidi aseme ukweli ni na nani yupo nyuma yake anaemlipa au kumchochea kufanya hivyo.

Serikali itumie mbinu za kawaida na zisizo za kawaida za kiusalama ili kulinda raia wa nchi hii kujiingiza katika chuki na migogoro isiyo ya lazima. Huu ni mtego wa panya watania waliokuwemo na wasiokuwemo.

Naamini katika uwazi na ukweli na naamini katika uhuru wa maoni na habari, lakini kila uhuru ni lazima uwe na mipaka yake. Naona au Tanzania hatuna mipaka ya kujielezza maoni yetu aukama tunayo ama hatuijuwi au tunaiwachiie makusudi mipaka inavukwa?

Serikali, hususa Waziri wa habari, Nape Nnauye tueleze tupo bado ndani ya mipaka ya sheria au tumekiuka? Kama bado upo ndani ya mipaka ya sheria za uhuru wa maoni, tunaomba shertia zikafanyiwe ukarabati. Ili tuwe nchi yenhe kuheshimu utowaji mapni yetu uwe wa kuheshimiana.

Wewe kama hupendi nilichosema au kufanya mimi nifahamisheni usinitukane.

Moderators wa JF tunaomba majukwa haya siasa na habari mchanganyiko yapewe kipa umbele ili yasiwe ni chimbuko la maafa.
Tundu Lissu akiongea na waandishi wa habari amesema haya...

Kwenye mamlaka ya moja kwa moja waliyonayo kama Wazanzibar kwenye huu MKATABA kwa makusudi kabisa hawajajumuisha bandari ya kwao Zanzibar ilhali ni jambo la MUUNGANO.

Hawa WAZANZIBAR wameuza mali yetu Watanganyika kwa MKATABA wa milele. Namaanisha hadi bahari itapokauka!"

Mimi ninao huo MKATABA lakini sijaona wapi pameandikwa tutapata hizo hela zinazosemwa na wapambe waliohongwa."

Ni wazi wao kuanzia Samia, Mbarawa na Katibu mkuu wa wizara husika ni WAZANZIBAR na kwa makusudi wameuza mali ya Tanganyika kwa sababu haiwahusu!"

Wengi wenu mnafikiri ni bandari pekee imeuzwa na hao WAZANZIBAR mnajidanganya! Kwa mjibu wa MKATABA hiyo reli ya Magufuli na mabarabara ni ya waarabu hadi maeneo yote maalum ya kibiashara yanakuwa yao."

Bandari kavu kwa mfano ile ya Isaka na zingine zote zinakuwa za waarabu wameuziwa na Samia ambaye ni Mzanzibar."

DPW wamehonga karibia kila awaye na ushawishi. Waandishi zaidi ya 40 walipelekwa kula raha na miongoni mwao yupo mmoja amenieleza kwa siku tatu alizokaa kule alirejea na hongo ya mililioni 6!"

Kama kweli huo mkataba una manufaa na faida kwanini hao WAZANZIBAR ( Samia na Mbarawa ) wameziacha bandari zao?!"

HATUPO TAYARI RASILIMALI ZETU WATANGANYIKA ZIUZWE HOVYO NA WAZANZIBAR - HATUPO TAYARI NASEMA!"

Hili suala halitaisha leo wala kesho na lazima Samia atambue. Huu MKATABA haufai na mbovu kuliko ubovu wenyewe!"

Lissu.
 
Hilo ni sawa kabisa, lakini si linatakiwa lijadiliwe kiamani, kila mwenye hoja aiseme hoja yake bila jazba wala uchochezi au kuomesha chuki kwa wengine?

Au wewe unaridhika na lugha za uchokozi (provoking) zinazowachiwa kutumika hivi sasa?
ukiambiwa ukweli wazanzibari wanaiuza Tanganyika,huo ni uchokozi.

ukweli unakwaida ya kuuma.Hiyo ni dawa wacha iwaingie!
 
we

we una maslahi yako binafsi na hiyo bandari? Maana umeng'ang'ani neno maslahi, utayapata kwa kupost matusi? Maana thread inahusu matumizi ya matusi, kingine hujaambiwa serikali imesitisha mipango yake ya kuendelea kukodisha uendeshaji wa bandari sasa hayo matusi yenu yanawasaidia nini. Tumia akili kufikiri badala ya makalio
Umesoma matusi humu???
Hewa tu na wewe..
 
Uliona kuna mtu au chombo chochote kimemzuia yoyote kutoa maoni? Lakini kutoa maoni kwa njia ya matusi, kejeli kwa viongozi, dharau hiyo si njia sahihi za kutoa maoni. Kumbuka inapoishia haki yako ya kutoa maoni ndipo inapoanzia haki ya mwingine.
ungeanza na sheikh ubwabwa Mwaipopo anayemtukana nguli wa sheri Tanzania na dunia kwa ujumla,Emeritus Prof.Shivji.
 
Ukiona hao uliowataja mawaziri wamekaa kimya ujue kweli nchi imeuzwa na hao mawaziri wameungana na wazalendo wenzao kupinga huo uuzwaji wa maliasili za tanganyika na hawa wanzabibari wala urojo
 
Samia kaingiaje hapa. Inaonyesha huyo ndiye target wala si bandari na kwa bahati nzuri mama wa watu kapiga kimyaaa, mnazidi kuumia. Mnatamani awajibu lakini ndo kwanza anaendelea na yake.
atajibu tu moshi ushafukizwa shimoni,nguruwe lazima atoke.
 
Host Governmental agreement zina ukomo kwani ni mikataba ya utendaji kati ya wawekezaji na wazalendo.

Inter Governmental agreement iliyopelekwa bungeni haina ukomo lakini ile ni framework tu ya mkataba wa HGA unaotumika kibiashara.
Hatutaki, uwe ni uwekezaji , makubaliano ya kudumu hatutaki
 
Ni wapi ulipoona kuwa bandari inabifsishwa? Unajuwa labda wenzetu mna habari ambazo sisi hatuzielewi. Nini kilichokupelekea kusema bandari inabinafsishwa? Mimi sijaona wala sijasikia bandari yetu au etu kubinafsishwa.


Mimi nnachokielewa kuna kampuni inaitwa TICTS ilipewa mkataba kuendesha bandari ya makontena, lakini kwa miaka 22 haijafikia malengo na haijaleta vifaa ilivyosema italeta kuendeshea bandari kiufanisi, wakaambiwa waondoke, wameondoka sasa inataka kupewa kampuni ya DP World inayomilikiwa na Dubai ili waendeshe bandari yetu kwa mkataba ambao bado wanaelewana wataouingia baina ya DP World Na Tanzania Ports Authority.

Huko kubinafsishwa kuko wapi?
Tushamwambia Samia kuwa hatutaki mkataba wake wa KIMANGUNGO na Waarabu kama anawapenda sana akawauzie mji mkongwe.
 
Back
Top Bottom