Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

Hivi unaongelea mkataba upi na DP EWorld? Una makubaliano yoyote na DP World?

Makubaliano niliyoyaona mimi yaliyopitishwa na bunge letu yanasema wazi serikali ya Dubai itapofikia utendaji wa kuboresha bandari lazima kuwe na mikataba.

Hiyo mikataba ndiyo bado. Au kama ipo tayari, mimi binagfsi sijaiona, mwenzetu umeiona utuoneshe na sisi?
 
Ishu ni mtuonyeshe tunapata faida kiasi gani kwenye huo mkataba na ukomo wake ni lini na nini kitafanyika endapo hawata deliver accordingly.
Ukiona mtu yoyote anauliza juu ya ukomo wa mkataba wa Bandari, basi anza ku question elimu yake na uelewa wake. Hivyo tu mkuu.
 
..heshima isiwe kwa viongozi wa Ccm na serikali peke yao.

..viongozi wa vyama vya upinzani nao ni binadamu na wanastahili kuheshimiwa.
Na sisi wazee wa kawaida tunastahili kuheshimiwa pia sio Chama kinatuma vijana wao kutukashifu kwa sababu tu za kutofautiana kimtazamo !!
 
Na sisi wazee wa kawaida tunastahili kuheshimiwa pia sio Chama kinatuma vijana wao kutukashifu kwa sababu tu za kutofautiana kimtazamo !!

..kila mtu anastahili heshima.

..pia viongozi wakifanya madudu wasitarajie kuambiwa kwa lugha za kubembelezwa.

..viongozi wawe na vifua vya kusikia ukweli na hisia za wananchi.

..hiki ambacho Samia anakiona ni matusi ndio hisia za wananchi kuhusu mkataba wa bandari.

..badala ya kuwalaumu wakosoaji Samia awashukie wasaidizi wake waliomuingiza ktk mkenge wa kusaini mkataba wa hovyo na DP World.

..pia Samia awakataze wahuni kama Steve Nyerere, Zembwela, Haji Manara, Sheikh Mwaipopo, Baba Levo,kuwa wasemaji wake kuhusu mkataba wa bandari.
 
Kwanini bandari za zanzibar hazijajumuishwa kwenye mauzo kwa waarabu?
Kwanini zimeuzwa za Tanganyika tuu?
 
Kweli, mama aendelee kuw mpole awaachie vijana waliwekwa kulinda usalama wa gtaifa letu waondo hivi vyanzo vya chokocoko.


Tuliiona migoma ilikuwa inasabisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia, kuna mtu mmoja tu akatiwa adabu, mpaka leo hatujasikia mgomo Hospitali.

Watu wanafikiri katiba imebadilika au system imebadilika?

CCM ni ile ile.
 
Amekosea imeporwa na wazanzubari na kupewa waarabu bure bure
 
lazima sheria zitumike. Mbona wakati wa Magufuli ndio ilisainiwa MoU ya kwanza baina ta Dubai na Tanzania na hatukuona yeyote aliyesema chochote?
Mou gani hiyo weka hapa acheni uongo nyie waunguja?
 
Kwa kifupi pande mbili ambazo hazikuwa zikimuelewa Magufuli sasa hivi zinakubaliana nae kimya kimya kwa mitazamo tofauti.

Wale wanaosema sasa hivi hakuna wazalendo wanakubali alikuwa sahihi kwenye ulinzi wa rasimali za nchi.

Wale waliokuwa wanasema anaua demokrasia sasa hivi wanakubali lazima kuwe na mipaka vinginevyo ni hatari.

Hizo njia zote tulishapita kuanzia 1985-2015, ndipo Magufuli na team yake wakaona inatosha kucheka na wapuuzi.

Ukitaka maendeleo kuna watu watakutakana na kuzusha uongo kama wanaopinga bandari kwa sababu ya maslahi yao either ya kifisadi au maslahi ya kisiasa (political mileage).

Hapo kwenye maslahi ya kisiasa utaambiwa wewe ndio mnufaika mwenyewe, utatukanwa na kuzushiwa uongo, watu watatumia hiyo nafasi kutaka kuhamasisha serikali isiheshimike.

Haya ni marudio tu, vyama vya siasa avikumuelewa Magufuli; ilikuwa ni kumaliza upumbavu huu. Rasimali za Tanzania ni kwa maendeleo ya taifa sio kundi la watu.

Na siasa sio mahala pa kutunga uongo na kuhamasisha kuto heshimu mamlaka.

Kazi ngumu ni kuwabadili hawa watu tabia mafisadi za ujambazi na wanasiasa waliozoea kufanya siasa za hovyo.

Hii nchi bado kuwa na raisi lege lege, atafutwe Magufuli mwingine. Tukiona anatosha katiba ibadilishwe aongezewe muda mpaka hayanyooshe haya makundi mawili ya mafisadi na wana siasa wenye viwanda vya uongo. Haya makundi mawili ni kikwazo kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi Tanzania.

R.I.P mwamba
 
Hapa utajionea kijana Mzanzibari na Mzee wa Dar Es Salaam Wakijadili bila jazba wala kejeli kwa yeyote:

Nyie wazanzibar hamna haki yeyote kwenye bandari ya Dar kama mna haki kwanini bandari zetu hamkuziuza mazima nyie waunguja?
 
Kwel kbs Leo umeongea point ya msingi Kwa kuanza serikali ianze na wapumbavu wawili humu wanaoeneza chuki za kidini humu Kuna mzee Moja na bibi flan ambae hafai hata kua mshangazi
Hao ni kina bibi Faiza na babu The boss wao wanafikiri kwenye uislam zaidi kuliko hoja….,

Wao kila mwarabu wanaona ni ndugu yao wako radhi tumpe kila kitu
 
umesema ukweli, yeyote anayependa amani, ustaarabu, kuheshimiana, umoja wa kitaifa atakuunga mkono. Hata mi najiuliza, hivi mbona km nchi imesimama? Hao mawaziri kweli wako wapi, waziri wa habari, waziri wa mambo ya ndani ya nchi, waziri wa katiba na sheria, au Rais kawazuia kutekeleza majukumu yao? KM ndivyo basi rais afanye kazi mwenyewe hakuna haja ya kuwa na mawaziri. Mi nna wasiwasi huyu rais wetu km ana kibri hashauriki, ila ajue yakitoke yakutokea lawama zote atabeba yeye hakuna mwingine. TCRA wako wapi ni km kuna maelekezo kutoka juu kuwa waacheni msiwabughudi. Maana matusi, lugha za chuki, lugha za ubaguzi zilizopo katika mitandao inatisha na kuogopesha. Makamu wa Rais yeye yuko wilayani kwake Buhigwe wiki nzima km tu Magufulli na Chato yake. Kuna mbegu imepandwa ndani ya nchi hii ya kibaguzi sijui siku ikiiva hayo mavuno yatakuwa ya aina gani.
 
ki
Kila mtu ana jambo lake ki maslahi, likiguswa atalalamika.

Jambo la DP World lina maslahi pande tofauti. Kila upande usikilizwe.

Hakuna kuona hawa ni hawa, wale ni wale..
kila mtu km nani, sisi tunaangalia maslahi ya Taifa hakuna maslahi ya mtu hapa na serikali ndiyo tumeikabidhi kusimamia maslahi ya Taifa.
 
Wakati tunapoteza muda kubishana na kuonyeshana ujuaji wa vifungu vya sheria huko Rwanda na Congo wameshasainishana na mwekezaji na shughuli za kiuchumi zinaendelea.
Ukiweka hapa mikataba ya uwekezaji ya huko Rwanda na Congo, naamini hoja yako ingekuwa na nguvu. La, ni hisia potofu
 
Tulia wewe mmejichanganya wenyewe wazanzibari hatukubali muuze mali na rasimali zetu tukae kimya nyooooo…..
Tulieni dawa iwaingie hata mkiamua kufanya lolote hatutaacha kusrma
 
Mawaziri wana mamlaka gani ya kisheria mpaka useme wachukue hatua? Pili wewe ndiye mchokozi na wakienda mahakamani hao mawaziri tutawashinda na ndipo tutauweka wazi upumbavu na mama yenu mliofanya huko na waarabu. Halafu tusitishane
 
Tatizo kinachokusumbua wewe mtoto kila siku huwa nakuambia usipoacha utateseka sana...mbona haukuyaongea haya Zito kabwe, kinana pamoja na january makamba walipokimuandama magufuli kila kukicha? Au ndio yale ya muislamu hakosei bali anaonewa?
Tukumbushe kidogo tuone lugha walizotumia kufikisha ujumbe wao.

Hao wote unaowataja mimi nafahamu kuwa ni watu wa system. Waarabu wa pemba wajuana kwa vilemba.
 
we
Watetezi wa maslahi wasikilizwe, mambo yarekebishwe na Wananchi waridhike na makubaliano ya uwekezaji, Huwezi kufanya uwekesaji nchini bila wananchi kuelewa.
we una maslahi yako binafsi na hiyo bandari? Maana umeng'ang'ani neno maslahi, utayapata kwa kupost matusi? Maana thread inahusu matumizi ya matusi, kingine hujaambiwa serikali imesitisha mipango yake ya kuendelea kukodisha uendeshaji wa bandari sasa hayo matusi yenu yanawasaidia nini. Tumia akili kufikiri badala ya makalio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…