Uhuru wa maoni uwe na mipaka. Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni uchokozi

FaizaFoxy silu hizi umekuwa mtetezi wa mafisadi sana sijui kwanini.

Kipindi cha Magufuli ilikuwa hata likifanywa jambo zuri bado ungepinga na kulaani, ila leo hii unawapapatikia Waarabu sana! Tumejua rangi yako halisi
 
Tatizo lililopo ni kuwa ukitoa maoni ambayo yapo kinyume na watawala huwezi kuwa salama.

Wewe tu binafsi mtu akiwa na mtazamo tofauti na wewe huwa unang'aka balaa.
 
We ndio usiongee kabisa maana RIP Magufuli mlimtukana na kumwita majina yote ya hovyo alipokaza mkasema anaminya demokrasia.
 
Kilichoridhiwa na bunge la Tanzania kuhusu DP World ni nini?
Mimi sijakiona, mimi nilichokion akilichoridhiwa na biunge ni hiki hapa:
MAKUBALIANO YA KISERIKALI KATI YA:

ΤHΕ UNITED REPUBLIC 0F TANZANIA

AND
THE EMIRATE 0F DUBAI
Bofya chini hapa utaukuta makubaliano kamili yametafsiriwa kwa Kiswahili:
 
FaizaFoxy silu hizi umekuwa mtetezi wa mafisadi sana sijui kwanini.

Kipindi cha Magufuli ilikuwa hata likifanywa jambo zuri bado ungepinga na kulaani, ila leo hii unawapapatikia Waarabu sana! Tumejua rangi yako halisi
Mnafiki mkubwa huyo, sahizi kwa mkojani mwenzie anaona hewala kila afanyalo hewalaa.
 
Kama hawataki kukejeliwa au kutusiwa waache kuwakejeli au kuwatusi watanzania kwa kuongoza vibaya kwa mfano kuingia mikataba mibovu.sio wao tu hata machawa wao kama wewe watakejeliwa wenyewe wakiwakejeli watanzania.
Wanafosi nyekundu kuwa kijani halafu wanategemea watu watakaa kimya tu. Theres something fishy 🤣
 
Umeongea kwa busara sana, hakuna shida kukosoana hilo mimi halinipi shida ni kawaida tu lakini usituhumu mtu jambo huna ushahidi nalo, usitukane taasisi kama ya Rais ila toa hoja yako na watu watakuelewa tu. Serikali lazima iweke mipaka na jukumu kubwa kulinda usalama wa Taifa kuepuka kauli za kichochezi ila mambo ya hoja, sera mtu aongee tu uhuru wake. Hoja ijibiwe na hoja ila matusi kwa mtu yoyote na hasa viongozi hapana hili tusiliache ni hatari sana.
 
Tatizo lililopo ni kuwa ukitoa maoni ambayo yapo kinyume na watawala huwezi kuwa salama.

Wewe tu binafsi mtu akiwa na mtazamo tofauti na wewe huwa unang'aka balaa.
Sasa ndiyo tutukane, kwa saabu ukiniktukana na mimi sitokubali ntakutukana, itakuwa tumeuwasha moto ambao kuuzima kwake inakuwa shida. Ndiyo maana nikaleta mada hii, serikali itusaidie huko nje, watu wachukuliwe wakasikilizwe kisheria badala ya kujaza wengine chuki.

Na pia tunahitaji hapa JF uongozi (moderators) wa JF wawe makini kutazama mipaka ya uhuru wa moni iwe ni mimi au mwengine yeyote, wafute posts, mbona kuna nyuzi ambazo wanaona zinaweza kuleta tabu wanazifuta?

Naamini Uhuru wa kujieleza una mipaka yake kisheria.
 
Uliona kuna mtu au chombo chochote kimemzuia yoyote kutoa maoni? Lakini kutoa maoni kwa njia ya matusi, kejeli kwa viongozi, dharau hiyo si njia sahihi za kutoa maoni. Kumbuka inapoishia haki yako ya kutoa maoni ndipo inapoanzia haki ya mwingine.
Na ikumbukwe maoni yoyote yatakayotolewa dhidi yako huwa sio lazima yawe ya kukusifu. Hata ya kukuvua nguo pia ni maoni vile vile.
 
Meshindwa hoja mmeanza kuita mahakamaCCM na mapoliCCM. Hoja hujibiwa Kwa hoja siyo Kwa Virungu
 
Ukiacha umalaya utafika mbali, kwa upumbavu huu nazidi kukuona taahira. Kwani mkijibu hoja mtapungukiwa nini? Acheni vitisho, hii nchi sio ya mamako na babako, ni ya kwetu sote!
 
Serikali ipi hio? 🤣 Huo utakuwa udikteta ule ule ambao mlimvalisha hayati Magufuli kwa chuki zenu. Mtu anapanga mipango mizuri linatokea kundi la watu linaanza kuropoka na kumdhihaki raisi ili kutafta sifa na kuvuruga utulivu. Walipoanza kuchukuliwa hatua ikaonekana raisi ameleta udikteta. It started in the same manner.
 
Hahahahahaha bi Mkubwa hapa ndo ataelewa kwa nn Mjomba mwendazake alipiga marufuku siasa baada ya uchaguzi
 
Watanzania tuna shida kubwa sana ya kujitafutia huzuni, chuki, hasira na uzandiki

Hadi sasa kuna baadhi ya kauli zinatolewa na viongozi hasa wa dini moja zikionyesha chuki mbaya sana mioyoni kwao… na to some extent zile chuki z inaonyesha hasira zao Kwa Mungu kuliko hata walengwa wa hapa duniani

TumeshasahAu all the fears and victimization zilizokuwepo

Tumeshaanza nchi lazima iende kisasa….

Acha tuonyeshe unafiq wetu…. ILA tusisahau siera Leone was once peaceful kama Tanzania

Nani anayefadhili chuki hizi?
 
Hahahah naona akili zimeanza kukurudia chawa mwandamizi. 🤣Maana ulikuwaga mtu wa kumdiss sana JPM.

Kinachotokea sasa ndio kile kile ambacho kilitokeaga kwa JPM na protestants ambao walikuwa wanamkejeli na kumdhihaki kwamba ni raisi mshamba 🤣!!! Kila alichokuwa anaplan kufanya mizozo ikawa mingi hadi alipoamua ku deal na hao wahuni. Kama malalamiko yalikuwa ni kuminywa kwa demokrasia na uhuru wa maoni naomba tusirudi kule.

Watu wawe na uhuru tu wa kuropoka na kusema wanachojiskia tusileteane habari za mahakamani sababu mama alikuwa ni msikivu ila juzi amesema ameziba masikio. Kwahio acheni watu waendelee kumzibua maskio.
 
kuna watu hawataki amani wanachochote vita,kuna watu wanataka utawala kwa njia za hadaa na uongo na watafanya uovu wa hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…