Uhusiano wa Intelijensia na watu kama kina James Bond

Uhusiano wa Intelijensia na watu kama kina James Bond

Hapa kidogo mkuu nimeanza kukuelewa

Uimara wa TISS unakuja katika dhana na sera yake ya kimgawanyo, yaani mpaka vijijini kuna mawakala wa TISS!
Rejea simulizi za jaribio la kutaka kuangusha serikali ya Mwalimu Nyerere!

Ipo hapa thread itafute!
 
Uimara wa TISS unakuja katika dhana na sera yake ya kimgawanyo, yaani mpaka vijijini kuna mawakala wa TISS!
Rejea simulizi za jaribio la kutaka kuangusha serikali ya Mwalimu Nyerere!

Ipo hapa thread itafute!

Nimeshaiona hiyo thread ila kuna hoja hapa hapa mkuu kuna watu wanasema Tiss ilikuwa ya nyerere tu hii ya sasa hivi ni dhaifu
 
Wapo mkuu, tena wamefundwa zaidi ya uonapo movie hizo!

Unapoona tukio lolote la kifisadi au vyovyote vile limewafikia Chadema au mbunge yeyote jua kuwa limetokea TISS!

Hakuna kitu ndani ya nchi hii kinachoweza kutokea bila TISS kujua!

Tatizo ni watawala, TISS wakishamaliza uchunguzi unaoonyesha kuwa kuna tukio linakuja au lipo wao hupeleka file mahali husika huko ndiko hupewa amri na maelekezo ya nini wafanye!

Jidanganye kuwa hawapo ulijua jiji mkuu!

Tanzania ndio nchi inayoongoza kwakuwa na Usalama wa Taifa imara kuliko nchi yoyote Afrika!

ngudu, TISS hawajafundwa kokote, ni mbovu kulko zote afrika, kwa mfano issue ya ULI, kama mtu anakwenda kum-assasinate mtu halafu katika zoezi hilo anatumia simu kumpigia mhusika na rekodi zote za sms zinabaki kwenye simu, then intelligence ipo wapi, walishindwa kuwa na special access kwenye mitanao ya simu ili kufanya shughuli zao bila kujulikana?

TISS ipo chini ya ofisi ya rais , kitengo cha utawala bora, unategeme kuwa na GHOST agent wakati una ma-assisin uchwara?
 
Uimara wa TISS unakuja katika dhana na sera yake ya kimgawanyo, yaani mpaka vijijini kuna mawakala wa TISS!
Rejea simulizi za jaribio la kutaka kuangusha serikali ya Mwalimu Nyerere!

Ipo hapa thread itafute!

Je hao wamakala wao wamefanya nini kudhibiti ufasadi katika ardhi za vijiji zinazovamiwa na wawekezaji wababaishaji?
TISS hana nguvu tena kama zamani,

na tumisikia wapo kila taasisi na mashirika ya umma, je walisaidiaje taifa hili katika uvumbua ubadhirifu, wizi, ufisadi, na ughaidi ? HAKUNA KITU!

WAZO binafsi

1. TISS iwe Taasisi Independent, yaani isiwe chini ya ofisi ya Rais.
2.TISS ipewe mamlaka ya kukamata,kuhoji, kuweka kizuizini yeyote kwa maslahi na usalama wa taifa,
3. TISS ipadilishwe jina iitwe TISA, yaani TANZANIA INTELEGENCE AND SECURITY AUTHORITY, kwa kiswahili, MAMLAKA YA INTELEJENSIA NA USALAMA YA TANZANIA.
4. Kuwe na vitengo vikuu viwili yaani INTELEGENCE na SECURITY.


LIST ITAENDELEA BAADAEE...
 
Majubu ni ndiyo,ndiyo,kwa maswali yako yote. TISS imekuwa trained na MOSSAD[Israel Intelligence Agency]

WALIKOkuwa trained na MOSSAD ni kizazi yaani rika la 1935, hawa watu walifundishwa URUSI, Israel, China, Cuba, UK.leo hii wengi wame staafu au wamefariki, sasa kizazi cha uhuru yaani 1960 wamefundishwa kule KUNDUCHI, je katika ulimwengu wa utandawazi utaweza kuwa na ujuzi wa kiintelenjinsia wa kisasa? TAFAKARI.
 
MKUU, NIMEKUKUBALI KATIKA KUANGALIA NA KUPAMBANUA FILAMU ZA KI-INTELEGENCE, Watengenezaji wa filamu hizi huwa na wanaeleza kila kitu wazi, lakini kwa mgongo wa FICTION yaani si mambo ya kweli, lakini ukweli ni ya kweli,.

WATANZANIA wengi bado ni Mambumbu hawaelewi, wazungu wanaweka ukweli kwenye filamu.
 
TISS ilikuwa zamani enzi za Nyerere,siku hizi wamejazana ndugu watoto wa shangazi na mjomba hakuna uwajibikaji wapo kama hawapo,uwezo wao wa kukusanya taarifa ni mdogo.

Vijana wachapakazi wenye fani mbalimbali hawapewi nafasi.

Wanakomoana na kupeana adhabu kwa makosa yasiyo na kichwa wala miguu
 
Aisee,

Ukiondoa Kiswahili, Kuondoa Udini na Ukabila. Mwalimu JKN aliweka TISS nzuri sana.

TISS ya Apson ndo ilikua na nguvu sana. Ila naamini bado wapo fresh tu.

Naweza kusema hawawezi kufikia uwezo wa "James Bond", sio kwa Tanzania kwa sababu hatuhitaji mtu kama James Bond!

Kwanza tatizo ni VIFAA, sio mafunzo.

Epa au hela za Uswisi wanazijua kama wapo smart. Mie ningekua Mkuu wa TISS ningekua na recruit first class students tu na second upper za juu.

Ila TISS yetu wapo watoto wa Dk Omar (RIP), fulani fulani. Sio who knows How ni who knows WHO!
 
Wapo mkuu, tena wamefundwa zaidi ya uonapo movie hizo!

Unapoona tukio lolote la kifisadi au vyovyote vile limewafikia Chadema au mbunge yeyote jua kuwa limetokea TISS!

Hakuna kitu ndani ya nchi hii kinachoweza kutokea bila TISS kujua!

Tatizo ni watawala, TISS wakishamaliza uchunguzi unaoonyesha kuwa kuna tukio linakuja au lipo wao hupeleka file mahali husika huko ndiko hupewa amri na maelekezo ya nini wafanye!

Jidanganye kuwa hawapo ulijua jiji mkuu!

Tanzania ndio nchi inayoongoza kwakuwa na Usalama wa Taifa imara kuliko nchi yoyote Afrika!
HAWA ghost/assets wapo tena wana uzalendo uliopea. Ila wao sio decission makers wa yale wayaonayo. CCM ya kuanzia Mwinyi imechakachua na kuwafanya wajione hawana maana. Kutokana na hilo, wamegeukia upande mwingine ambao wanaona watathaminiwa wao na kazi zao.
Kelele zote za CDM na magazeti kama "Mwanahalisi, Jamhuri, Dira" nk kwa kiasi kikubwa zinatokana na uzalendo wa hawa ghosts/assets wetu hapa Tanzania ndani ya TISS. Na ikitokea nchi hii ikapata chama mbadala wa CCM ndipo utaona ni kwa jinsi gani ghosts/assets wetu wanavyoipaisha nchi hii na raia wake kufikia maendeleo yaliyotukuka kwa chunguzi na tafiti zao za kimaendeleo katika kila sekta.
 
mimi nadhani usalama wa taifa ulipaswa uwe kama division, yaani bos wake anao uwezo wa kuchimba biti mpaka mkuu wa nchi.
 
Hivi mnaoongelea usalama wa taifa wa Tanzania mnaufahamu au hisia tu. Maana sioni mtu anayetoa point ya maana. Kila mmoja anahisi hisi tuuuu. eti enzi za...
Waacheni usalama wa taifa wafanye kazi zao. Nyie tulieni mlindwe.
Wanapata mafunzo mbali mbali duniani.
Na ifahamike Tanzania iko duniani haipo kwenye sayari nyingine.
 
Wakuu habari zenu,

Mimi nikiwa sina kazi siku za wikiendi huwa napenda sana kwenda movie na vijana wangu juzi kati nilikuwa mmoja ya watu n waliokuwapo katika kuangalia movie mpya ya Skyfall iliyochezwa na James Bond kwa udhamini wa heineken movie ilikuwa ni nzuri ila katika kuangalia nikapata wazo ambalo kidogo nikaona sio haba kuja kushare na nyinyi hapa

Daniel Craig aliyecheza kama James Bond anaonekana anafuatilia hardware fulani ya siri na hiyo hardware inatumika katika ku hack system za mi6 na kuuwa baadhi ya agents wa mi6 nilipenda jinsi jamaa alivyokuwa anaunganisha upelelezi wake jamaa alikuwa yuko fiti katika vitu vifuatavyo anatumia systema as fighting combat style yake systema kwa wasiofahamu ni ni aina ya russia martial arts training includes but not limited to hand to hand combat, grappling, knife fighting and fire arms training as well.

Training involves drills and sparring without set kata

Pili ana 'iq' kubwa


pia ni mtaalamu wa computer, (naposema computer namaanisha ku hack sio kutumia microsoft words na kuingia facebook na jf)
magari na ni mtumiaji mzuri wa silaha bila kusahau gadgets mbali mbali anazotengenezewa na q.

Sasa swali langu ni hili;

Mi6 kama Mi6 naamini wana watu wa aina ya Bond people who do not exist ila wapo katika mi6 wanakuwa wanajulikana na watu wachache sana kama m, q na moneypenny. sawa ni movie ila ni movie iliyo reflect mazingira halisi ya mi6

suali langu ni kwamba je TISS inazalisha na kutengeneza watu kama bond watu ambao wako fiti katika kila kitu kuanzia uwezo wa kupigana , utumiaji wa silaha, iq na masuala ya gadgets ?

Tiss wana watu ambao they dont exist? Watu ambao kwa lugja ya kiiteligensia wanaitwa "ghosts"

watu ambao wako mbele katika kuhakikisha usalama wa nchi na mustakaballi wa nchi unalindwa


sidhani kama wapo (kwanini sidhani)

1.suala la epa "ghosts" walitakiwa wawe wamelijua since the first time sio linakuja kuibuliwa na wabunge
2. Wizi wa raslimali kama madini, twiga nk "ghosts" walitakiwa wawe na data zote na wawe wamelizuia siku nyingi sio kuja kuibuliwa na wanasiasa
3. Suala la rada n.k ni lazima wawe mstari wa mbele katika kulinda mustakaballi wa tiss kwani kitu kikiibuliwa na wabunge watu wataulizana tiss wako wapi??


Kama haipo iundwe
undeni "ghosts" people they dont exists
people who the dont have restrictions we know mna assasins but assasin sio "ghosts"

wenzenu wa marekani ana watu wanawaita "assets" hawa ndio kama ma ghosts wa mi6
Niliipenda sana hii kazi lakini sikujua naipataje
 
Nani kakwambia hatuna ghosts? Waliomtesa dr. Uli wasingekuwa ghosts wangesha patikana.
wale sio ghosts. ghosts they dont leave the footprints cause they dont exist. sio kama hawa waliomtesa ulimboka mpaka namba zao za simu zimepatikana.
 
ndugu hebu nisaidie kunitofautishia hao ghost na agent
Ndio hicho nilichokuwa nakisema mkuu kuna tofauti kati ya "Ghosts" na agents wa kawaida kuanzia nyumba wanayopewa, magari wanayopewa na mishahara "Ghosts" au "Assets" ni tofauti sana na ma agents wa kawaida unaopishana nao barabarani na kunywa pombe na wanaovaa kaunda suti..
 
inapopiga twanga ndio huwa nasikiliza wanaotaka kuangusha system:becky::becky::becky::becky::majani7::majani7::majani7:

TrojaN
kama ukisoma post yangu vizuri utaelewa ila kwa ufafanuzi zaidi ni hivi
agent wa kawaida au officer ni yule mfanyakazi wa secret agency yeyote ambaye kapata mafunzo yote as agent na anajulikana na timu nzima ya agency na anakuwa na id ambayo iko kwenye database ya agency mfano agent trojan mwenye id namba 52684 ambapo wewe agent as agent unakuwa unafanya kazi ambazo unapangiwa na department yako na unakuwa ume specialise katika kazi stahiki ya department hiyo
mfano wewe ni IT basi utakuwa katika agency hiyo umeajiriwa katika department ya it na kazi yako itakuwa ni It na utakuwa ni mtata sana katika maeneo hayo, kama wewe ni udereva basi utaspecialise katika udereva na utakuwa ni mtata sana kwenye udereva, kama ni upelelezi basi wewe ni mtata kwenye upelelezi, muajiriwa wa agency katika sekta ya upelelezi na kazi yako ni kufuatana na taratibu na sheria pamoja na policy za agency na details zako zote zitakuwa ndani ya agency na sawa watu wengine wanaweza wasikujue ila ni lazima utajulikana na ma agent wenzako wa pale pale kwenye agency kwani aina ya magari unayotumia yatakuwa ya ofisini, (yanayojulikana) hapa kwetu zamani ilikuwa pajero sasa hivi ni nissan na rav 4, u.s ni gmc na chevroret , aina ya uvaaji (suti za kaunda suti)

GHOSTS
hawa ni aina ya ma agents ambao kwanza wamepitia mafunzo yote ambayo hawa ma agent wote wamepitia
ILA mafunzo yao yanakuwa ni tofauti kuanzia na recruitment hawa base wanayotumia katika mafunzo ni tofauti sio sawa na hawa ma agent wa kawaida (base ambayo it doesnt exist)
budget yao hawa majamaa katika mafunzo sio bajeti ya kitoto
salary zao nyumba zao wanazokaa na magari wanaoendesha sio ya kitoto hata bosi wa department zingine za agency hizo hawafikii

wako under the departmnet which it doesnt exist
sio kila mtu wa ndani ya agency anaijui department ambayo hawa ghosts wako ambao kwa marekani wanaitwa (ASSETS)
hii ni list ambayo inaweza jua existence ya GHOST/ASSETS
president, mkuu wa agency, mkuu wa department ya ghosts na shadows pamoja na real Ghosts

shadows ni akina nani?
shadows ni ma agent ambao wanampa support Ghosts katika kufanikisha mission zake katika sekta ya usafiri, It, pesa, na accomodation
hawa wahajuani na Ghosts na ghosts hawawajui shadows arrangement inafanywa na department ya Ghost mfano narudia tena huu ni mfano tu
Ghost anatakiwa akafanye mission kigoma anaambiwa atoke mjini kariakoo (ofisi yake ilipo) mpaka mbezi pale mbezi atakutana na shadow anampa gari na funguo likiwa na mafuta anamwambia atapandia ndege arusha so anaendesha gari mpaka arusha akifika arusha atakutana na shadow huyu ndio anayempa tiketi ya ndege usishangae shadow akawa ni mfanyakazi wa ndege(mjaza mafuta) ataenda mpaka kigoma kule atafika kwenye hoteli ambayo imeshalipiwa kila kitu aliyelipa anaweza kuwa ni mwanamke na atajifanya kuwa yule ghost ni mpenzi wake na watalala wote chumba kile na watafanya mapenzi (yule mwanamke ni shadow) kesho watatoka hotelini wataenda kwenye mission wanaweza ingia kwenye mission as couples (ghost na shadow) shadow anakuwa kama ni backup ya ghost katika mission
watafanya mission yao ambayo inaweza kuwa aidha ni kukusanya data, au ni ku attack au ku defence inategemea na mission

hii mission agency inakuwa haijui chochote ila iko chini ya department ya Ghosts
Raisi, mkuu wa idara na mkuu wa agency na Ghosts na shadows tu ndio wanaojua hii inshu

ma agent wengine wanaweza wakawa hawajui chochote kinachoendelea na hawajui kuwa kuna hii department katika agency yao hata makamu wa raisi mwenyewe anakuwa hajui

na hiyo ndio tofauti kati ya ma agent na ghosts
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom