Hili pia kwetu lipo ,, lakini toka nimejitambua najaribu kuli balance
Mimi upande wa baba ni hapa hapa mkoa ninao ishi ,, nauli toka ninapoishi mpaka kijijini kwa baba ni sh 7000/= tu ,,, lakini mara ya mwisho kukanyaga huko ilikuwa ni mwaka 2004 ,, yani nikiwa darasa la nne ..
Kwa kweli nilikaa chini na kutafakari juu ya hili na kuamua kuchukua hatua ,, hapa naandika nilikuwa kijijini kwa mzee (baba) kwa siku tatu ..Siku namwambia bibi yangu mzaa Baba nipo njiani nakuja kwa njia ya simu
Bibi yangu alifurahi sana nilitoka nyumbani saa tatu na nusu usiku kwa pikipiki (bodaboda) ambako ingenichukua masaa mawili mpaka matatu tu kufika huko ,,, kwa kawaida Bibi yangu huwa analala saa 3 usiku ,, lakini siku hiyo aliniambia sitolala mpaka ufike ,, nilifika kijijini saa tano na nusu usiku na nilikumkuta bibi yangu akiwa macho ananisubilia hakika alifurahi sana kuniona alinikumbatia na kubusu viganja vangu hakika nilijisikia vizuri kumuona tena bibi yangu lakin pia nilihisi uchungu kwa jinsi bibi yangu alivyokuwa anaonesha kuumia kwa kitendo cha sisi wajukuuu wake kutotaka kwenda kumsalimia kwani niliona ni jinsi gani bibi alikuwa anapenda mimi niende kumsalimia kijijini lakani mimi nikawa tu mkaidi ,, bibi aliniambia "nilidhani utakuja tu siku tu utakayosikia nimekufa kumbe sikuwa sahihi karibu sana mjukuu wangu karibu nyumbani karibu katika ardhi ya babu na babu zako"
Bibi yangu kwasasa anamiaka miaka 70 anatembea kwa tabu sana lakini kesho yake alinitembeza mpaka eneo ambalo babu zangu na ndugu zangu wengine wamezikwa ,, kikubwa kilichonishangaza hapa ni uwezo mkubwa alionao bibi yangu katika kumbukumbu alizonazo juu ya watu wale muhimu katika historia ya ukoo wetu alinionesha moja mpaka jingine ( maana mahali pale wanezikwa watu tofauti tofauti wa kijijini pale ) na kunielezea mahusiano yetu yakoje na watu wale ..
Baada ya zoezi lile ilinibidi nichukue namba za ndugu zangu wengine kwa ajili ya kujenga uhisiano wetu kwa upya .. hakika niliona jinsi gani nilikuwa nakosea na kwasasa nimeapa nitajitahidi kila mwezi niwe naenda kumsalimia bibi yangu na ndugu wengine kule kijijini
Kwanini niliamua kukaa mbali na ndugu wa upande wa baba
Hii ilitoka na kuona hawana msaada kwangu ,,, wao walikuwa wanaongea pindi tu napokesea shangazi zangu walikuwa wkionesh waziwazi kunitenga hii ilitokana na mama yangu kuwa mtu wa kabila tofuti na kabila la baba yangu
Hali hii ilileta tabaka kubwa katika yangu na hawa ndugu zangu maana niliona kama wanamchukia na kumsemea vibaya mama yangu hivyo niliamua kukaa nao mbalii
Nataka niwe na mahusiano yenye nguvu na hawa ndugu zangu maana najua hawa ndiyo watako nizika siku moja au mimi ndiyo nikawazika wao hivyo hamna haja ya kuendelea kuishi kwa mfumo huu wa kukaliana kimya