Uhusiano wako na ndugu zako wa baba upo sawa ?

Uhusiano wako na ndugu zako wa baba upo sawa ?

Endeleeni, wengine tunasoma watu na ndugu zenu...
Tresor Mandala pole sana kaka.
Nuzulati hiyo ya Ubaya Ubwela nimeilewa ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
kwa kweli mimi kwa sasa sitaki tukutane kwenye msiba au sherehe eti nielekezwe โ€œMimi unanijua,Mi mjomba wako,shangazi yako au baba yako mdogo huwa naitika kwa dharau sana.
 
Hili pia kwetu lipo ,, lakini toka nimejitambua najaribu kuli balance

Mimi upande wa baba ni hapa hapa mkoa ninao ishi ,, nauli toka ninapoishi mpaka kijijini kwa baba ni sh 7000/= tu ,,, lakini mara ya mwisho kukanyaga huko ilikuwa ni mwaka 2004 ,, yani nikiwa darasa la nne ..

Kwa kweli nilikaa chini na kutafakari juu ya hili na kuamua kuchukua hatua ,, hapa naandika nilikuwa kijijini kwa mzee (baba) kwa siku tatu ..Siku namwambia bibi yangu mzaa Baba nipo njiani nakuja kwa njia ya simu

Bibi yangu alifurahi sana nilitoka nyumbani saa tatu na nusu usiku kwa pikipiki (bodaboda) ambako ingenichukua masaa mawili mpaka matatu tu kufika huko ,,, kwa kawaida Bibi yangu huwa analala saa 3 usiku ,, lakini siku hiyo aliniambia sitolala mpaka ufike ,, nilifika kijijini saa tano na nusu usiku na nilikumkuta bibi yangu akiwa macho ananisubilia hakika alifurahi sana kuniona alinikumbatia na kubusu viganja vangu hakika nilijisikia vizuri kumuona tena bibi yangu lakin pia nilihisi uchungu kwa jinsi bibi yangu alivyokuwa anaonesha kuumia kwa kitendo cha sisi wajukuuu wake kutotaka kwenda kumsalimia kwani niliona ni jinsi gani bibi alikuwa anapenda mimi niende kumsalimia kijijini lakani mimi nikawa tu mkaidi ,, bibi aliniambia "nilidhani utakuja tu siku tu utakayosikia nimekufa kumbe sikuwa sahihi karibu sana mjukuu wangu karibu nyumbani karibu katika ardhi ya babu na babu zako"

Bibi yangu kwasasa anamiaka miaka 70 anatembea kwa tabu sana lakini kesho yake alinitembeza mpaka eneo ambalo babu zangu na ndugu zangu wengine wamezikwa ,, kikubwa kilichonishangaza hapa ni uwezo mkubwa alionao bibi yangu katika kumbukumbu alizonazo juu ya watu wale muhimu katika historia ya ukoo wetu alinionesha moja mpaka jingine ( maana mahali pale wanezikwa watu tofauti tofauti wa kijijini pale ) na kunielezea mahusiano yetu yakoje na watu wale ..

Baada ya zoezi lile ilinibidi nichukue namba za ndugu zangu wengine kwa ajili ya kujenga uhisiano wetu kwa upya .. hakika niliona jinsi gani nilikuwa nakosea na kwasasa nimeapa nitajitahidi kila mwezi niwe naenda kumsalimia bibi yangu na ndugu wengine kule kijijini


Kwanini niliamua kukaa mbali na ndugu wa upande wa baba

Hii ilitoka na kuona hawana msaada kwangu ,,, wao walikuwa wanaongea pindi tu napokesea shangazi zangu walikuwa wkionesh waziwazi kunitenga hii ilitokana na mama yangu kuwa mtu wa kabila tofuti na kabila la baba yangu

Hali hii ilileta tabaka kubwa katika yangu na hawa ndugu zangu maana niliona kama wanamchukia na kumsemea vibaya mama yangu hivyo niliamua kukaa nao mbalii

Nataka niwe na mahusiano yenye nguvu na hawa ndugu zangu maana najua hawa ndiyo watako nizika siku moja au mimi ndiyo nikawazika wao hivyo hamna haja ya kuendelea kuishi kwa mfumo huu wa kukaliana kimya
Umefanya vizuri mkuu....hivi viburi japo vya muhimu....lkn sometimes ni havitusaidii

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Pole! Ila hapa Tz watu wa kabila lako wapo wengi sana ukifanikiwa wanaweza kua ndugu zako.
Mimi mama yangu ana ndugu wengi hapa baada ya kujikuta wengi wao walipotezana na ndugu zao wa kuzaliwa hivyo wakajiunga kuunda familia kutokana na historia yao.
Mtu wa Kabila moja anaeza kuwa ndugu?
 
Tuko karibu kama chanda na Pete. Kwa baba wako zaidi ya ishirini na kitu yaani baba wakubwa, wadogo na mashangazi. Tunapendana sana, mmoja akiumwa vibaya basi lazima usikie. Kila mwaka huwa tunakutana kijijini haijalishi uko wapi lazima uje, Kijiji ghafla kinakuwa mji Kwa ujio wetu, zaidi ya watu mia mbili hufika, Kwa hili nampongeza Babu wa Babu yangu, Happiness is simple.
 
Tuko karibu kama chanda na Pete. Kwa baba wako zaidi ya ishirini na kitu yaani baba wakubwa, wadogo na mashangazi. Tunapendana sana, mmoja akiumwa vibaya basi lazima usikie. Kila mwaka huwa tunakutana kijijini haijalishi uko wapi lazima uje, Kijiji ghafla kinakuwa mji Kwa ujio wetu, zaidi ya watu mia mbili hufika, Kwa hili nampongeza Babu wa Babu yangu, Happiness is simple.
Amazing ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
 
Ni miaka mingi toka baba afariki lakini ndugu wa baba wako na Mimi na familia yetu...
Mashamba wametutunzia ziko heka 75 japo mzee aliacha 120 na wakati huo tulikuwa wadogo sioni tatizo.
Hizo heka walizochukua kila wanapolima hututumia chakula.
Tunawasiliana vizuri yaani hata kwa shida napiga cm wananipigia.

Ndugu wa mama wao mpka wawe wanataka kutuchonganisha au wawe na shida ya hela ndio utaona wakipiga simu.
Dah! unabahati sana wengine wangeshafanya yao.
 
Sijapata fursa ya kua karibu na pande zote kiivo ila hamna kibaya, zaidi zaidi tunakutana kwenye events tunabadilishana namba!
 
Binafsi ni mm na mdogo wangu over,cjuagi kama kuna ndugu.
 
Back
Top Bottom