Uhusiano wako na ndugu zako wa baba upo sawa ?

Uhusiano wako na ndugu zako wa baba upo sawa ?

Jinsia yako mkuu
Mtoto wa kiume lazima uwe karibu na asili ya babako ila ujue jinsi ya kubalance na reciprocation ya treatment
Huyo ndo huwa wakifa wanazikwa makaburi ya jumuia na msiba unakuwa wa majirani tu.
 
Sisi kwetu huwezi tofautisha yupi mtoto wa Baba mkubwa, Baba mdogo wala shangazi. Yaani wote tuko pamoja kwenye kila kitu, kuna wakati sikukuu tunaamua kwenda Kula kwa Baba Fulani, wakati mwingine kwa shangazi, wakati mwingine kwa Baba huyu yaani tuko hivo. Tunawashukuru waasisi wetu ( Baba zetu) walijenga bond nzuri Sana tunayoishi nayo mpaka Leo. Uzuri Baba zetu wote wako kijijini na wanaishi jirani hivyo hata MTU anapoenda huko habebi vitu kwaajili ya Baba Yake au mama Yake tu, huwa tunapoenda unajipanga kabisa unabeba vitu/zawadi za familia yote iliyopo kule na ukifika unapokewa vitu vyote vinawekwa nyumbani kwa Bibi na wanafamilia kutoka kila nyumba wanaenda kuchukulia halo, tumejengwa hivo na tuko hivo mpaka leo
Hivi ndio inatakiwa sasa ndio maana ya familia
 
Hauwezi kuwa sawa kama mama alichepuka maana mama mmoja baba mbalimbali ndani ya ndoa moja
 
Kwakweli ndugu upande wa baba sasa hivi ni hamna kitu....... Mm nachojua nishikamanr na ndugu zangu tuliozaliwa na wazee wetu basi!
 
Nimejitahidi kujisogeza lakini naona wapi nimefika mahali jamaa nawategemea sana kuliko watoto hao wazee ndugu nababa
 
Mimi niwe mkweli tu hakuna ndugu upande wa baba amenikosea lakini hatuna mazoea. Sehemu pekee tunayoweza kujuliana hali ni kwenye misiba tu.

Nipo karibu zaidi na upande wa mama. hawa wajomba, kina mama mdogo, watoto zao, n.k. tupo karibu sana.

What's your story?
Wamama wanawafundisha watoto wako, shangazi zenu wachawi, baba zako ni malatili, etc.... watoto wanaserereka humohumo.
 
Miaka kadhaa ya nyuma,haikuwa shwari”

Kwa sasa kila kitu shwari ingawa matatizo hayakosekani kwenye family.
 
Back
Top Bottom