Uhusiano wangu na baba yangu

Uhusiano wangu na baba yangu

Ninachokiona kutoka kwako ni u much know mwingi kwenye fuvu lako. Hizi dini za kuja zinawapogusha Sana vijana na kuona wachungaji na wazee wa kanisa ndio Wazazi wenu. Nina uhakika kuwa Richa ya kuwa umeenda mpaka chuo lakini maisha Yako hayana Amani kisa ujuaji na kukosa ndugu. Baba Yako amekuvumilia Sana licha ya dharau zako unazomuonesha

Sasa dogo, nenda Kwa ndugu ukaombe msamaha na useme kuwa ulimkosea baba Yako. Mpaka Sasa niamini Mimi ya kuwa umeunganishwa na mama Yako. Yaani wanakuona kuwa wewe na mama Yako lenu ni Moja na wanahisi labda mama alikuonesha baba mwingine. Ili kuyaepuka haya na mengine kubali yaishe.
 
Pole, kwakua tayari unafamilia yako, kama unaweza jaribu kuona kama mnaweza kuyamaliza na mzee, maisha haya mafupi sana, ouwekeana vinyongo sio poa
Sasa masharti ya kwenda kuungama makaburini ya nini zama hizi?
 
Baba hata azeeke vipi hawezi kuwa mpumbavu, hata awe na mambo gani ya hovyo hawezi kuwa mpumbavu, tujifunze kutowawekea vinyongo na kupuuza baadhi ya mambo ya mambo yao.

Kikubwa ni kujishusha zaidi na kutoonyesha hasira zako, chuki zako mbele yake kwa kuwa tunahitaji baraka zao zaidi.
Well said. Mimi binafsi nimemueleza mengi hapo juu. Hawa watoto wanapenda sn kuleta ligi hata kwa wazazi wao kwa kuokota ushauri kutoka kwa wenzao waliokwisha shindikana kwa wazazi wao.

Nimekukubali sn kwa ushauri uliompa. Kumbe vijana wenye akili bado mpo nilidhani wamebaki wahuni tu na mashoga kumbe wenye busara bado mpo. Cha ajabu utaona anadharau ushauri wako anachukuwa wa wale wanaomwambia aachane na huyo baba yake yeye akomae kivyake na maisha yake.
 
Kwanza, hakikisha haya uliyoyanena ni ukweli kutoka moyoni mwako;

Pili, ikiwa hayo uliyoyanena ni kweli, ongeza juhudi za kujikabidhi machoni pa Bwana Mungu wa Utatu Mtakatifu afunge kila mlango wa laana itakayo kwa mwanadam.

Tatu, kumbuka adui yako naye kwasasa atakuwa madhabahuni pa miungu aijuayo akiomba mabaya yakupate ili utambue ukuu wake kwako.

Nne, katika sala zako Muombe huyo Baba kwa Mwenyezi Mungu amsamehe lkn nawe pia umsamehe. Muombe na huyo umuitae Mamdogo, kuna uwezekano mkubwa ndiye mwenye pando la ibilisi moyoni mwa Mzee.

Tano, ukifanya sala niliyoisema hapo juu kwa kumaanisha kwa angalau siku 7 mfululizo asbh, mchana na usiku saa 10, anza kumuomba msamaha tena Mzee kwanza katika ulimwengu wa imani kabla ya kumwendea physically. Ukifanya hivyo kwa kumaanisha utajikuta katika ndoto mmefanya majadiliano. Hapo ndipo utakapoanza kujisogeza kwake physically. Kwa sasa usijisogeze haraka, atakudhuru. Usiende!

Sita, ujue tu kwamba wapo watu imewakumba mikasa mikubwa zaidi ya huo dhidi ya wazazi wao. Juzi tu nimeona Video Clip moja Mama mmoja huko kenya anamuonesha utupu wake mtoto wake kwa nia ya kumlaani.

Saba. Kaa nyumbani mwa Bwana.

Mwisho, mhimidi Bwana kwakuwa ni mwema lkn pia fadhili zake ni za milele Zab 117:2
Ushauri mzuri.
 
Mimi ni Mtu mzima wa Miaka 97 mwez wa 8 nafkisha miaka 98, Nakushauri kijana Wangu Achana na huyo baba mpotezee tu hii dunia wte tumekutana tu Hakuna cha Mungu wa pili wala watatu,

Huna baya kam amenyamaza na wew nyamaza Deni la Damu hulipwa kwa Damu, Deni la Shari hulipwa kwa shari,Deni la jeuri hulipwa kwa Jeuri, Jino kwa Jino tu kam hujamkosea usijishushe Na akifa usiende ili iwe fundsho kwa Wapuuz wengne waliobaki.
Akili na umri mkubwa(>80yrs) huwa viko vice versa.
 
Huna tatizo lolote wewe focus na maisha yako ila usiache kumhudumia mzee nyumbani, hakikisha unamrushia kitu kidogo ale na ma' mdogo ajue huna shida naye.
Hapana huyo mama ni mshrikina na ndio anawakoroga ogopa wanao ingilia mambo ya watu
 
Pole kwanza kwa kupitia hiyo experience ambayo si ya kawaida kwa jamii zetu za kiafrika, yaani mzazi kuweka kisasi na mtoto ni jambo la ajabu kama sio nadra kulisikia na tena ukilisikia basi ni mtoto mtukutu asiye na adabu ambae hasikii na ni mkaidi na viburi juu ndipo mzazi hufanya kubwaga manyanga na kumsusa kama sio kumkana kama sehemu ya uzao wake sababu ya kukosa utii na mwenendo mzuri.

Lakini hili lako ni la tofauti na inashangaza sana tena sana eti baba mzazi kumsusia mtoto wake wa kiume kwasababu ameamua kuwa na maisha na maamuzi yake binafsi. Na mbaya zaidi anafikia hatua ya kukugombanisha na ndugu zako wa familia moja na mbaya zaidi anakuongelea mbovu.

Kumradhi kama nitakuwa nimekukera na kauli yangu ila ukweli ni kuwa hapo hauna baba, bali huyo ni mtu ambaye amejitolea kutoa mbegu zake ili wewe uzaliwe.

Baba huwa ni kiongozi rafiki ambaye bila kujali mazingira ni yapi ila haitatokea yeye aharibu mahusiano na mtoto wake kwa sababu yoyote ile na siku zote anabakia kuwa kiongozi na mshauri namba moja kwa mtoto. Huyu uliyenae ni kinyume cha Baba bali ni msela aliyekulea.

Usivunjike moyo, kujisikia vibaya wala kuhisi umepotea njia. Ungekuwa mtu mwenye matatizo usingeweza kuishi vizuri na watu baki hadi wakakusaidia nyakati ngumu za msiba ambapo yule unayemtambua kama baba mzazi ameamua kukuletea upinzani usio na mbele wala nyuma na mbaya zaidi analeta udwanzi wake kwenye swala ambalo hata watu baki wasingeweza kukutenga.

Upo sahihi, hii utaweza kuipima kwa namna umeweza kuishi vema na jamii iliyokuzunguka mbali na familia uliyotokea. Ndugu ni kufaana sio kufanana. Chukua glass ya maji kunywa shusha pumzi. Then futa mawazo ya majuto kuwa kuna mzazi umemkwaza. Muache aishi hayo maisha ya chuki na uhasama hadi uzeeni mwake.

Endelea kujijenga kijamii na watu waliokuzunguka na shirikiana nao vema hao hao kwenye hali na mali. Mzazi wako pia ni binadamu. Wanadamu huwa na visirani vya ajabu nyakati zingine hadi unajiuliza imekuwaje mtu anakuwa na mambo ya ajabu kiasi hicho. Sasa ukiendelea kumstaajabu utaona kama Dunia inakuelemea. Ila ukimpuuza na kumuona mwehu tu then upuuzi wake wowote anaofanya hautakudhuru wala kukuumiza.

Chukulia kama tayari ulishamzika huyo anaekusumbua ni mtu baki au baba mdogo. Unafanya vema sana kumkalia mbali na kumpotezea hii inakujenga kuishi bila kero zake na kujipanga kivyako. Na huo ndio uanaume. Wanasema utaachana na baba na mama yako utashika Tecno yako mkononi utaenda uraini kupambana ukitafuta maisha.

Endelea kujenga ukoo wako na uhakikishe hicho kirusi cha tabia mbovu ya baba yako hakitakuja jirudia kujipandikiza katika uzao wako milele.

Yangu ni hayo tu naomba kuwasilisha.
 
Pole, kwakua tayari unafamilia yako, kama unaweza jaribu kuona kama mnaweza kuyamaliza na mzee, maisha haya mafupi sana, ouwekeana vinyongo sio poa
Umesoma lakini alichokiandika au umetoa tu ushauri boss?
 
Pole sana ikiwa usemayo ni kweli , ila nikuombe kurudi kwa baba yako na umueleze uko tayari kufanya yale aliyokueleza kubali yaishe , huyo ni baba yako .

Najua hukwenda kanda ya ziwa kisa wewe ni mtu wa kanisani so huwezi kwenda kaburini kuomba msamaha kwa bibi yako hivyo husijali kaongee na ndugu zake wa huko yaishe , habari za wewe kwenda kaburini au kutokwenda kaburini hatazijulia wapi na wakati yupo Dar .

Kubali yaishe maana unaonekana una mgogoro wa nafsi juu ya haya mahusiano na baba yako.
Haukusoma alipoandika kuwa siku ya msiba wa bibi yake waligoma kuzika hadi yeye na baba yake waombane msamaha na mzee wake akasema yaishe. Then mzee wake akaliwasha tena ? Kuna wazazi ukiwaendekeza hautafanya maisha yako.

Usiombe haya yakukute unatamani urudishe siku nyuma uombe kubadilishiwa mzazi wa kukuleta duniani.

Haya anayofanya huyu mzee ni mwiko tena marufuku kabisa kwa mzazi kumfanya mtoto wako asotee kupata maelewano na wewe mzazi wake.

Mtoto hanaga ujanja kwa mzazi sasa ni ujinga kwa mzazi kuanza kumtesa mtoto.
 
mama hataki kbs kumskia mzee yuko uko kwao alishaolewa ana maisha yake kwan inasemekana chanzo cha yeye kuachana na mzee ndugu wa mzee wifi zake walimuunganishia mzee kwa dada wa kazi awe mkewe na amuache mama, wkt huo mama alikuwa kaenda kujfungua mdogo wangu wa mwsho aliporud akakuta dada wa kaz katawala mji akaamua kujiondokea tu hakuwahi kurudi tena. Na uyo dada wa kaz ndo ma mdogo nliyemzungumza hapo.
Ona sasa, mzee anaruka na beki tatu. Na anafamilia. Hivi anajielewa kweli huyu mzee?

Inaonekana ukoo wa baba yako ni changamoto, jiweke nao mbali hivyo hivyo, hawana maajabu hao na hakuna kitu watakufanya.
 
Usidanganywe eti una maisha yako. Baba yako siyo mshikaji wako. Hata kiroho ana nguvu sn. Ninachokiona kwako na ambacho baba yako hakukigundua ni umri uliokuwa nao wakati unamaliza form 4. Ulikuwa kwenye kipindi Cha FOOLISH AGE ambacho huambatana na hulka mbalimbali km kujiona mkubwa na mwenye nguvu za mwili kuliko MTU yeyote. Ndiyo maana baada ya kuambiwa uingie kazi ya Police wewe uliamua kuondoka bila kujali impact ya uamuzi wako kwako mwenyewe na kwa baba yako. Kitendo hicho ni dhahiri ulimdharau sn baba yako. Hata km hukutaka kwenda u-police ulitakiwa kuongea kwa upole na staha na baba yako kwa kumshawishi uendelee na masomo na pengine hata kuwatumia ndugu wa baba yako km shangazi na baba zako wadogo au wakubwa au huyo mama yako wa kambo.

Kila mzazi anapenda kuona mtoto wake akifanikiwa. Najua wakati anakuambia uende police huenda kuna kitu alikiona ndani yako. Ila wewe kwa kibri kutokana na foolish age ukamdharau ukaamua kuhama nyumbani. Ukasahau kuwa "running away from a problem is not a way of solving a problem".

Km ni mimi hapo usingerudi milele. Ifike wakati tujue wazazi siyo wake wenza au sawa na mawifi kila mara kusuguana kwa maneno. Yakupasa kumsikiliza mzazi wako, penye shida unatufuta njia sahihi siyo kumuonesha kibri kuwa hata bila yeye wewe mwenyewe unasonga mbele. Huo ni ukosefu wa nidhamu na maadili. Leo ni mzima unaongea kwa kibri ipo siku unaweza kumuhitaj kwa lolote na ndiyo maana hata wakati unaomba mkopo Bidi ya elimu ya juu ulitumia jina lake km unajiona baba yako siyo kitu Wala lolote kwa nini usingeandika hata jina la mjomba wako kwenye hizo form za mkopo.

Mimi km mtu mzima nakushauti nenda kamuombe baba yako msamaha hata km unaona huna kosa, yeye analiona na hata mimi nineliona. Vijana msijianye wa mjini sana au kujitia ujuaji wa kipuuzi kwa sababu za marafiki waliokosa maadili ya wazazi wao, mtapotea. Hata uwe na elimu kiasi gani au mali kiasi gani hivyo vyote havijawahi kumzika mtu.

Alafu eti unajinasibu kuwa wewe ni mhitimu chuo kikuu. Chuo kikuu gani hicho ambacho huwezi kutumia intellects zako ku-solve mambo madogo km hayo hadi unakimbilia mitandaoni.

Usidharau maneno yangu, what goes around comes around. Na ukishupaza shingo kwa kuokoteleza ushauri wa humu wa baadhi ya watu wanaokusapiti ipo sku utakuja kujuta na tayari itakuwa too late. Take care.
Dahhh umeongea kama Baba

Embu amsikilize huyo mama.
 
Huu sio ushauri mzuri hata kidogo na sitoshauri muhusika aufanyie kazi.

Hii mifumo ya kikoloni ya kuwapa wazazi u'Mungu mtu hata pale pasipostahili imepelekea kuvuruga vijana wengi sana kuishi maisha nje ya rada zao.

Sasa wewe unataka nambia huyu kijana hana maisha yake kwasasa?!

Kwann baba yake atake kijana wake awe polisi ya lazima?! Ndio maana tuna askari wasiotendea haki hii kazi halafu tunawalaumu kumbe ni matokeo ya kuwa na mitazamo kama hii ya kutii wazazi hata pale isipostahili kuwapa utii.

Mzazi anapewa hadhi ya MUNGU wa pili Duniani endapo atakuwa ni mtu wa hekima, subira, upendo, kiongozi, mshauri na msimamizi mzuri kwa kijana au binti yake.

Sio mzazi analeta bangi wewe unasema mtu ahangaike nae. Mtu kama hakukua vizuri au amelelewa makuzi yankudeka deka ndio iwe haki yeye kusumbua wengine eti kisa ni mtoto wake, THAT'S NONSENSE TOP MOST.

Ingekuwa huyo mzazi yupo sahihi basi huyo kijana asingekuwa na maisha. Mtu kapotea miaka 5 yote na ana maisha yake mazuri tu shida ni nini sasa.
 
Kwanza, hakikisha haya uliyoyanena ni ukweli kutoka moyoni mwako;

Pili, ikiwa hayo uliyoyanena ni kweli, ongeza juhudi za kujikabidhi machoni pa Bwana Mungu wa Utatu Mtakatifu afunge kila mlango wa laana itakayo kwa mwanadam.

Tatu, kumbuka adui yako naye kwasasa atakuwa madhabahuni pa miungu aijuayo akiomba mabaya yakupate ili utambue ukuu wake kwako.

Nne, katika sala zako Muombe huyo Baba kwa Mwenyezi Mungu amsamehe lkn nawe pia umsamehe. Muombe na huyo umuitae Mamdogo, kuna uwezekano mkubwa ndiye mwenye pando la ibilisi moyoni mwa Mzee.

Tano, ukifanya sala niliyoisema hapo juu kwa kumaanisha kwa angalau siku 7 mfululizo asbh, mchana na usiku saa 10, anza kumuomba msamaha tena Mzee kwanza katika ulimwengu wa imani kabla ya kumwendea physically. Ukifanya hivyo kwa kumaanisha utajikuta katika ndoto mmefanya majadiliano. Hapo ndipo utakapoanza kujisogeza kwake physically. Kwa sasa usijisogeze haraka, atakudhuru. Usiende!

Sita, ujue tu kwamba wapo watu imewakumba mikasa mikubwa zaidi ya huo dhidi ya wazazi wao. Juzi tu nimeona Video Clip moja Mama mmoja huko kenya anamuonesha utupu wake mtoto wake kwa nia ya kumlaani.

Saba. Kaa nyumbani mwa Bwana.

Mwisho, mhimidi Bwana kwakuwa ni mwema lkn pia fadhili zake ni za milele Zab 117:2
Naomba unisaidie. Katika huo msamaha anatakiwa kusema maneno gani?!

"Baba naomba unisamehe kwa kukataa upolisi" au anasemaje?
 
Back
Top Bottom